Rekebisha haya kuondoa uwakilishi haramu!

mnombesa

Member
Jan 28, 2019
11
9
KATIBA NA SHERIA YA UCHAGUZI zalilia marekebisho mengi!
Tangia chaguzi za mfumo wa vyama vingi vya siasa 1995 hatujawahi kuwa na chaguzi huru na haki!

Wapigakura hutimiza wajibu wao lakini sheria hazitimizi wajibu wake.

Maeneo yafuatayo yanalilia marekebisho :-
Tume ya uchaguzi isiongozwe na Jaji wa aina yoyote ili kukidhi mahitaji ya kikatiba ya kuondoa migongano kati ya mihimili mitatu ya dola ambayo ni mahakama, watendaji na bunge.

Ushiriki wa Jaji uliomo kwenye katiba unaondoa uhalali wa tume kwa kukiuka ibara ya katiba inayokataza mwingiliano tajwa.

Uwakala wa serikali za mitaa kupitia wakurugenzi wake tayari kumetenguliwa na mahakama lakini hadi leo Tume ya uchaguzi haijateua wasimamizi wake wa uchaguzi wa majimbo ya uchaguzi ikiashiria hawana mpango wa kuzingatia maamuzi ya kimahakama.

Usafirishaji wa matokeo ni eneo pana ambalo hutoa mwanya mkubwa wa kughushi kwa kubadilisha fomu na kubandika fomu haramu jinsi wanavyowadhulumu wapigakura.

Matumizi ya tekinolojia ya KIMS KIT ndiyo muarobaini wa wizi wa kura wa kubadilisha matokeo. Kwenye uchaguzi wa 2015 jimbo la uchaguzi la TAHIMBA, NEC walitangaza matokeo batili yaliyotokana na fomu iliyoghushiwa kwenye uchaguzi wa Rais na walishinikizwa kurekebisha pale walipoona kwenye mitandao fomu halali kivuli chake kiko kila kona.

Matokeo ya majumuisho ya kura za majimbo hayawi na vivuli vya fomu zake na fomu za majumuisho ya vituo vyake vya kupiga kura. Huu ni mwanya mkubwa wa kuiba kura kwa kuwanyima wapigakura nafasi ya kukagua kama fomu zilizowakilishwa NEC ni sahihi na kama zimejumlishwa ipasavyo.

Matokeo yote ya uchaguzi yatangazwe ndani ya masaa 48. Kulingana na tekinolojia ya KIMS KIT hatuna tena visingizio vya mwaka 47 vya Nchi ni kubwa, hakuna usafiri, barabara mbovu, kazi kubwa ya kujumlisha au fomu hazijatufikia ili tuyatangaze matokeo. KIMS KIT tekinolojia inatumia solar haihitaji purukushani za tetema ya Tanesco.

NEC walirudisha mabilioni Hazina huku hawajanunua KIMS KIT kwa madai ya kipuuzi hayakuwemo kwenye bajeti yao lakini Biometric registration equipment walizonunua nyingi kulingana na taarifa za CAG zilikiuka taratibu za manunuzi na mbovu au haziwezi kufanya kazi kwa kutofautiana na mfumo mzima wa Tehama wanaoutumia na hakuna hata mtumishi mmoja wa NEC aliyefikishwa mahakamani na kuthibitisha kuna mahusiano yasiyo na lishe kati ya watawala na dola.

Mamlaka ya Spika ya kuwanyang'anya wabunge yanatumika vibaya na hayathibitiwi na taasisi yoyote ile. Hivyo basi kuwatendea haki wapigakura mamlaka hayo anyang'anywe na kupewa wapigakura wenyewe kwa kukusanya sahihi zao na zikifika theluthi moja kwa sababu yoyote ile uchaguzi urudiwe.

Wapigakura siyo spika wa Bunge ambaye hakujiandikisha kama mpigakura wa Jimbo husika na wala hakupiga kura kwenye jimbo husika kupewa mamlaka makubwa ya kuwafuta ubunge wapinzani tu ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya utu na ya kidemokrasia.

Bunge likatazwe kuwasimamisha wabunge kwa sababu zozote bila kupeleka malalamiko yao mahakama kuu na shauri husika kuamuliwa kimahakama.
 
Unaandika vitu vya msingi Sana mleta Uzi,Mungu akubariki.lkn uzi wako wa pili huu wachangiaji wanachelewa.
 
Back
Top Bottom