Regional Per Capita GDP: Hii ndio Mikoa 7 ambayo Wananchi wake wana kipato cha Uchumi wa kati Tanzania Bara

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,905
Habari zenu wadau!

Mwaka 2020 tulitangaziwa Tanzania kusajiliwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake wamefikia kiwango cha Uchumi wa Kati wa chini yaani Lower Middle Income Country.

Hesabu hiyo huwa inazingatia GNI per Capita Income ambayo ina range Kati ya $1'036-$4,045 ,,ambapo kwa Tanzania hapa ni mikoa michache Sana ambayo wananchi wake ndio wako Uchumi wa Kati,yaani wenye kipato kuanzia milioni 3 kwenda juu.

Ifuatayo ni orodha ya mikoa 7 ambayo wananchi wake Wana mapato yaliyofikia hicho kigezo cha Uchumi wa Kati, pato la kila mwananchi kwenye mkoa husika limeanishwa.

Regional Per Capita GDP at Current Market Prices,Tanzania Mainland, financial year 2019.Figures in Million TZS

1. Dar es Salaam (4,529,876)

2. Iringa (3,868,283)

3. Mbeya (3,675,999)

4. Kilimanjaro (3,302,915)

5. Ruvuma (3,288,252)

6. Arusha (3,198,260)

7. Njombe (3,073,361)

Sambamba na hiyo kuna Mikoa 5 iliyopo mkiani ambayo hali ya vipato kwa wananchi wake ni mbaya sana,mikoa hiyo ni;

1. Shinyanga (1,857,610)

2. Tabora (1,740,554)

3. Dodoma (1,677,901)

4. Singida (1,578,040)

5. Kagera (1,143,992)

MY TAKE;

Hongera Sana wachapa Kazi wa Nyanda za Juu Kusini.

ANGALIZO,

Kwa kweli hali za sisi wananchi ni mbaya, Serikali ijitahidi kuwekeza kwenye uchumi wa watu la sivyo tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya maana na kasi ya kuzaliana ni kubwa mno. Ikumbukwe Tanzania ni kati ya nchi 5 zenye idadi kubwa ya watu na pia zenye idadi kubwa ya maskini barani Afrika.

SOURCE-TANZANIA IN FIGURES 2019.(pg 50-53)

CREDITS-National Bureau of statistics,Ministry of Finance and planning, 2020.
View attachment 1773908
 

Attachments

  • Tanzania_in_Figures_2019.pdf
    3.2 MB · Views: 39
Hata Kagera? Mkoa uliobarikiwa kila aina ya mazao; evergreen everywhere unakosaje kuwa kwenye list ya 10 bora?
Kweli evergreen kama zote lakini nakumbuka Mwaka jana nilinunua ndizi mikungu miwili ya nguvu Kagera kwa shilingi 1600 yaani watu wanavuna huko lakini mikoa inayokuja kupata faida ni kule mazao yanapopelekwa na sio wakulima wenyewe.
 
Kuwa makini
Kataja mikoa Saba
Wewe umejuaje km kagera haipo top ten?
Poor analytical skills! Kagera iko mwisho (ya 5) kwenye list mikoa ambayo "hali zao ni mbaya sana". This means, hiyo list ya mikoa ambayo hali zao ni nzuri hata ungei-extend hadi 10 kwa kuongeza mikoa yenye nafuu bado Kagera haiwezi kuwemo!

Mwanao (Alice) kawa wa 50 darasani katika darasa la wanafunzi 50 na inaeleweka hivyo. Orodha ya wanafunzi 5 bora imetolewa kwa ajili kupongezwa. Watu wanashangaa jamani mbona Alice ana akili sana imekuwaje hata 10 bora hayumo? Juha mmoja anauliza mmejuaje kuwa hajawa wa 10 wakati wametajwa watano tu wa kupewa zawadi? Wa 50 kati ya 50 anawezaje kuwa wa 10 hata kama 10 bora hawajatajwa? Kagera si imetajwa ya mwisho kwenye hiyo list? Na Tanzania Bara ina mikoa mingapi? Simple logic!
 
Kweli evergreen kama zote hizo lakini nakumbuka Mwaka jana nilinunua ndizi mikungu miwili ya nguvu Kagera kwa shilingi 1600 yaani watu wanavuna huko lakini mikoa inayokuja kupata faida ni kule mazao yanapopelekwa na sio wakulima wenyewe.
Duh! Wakulima wanaumizwa sana kwa kweli! Sijui nini kifanyike kuwakomboa babu na bibi zetu huku vijijini!
 
Back
Top Bottom