Rekodi zilizowekwa kwenye hatua ya Makundi Kombe la Dunia Qatar 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
Hatua ya makundi ya kombe la Dunia ilikamilika jana huku huku Cameroon ikiaga mashindano kishujaa kwa kuibamiza Brazil 1-0 katika dimba la Lusail.

Baadhi ya rekodi zimewekwa na zingine kuvunjwa.

1. Vincent Aboubakar amekuwa mchezaji wa kwanza tangu Zinedine Zidane 2006 kufunga goli na kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mechi moja ya kombe la Dunia.

2. Kwa mara ya kwanza tangu 1994 hakuna timu iliyoshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi ya kombe la Dunia.

3. Cameroon imekuwa Taifa la kwanza kutoka Afrika kuifunga Brazil kwenye historia ya kombe la Dunia.

4. Cameroon imevunja rekodi ya unbeaten ya Brazil tangu ilipofungwa na Argentina katika fainali ya Copa America huku ikivuruga mwenendo wa Brazil wa ushindi mechi 9 mfululizo.

5. Vincent Aboubakar sasa amefunga magoli 10 kwenye michuano mikubwa ndani ya mwaka 2022. Magoli 8 kwenye AFCON 2022 na magoli mawili kwenye kombe la Dunia 2022.
 
Hatua ya makundi ya kombe la Dunia ilikamilika jana huku huku Cameroon ikiaga mashindano kishujaa kwa kuibamiza Brazil 1-0 katika dimba la Lusail.

Baadhi ya rekodi zimewekwa na zingine kuvunjwa.

Vincent Aboubakar amekuwa mchezaji wa kwanza tangu Zinedine Zidane 2006 kufunga goli na kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mechi moja ya kombe la Dunia.

Kwa mara ya kwanza tangu 1994 hakuna timu iliyoshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi ya kombe la Dunia.

Cameroon imekuwa Taifa la kwanza kutoka Afrika kuifunga Brazil kwenye historia ya kombe la Dunia.

Cameroon imevunja rekodi ya unbeaten ya Brazil tangu ilipofungwa na Argentina katika fainali ya Copa America huku ikivuruga mwenendo wa Brazil wa ushindi mechi 9 mfululizo.

Vincent Aboubakar sasa amefunga magoli 10 kwenye michuano mikubwa ndani ya mwaka 2022. Magoli 8 kwenye AFCON 2022 na magoli mawili kwenye kombe la Dunia 2022.
Cameroon this,Cameroon that! So where are they?
That's bullshit!! Africa tumerogwa
 
Tayari Vincent kashasema anataka kuja kuichezea yanga ,maana ndoto zake kuichezea timu kubwa ya kihistoria nchin Tanzania....
Inawezekana kabisa kama wamechukua mchezaji kutoka Newcastle hawawezi mshindwa huyo
 
Back
Top Bottom