Regnald Mengi na Mdawa ya kulevya!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Wana JF nimekuwa najaribu kusubiri nisikie majibu ya uchunguzi unaofanywa na PCCB na Jeshi la polisi kuhusiana na matamshi ya Mengi kuwataja Viongozi katika sekta ya usalama wa nchi yetu na watu mbali mbali kuwatuhumu kwamba wameshiriki katika njama za kumchafua kumbambikiza mwanae madawa ya kulevya.

1. Naomba kuuliza kama kuna mtu anafununu kama matokeo yeyote ya uchunguzi yametolewa?

2. Kama bado kwanini wanachelewa kupata ukweli hasa ukichukulia bwana mengi alisema ana ushahidi? binafsi nahisi huu ushahidi ungerahisisha sana kazi ya uchunguzi

3. Je hawa viongozi waliotajwa wamemshtaki?, hasa ukichukulia kwamba amewachafua sana majina yao maana aliwataja kwa majina.

4. Ikiwa ni kweli aliyoyasema Mengi, je kuna umuhimu wa kurudia kufanya uchunguzi wa kesi za watu woote waliokamatwa na madawa ya kulevya kwani yaweza kuwa walionewa lakini hawana uwezo kama wa Familia ya Mengi kuikwepa hii fitina.

Naomba mwenye updates zozote anijaaliye maana nasubiri sana kuona Mengi anashitakiwa kwa kuwachafua Viongozi ya serikali yetu tukufu au Serikali yetu tukufu inajiuzuru kwa kuweka watu wanaoweza kununuliwa kukandamiza wananchi kinyume na matarajio ya Wananchi.
 
Back
Top Bottom