Reincarnation: Could it be real? (Kuzaliwa upya inawezekana kuwa kweli?)

Wickama

JF-Expert Member
Mar 8, 2009
1,466
1,194
Almost half of the global population believes in the concept of re-incarnation. This is a belief of the soul re-living the physical life after the death of an individual. The form and status of the new life is said to depend on one's deeds in the former life. This belief is wide spread in the Indian sub-continent and other oriental religions.

Considerable efforts have been made to investigate truthfulness of accounts of especially children who recounted their past lives. The majority of these cases are reported to have been corroborated as being consistent/matching with people who described by the investigated subjects.

In this video, some of the investigator are sharing their findings. Please share your thoughts after listening to the video. Could this be real?





-----------
Cryptopotato anasema..,

Wengi tumekuwa tukifikiria kunamaisha baada ya kifo kulingana na imani zetu namafundisho tuliyopewa kuanzia watoto.Mmoja anaweza kudai mafundisho yake ni bora kuliko aliyo yapata mwingine kwasababu ya imani yake juu ya hayo mafundiaho ambayo ameaminishwa kwa kurithishwa na wazazi, kufuata mkumbo au uoga wa kujifunza cha mwenzake akiwa na akili ya wazi(open mind).

Tunaamini binadamu ni kiumbe wapekee na tofauti sana na wengine waiyopo hapa duniani.wengi wanasema ameumbwa kwa mfano wa muumbaji wa kila kitu na kupewa akili za ziada ili atunze viumbe wengine.lakini je muda wake unapoisha duniani roho ambayo ndiyo inabeba ufahamu wa mtu inaenda wapi?

Kuna kitu kinaitwa reincarnation(roho kurudi upya duniani baada ya kifo) ambapo roho ya mtu aliye fariki itarudi tena duniani baada ya muda mrefu na atazaliwa kama mtu mwingine huku mara nyingi akiwa hakumbuki chochote cha nyuma, labda mpaka pale siku inayo subiriwa na wengi itakapo wadia(siku ya hukumu).

Lakini kuna story za watoto wadogo waliokuwa kidai kwamba walikuwa watu flani katika maisha yao ya za mani kabla hawajafariki na kuzaliwa upya duniani na wengi wamekuwa wakielezea story za maisha ya hao watu wanaodai walikuwa ni wao kwa usahihi mkubwa mpaka kuwa ogopesha ndugu waliobaki wa hao marehemu.

Je, kama haya haya tu na yaona kwa macho kuna ukweli kuhusu roho kurudi duniani baada ya kifo?

Baadhi ya story za reincarnation(roho kurudi duniani baada ya kifo hizi hapa)


---------
mareeTZ anasema..,

Reincarnation ni falsafa na Imani iliyojengeka toka enzi na enzi inayoamini kuwa baada ya kifo cha mwili au roho, nafsi ya mwanadamu huanza tena maisha mengine katika mwili mpya hapa hapa duniani. Neno reincarnation limetokana na lugha ya kilatini likimaanisha "kuingia tena katika mwili". Imani hii huaminiwa sana na waumini wa dini ya hindu kutoka nchini india, na dini nyingine za zamani kama theosophy, spiritism pamoja na eckankar pia zipo baadhi ya jamii na makabila makubwa nchini Australia, asia mashariki, Siberia na America ya kusini ambayo pia huamini sana Imani hii.

Katika jamii ya zamani ya ufalme wa farao nchini misri pia kulikuwa na Imani ya maisha baada ya kifo ambapo wafalme wote waliokuwa wakizikwa katika mapiramidi walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya maisha baada ya kifo, kwa kuzikwa na fedha ,manukato,nguo na vitu mbalimbali kwa Imani kuwa kuna maisha baada ya kifo.

Matukio mengi yametokea duniani na kupelekea watu wengi kuanza kudadisi juu ya ukweli wa Imani hii ya kuishi tena hapa dunianai baada ya kifo (reincarnation). Baadhi ya matukio kadhaa yameripotiwa yakihusisha kumbukumbu za maisha ya nyuma kabla ya mtu kuzaliwa, alama mbalimbali katika mwili na ulingano wa tabia tofauti baina ya waliofariki na waliozaliwa. Na wengine kuzaliwa wakiwa na uwezo wa kuzungumza lugha Fulani.

Tukio moja linalohusisha ukweli juu ya Imani hii ni la kijana Tarajit sing amabaye anaishi katika kijiji cha alluna miana. Tangu akiwa na miaka miwili Tarajit Singh amekuwa akidai kuwa jina lake la kweli ni Satman singh na alizaliwa kijiji cha chakkchela kilomita 60 kutoka kijiji chao

Taranjit anadai anakumbuka alikuwa mwanafunzi wa darasa la 9 akiwa na miaka 15 au 16 na jina la baba yake ni Jeet singh, na anakumbuka aligongwa na pikipiki akiwa anaendesha baiskeli na kufariki septamba 10 1991, Anakumbuka pia siku ya ajali alikuwa amebeba daftari zake ambazo zililowa damu huku akiwa kiasi cha rupii kumi mfukoni. Baadaye wazazi wake walianza uchunguzi ambapo mwalimu mmoja katika mji wa Jalandhar alithibitisha kijana aitwaye satman alifariki katika ajali na baba yake anaitwa jeet singh. Baba wa tarajit alisafiri hadi kwa wazazi wa Satman ambao walithibitisha kifo cha mwanao pamoja na kuonesha zile daftari zenye damu na zile rupii mfukoni.

Baada ya tukio lile mwanasayansi Vikram raj Chauhan alichukuwa daftari za Satman zenye damu pamoja na daftari za Taranjit ambapo baada ya vipimo ilionekana miandiko yao inafanana kwa kila kitu.

View attachment 432833

Tukio lingine linamuhusisha John Mcconnell aliyepigwa risasi mara sita na kufariki mwaka 1992 na kuacha binti mmoja aitwaye Doreen. Baadaye mwaka 1997 doreen alijifungua mototo wa kiume aliyemuita William. William alizaliwa na tatizo la mshipa mkubwa ya kushoto moyo kushindwa kupeleka damu katika mapafu huku baadhi ya mirija ikiwa imekaa vibaya baada ya tiba na upasuaji kadhaa alipona. Wakati john mcconell anapigwa risasi mara 6 risasi moja iliingia katika mapafu na nyingine katika mshipa mkubwa wa kushoto wa moyo. Tukio lililohusihswa na ugonjwa aliozaliwa nao William.

Siku moja wakati Doreen anataka kumchapa willian, willian alimwambia Doreen ulipokuwa msichana mdogo mimi nilikuwa baba yako, ulikosea mara nyingi na wala sikukuadhibu. Baada ya tukio hilo William aliendelea kumdadisi mama yake kuhusu familia jambo lililoshangaza , alimuuliza Doreen kuhusu paka ambaye Doreen alikuwa anamfuga kipindi akiwa binti mdogo , William akamtaja yule paka kwa jina la boss na cha kushangaza ni john mcconnell pekee ndiye alikuwa akimuita yule paka jina lile akifupisha kifupi cha jina lake boston.

Willian pia aliweza kutaja siku aliyozaliwa (jumanne ) na siku john mcconnell aliyofariki ya alhamisi, na alitaja siku hizi akiwa bado mototo mdogo hata hajajua majina ya siku. Anadai siku ya jumanne( ambayo ndiyo alizaliwa ) aliambiwa na mungu kwamba alikuwa tayari kurejea tena. Matukio haya mawili pamoja na mengi ya namna hii yaliyoripotiwa yameacha maswali mengi vichwani mwa watu bila ya majibu.
--------------------------

Pia soma => Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile
 
Last edited by a moderator:
Reincarnation si ndio ile unaweza ukafa huku Tanzania ukaenda kuzaliwa sehemu nyingine kama mbwa au mnyama mwingine, ama?! hiyo concept kwa kweli hainiingii akilini...
 
Reincarnation is the religious or philosophical concept that the soul or spirit, after biological death, can begin a new life in a new body.

Recently, a number of cases have been investigated using scientific methods to determine truthfulness of the claims.






mkuu hii kitu ni pasua kichwa ubongo nje ndani kuielewa
naomba niulize kidogo
katika sayansi wanasema spirit/soul ni nini ?

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Reincarnation si ndio ile unaweza ukafa huku Tanzania ukaenda kuzaliwa sehemu nyingine kama mbwa au mnyama mwingine, ama?! hiyo concept kwa kweli hainiingii akilini...

Mkuu, ndio hiyo. Wenzetu wanapokuwa wanyenyekevu ni pamoja na kujipandisha daraja akizaliwa upya awe mtukufu zaidi. Akifanya madhambi basi anaamini anaweza kuzaliwa tena akiwa hata jongoo
 
mkuu hii kitu ni pasua kichwa ubongo nje ndani kuielewa
naomba niulize kidogo
katika sayansi wanasema spirit/soul ni nini ?

.made in mby city.

Mkuu hii kitu kwa mbali inafanana na ile desturi iliyokuwapo hata huku kwetu kwamba mtoto mchanga hapati kwa mfano haja hadi anapoitwa jina la mkuu fulani wa zamani
 
Majinni si nayo ni Maislam kama wewe. Kumbe wanayo yaamini hawana imani bali wana dini. I can see the logic here.
Watafiti wazungu, wanaoamini reincarnation, buddhits and hindusts siioni role ya uislamu hapa
 
Watafiti wazungu, wanaoamini reincarnation, buddhits and hindusts siioni role ya uislamu hapa

"I did not create the Jinn and mankind except to worship Me." (Quran 51:56)

"Say (O' Muhammed): It has been revealed to me that a group of Jinn listened and said; ‘Indeed we have heard a marvelous Quran. It guides unto righteousness so we have believed in it, and we will never make partners with our lord'."(Quran 72:1-2)
 

"I did not create the Jinn and mankind except to worship Me." (Quran 51:56)

"Say (O' Muhammed): It has been revealed to me that a group of Jinn listened and said; ‘Indeed we have heard a marvelous Quran. It guides unto righteousness so we have believed in it, and we will never make partners with our lord'."(Quran 72:1-2)


Umeshasikia neno OBSESSION? Wanalitafsiri kama

an idea or thought that continually preoccupies or intrudes on a person's mind
 
Reincarnation si ndio ile unaweza ukafa huku Tanzania ukaenda kuzaliwa sehemu nyingine kama mbwa au mnyama mwingine, ama?! hiyo concept kwa kweli hainiingii akilini...


Pia unaweza ukazaliwsa binadamu ila mtukufu zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom