Relationship is a team work, wanawake msiyachukulie mahusiano kama sehemu ya kutatua matatizo yenu ya kiuchumi

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,273
7,362
I hope everyone is fine,

Mahusiano yeyote ili yaweze kufanikiwa inabidi pande zote mbili ziwe na ushirikiano, ila hali ni tofauti kabisa kwa asilimia kubwa ya wanawake tulio nao, wamegeuza mahusiano kama ndo kitega uchumi kikuu kwao.

Kwa dunia ya sasa sio swala la ajabu kukuta mwanamke akiwa na wanaume zaidi ya watano na kote huko akiwa na lengo moja tuu la kuchuma.

Ndoa nyingi zinayumba sababu ya hili kundi kubwa la wanawake wasiojua majukumu yao katika mahusiano na ndoa kwa jumla na badala yake wanakua wanalenga kwenda kupata pumziko la kiuchumi, na kuwaachia wanaume mzigo mkubwa wa kuendesha familia.

Malalamiko mengi ya wanawake katika mahusiano ni kuhusu wanaume kutowapa fedha ,na kutotatua shida zao tuu, lakini hawataki kukubaliana na ukweli kwamba , ili waweze kuhudumiwa 100% ,inabidi na wao wafanye majukumu yao kama inavyopaswa ili kujenga mahusiano imara.

Wanaume wengi wanaishia kwenye msongo wa mawazo na kutofurahia maisha ya ndoa kutokana na baadhi ya wanawake wabinafsi wasiotaka kujiongeza na kusubiri kufanyiwa kila kitu.

Kwa dunia ya leo ukiweza kuepukana na aina hii ya wanawake ,utaishi maisha ya amani na furaha siku zote.
 
I hope everyone is fine,

Mahusiano yeyote ili yaweze kufanikiwa inabidi pande zote mbili ziwe na ushirikiano, ila hali ni tofauti kabisa kwa asilimia kubwa ya wanawake tulio n

Kwa dunia ya leo ukiweza kuepukana na aina hii ya wanawake ,utaishi maisha ya amani na furaha siku zote
Soma vizuri vitabu vya dini unayoiamini utakuta kumtunza mke ni jukumu la mume.

Sasa acha kulialia, ukimpata ambaye na yeye ana income mkae chini wekaneni sawa kwamba kwenye nyumba utafanya abcd na yeye akusaidie efg maisha yanakwenda.

Tatizo mnaogopa kuongea na wake zenu mnakuja kuwasimanga hapa JF.

Mimi kwangu habari sijui za gesi ya kupikia shopping za watoto na mambo madogomadogo huwa sihusiki nayo, nadeal na viti vya kiume, lakini hii pia inategemea mke wako anafanyakazi? Au ana source of income?

Kulialia will not help you, vunja ukimya sema naye.🙏🙏
 
Soma vizuri vitabu vya dini unayoiamini utakuta kumtunza mke ni jukumu la mume.

Sasa acha kulialia, ukimpata ambaye na yeye ana income mkae chini wekaneni sawa kwamba kwenye nyumba utafanya abcd na yeye akusaidie efg maisha yanakwenda.

Tatizo mnaogopa kuongea na wake zenu mnakuja kuwasimanga hapa JF.

Mimi kwangu habari sijui za gesi ya kupikia shopping za watoto na mambo madogomadogo huwa sihusiki nayo, nadeal na viti vya kiume, lakini hii pia inategemea mke wako anafanyakazi? Au ana source of income?

Kulialia will not help you, vunja ukimya sema naye.
Mkuu mantinki yangu ni hiyo hiyo kuwa lazima na mwanamke awajibike ...
 
Mkuu mantinki yangu ni hiyo hiyo kuwa lazima na mwanamke awajibike ...
Ili mwanamke awajibike timiza kwanza wajibu wako wote kikamilifu na hasa ule wa kitandani.

Kwa kawaida mwanamke ana masikio matatu, haya mawili unayaona anakusikiliza lakini bila kulizibuwa vizuri sikio la tatu hawezi kukusikiliza vizuri, do ur home work.

Angalia hii video hapa chini, ni mb chache tu usiskip.
 
Attachments

  • VID-20211026-WA0006.mp4
    9.8 MB
Choose wisely, ukiona mwanamke anajivua responsibility kwenye maisha yake achana nae mazima tafta mwanamke ambaye anapenda kushirikiana katika kujijenga!

Wanawake aina hii wengi tunawa overlook tu! Aina hii hawabandiki makope, makucha na wanapenda kujishughulisha zaidi na kuongea future!
 
Hao sasa ni wakutafuta kwa binoculars, sisi ndio tupo.....😂😂😂
 
Ili mwanamke awajibike timiza kwanza wajibu wako wote kikamilifu na hasa ule wa kitandani.

Kwa kawaida mwanamke ana masikio matatu, haya mawili unayaona anakusikiliza lakini bila kulizibuwa vizuri sikio la tatu hawezi kukusikiliza vizuri, do ur home work.

Angalia hii video hapa chini, ni mb chache tu usiskip.
Hako kadingi kwenye video hadi kanaona aibu.😂😂
 
Back
Top Bottom