Regional News

..nimeona habari hii toka Liwale-Nachingwea.

..very interesting kujua nini kinaendelea Southern Tanzania.

Habari Leo said:
LIWALE ILE SI YA SASA, KUMEPAMBAZUKA.

LIWALE wilaya ambayo ilianza rasmi Julai 7, 1975 baada ya kumegwa kutoka Nachingwea ni moja ya majimbo ya uchaguzi yaliyo Kusini mwa Tanzania yenye historia ndefu ya kukwama kimaendeleo.

Lakini kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita Liwale ile si Liwale ya leo, zipo sababu na Beda Msimbe anazipitia kwa kuangalia maneno ya wakazi wenyewe wa Liwale.

MBUNGE wa Liwale Hassan Chande Kigwalilo anapenda kuamini kwamba amelisaidia sana jimbo lake kuwa pale lililopo kwa leo, kutazama upya dira yake ya maendeleo na kusafisha barabara kwa ajili ya ustawi.

Hayuko peke yake, diwani wa viti maalumu Anna Marianus Simba kutoka Liwale B naye anasema Liwale sasa imechangamka, programu za maendeleo kuanzia elimu hadi kilimo zinatia moyo huku miundombinu inayoimarika katika barabara ikiwahakikisha kutokuwa mbali na soko la mazao.

Mkulima na mfugaji Omar Mshamu Libuka anasema hakutarajia katika maisha yake kuwa na uwezo wa kulisha maziwa wengine, na yeye kutumia ng'ombe ambao amepatikana kutokana na mradi wa halmashauri ya Liwale ya kuibua miradi, kubadilisha maisha yake.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Liwale, Salvinus Kilowoko anasema katika kipindi cha miaka miwili mitatu hata watumishi wanaofika na kuondoka wamepungua sana, wengi wakifika wanaamua kukaa.

Mwanamke Zainab Mohamed Aziz yeye anasema kwamba kama kuna wakati alifikiri serikali imemjali ni wakati ilipomuwezesha kupata ng'ombe wa kufuga na kusema kumbe maisha bora kila mtu yanawezekana kwa kuthubutu.

Naam, kila mtu anaweza kusema lake kuhusu Liwale katika kipindi cha miaka miwili mitatu iliyopita. Pamoja na kufanikiwa katika programu zake wanafunzi wa shule ya sekondari ambayo ni ya mfano ya Liwale wao walilalamikia ufinyu wa mabweni yao, na kwamba nafasi ya kujitanua hawana, wenzao wengine wanalala chini. Ofisa elimu wa wilaya Amos Kabura alisema kwamba kuna wakati walitamani kuifunga hosteli hiyo kwa kuwa ilikuwa inakosa wanafunzi.

Hosteli hiyo ilijengwa mahsusi kusaidia watoto wa kike na safari ndefu za kufuata masomo. Mhandisi wa barabara Liwale, injinia Stafford Buhoma anasema kwamba kwa sasa Dar-Liwale ni safari ya siku moja ingawa miaka mitatu iliyopita hali ilikuwa mbaya sana.

Miaka kadhaa iliyopita Benki ya NMB, benki pekee iliyopo Liwale, ilifikiria kufunga tawi lake kutokana na kuyumba kwa mawasiliano lakini kwa sasa wazo hilo halipo kwani mawasiliano ya Siwaya na mengine ya kimtandao yapo na huduma mpaka za ATM zinapatikana. Liwale kwa kuiangalia inakua, inakomaa na inaonyesha matumaini, anasema mwanadada mmoja ambaye alitaka atambulike kwa jina la mama Marko.

Mkuu mpya wa wilaya, Paul Chiwile anasema: "Kawaambie huku kumekucha na mambo mengi sasa yanawezekana, sio kama zamani eti hakuna usafiri, sisi tupo mjini . Alisema kwa kujiamini na kweli wapo mjini hasa kipindi hiki ambacho kupitia Nachingwea ni bomba na huku njia ya Liwale-Nangurukuru ikiwa inachongwa. Njia hii itapunguza mwendo kwa karibu nusu na badala ya kupitia Lindi mtu atapitia Liwale na kuiona Dar kwa saa chache zaidi kuliko sasa.

Ni kweli wapo mjini, nyumba za kulala wageni zenye heshima zake zipo na zile za vurumai zipo huku disko likiwaka karibu kila siku katikati ya mji na usafiri wa pikipiki ukikuwezesha kufika maeneo ya mbali zaidi kutoka katika mji wa Liwale na ingawa ipo karibu na Selous si kila siku kuna balaa la wanyama.

Nini kiashiria cha kupambazuka Kuna mabadiliko makubwa miongoni mwa wananchi hasa katika suala la kutaka shule, mabadiliko ya maisha na pia uthubutu wa kuuliza kunaendelea kitu gani katika wilaya yao.

Uthubutu umefanya baadhi ya miradi migeni kabisa katika himaya za Kingido yaani Liwale kuonekana inafaa kufanyiwa majaribio huku hamu ya kuendelea kulima mpunga kwa ajili ya soko ambalo sasa linafikia ikilazimisha halmashauri kuomba msaada wa serikali kuu kuhusu mabonde yanayofaa kulimwa mpunga.

Mabonde ambayo yameshaangaliwa na fedha kuombwa ni ya Mtawango, Mtawatawa na Ngongowele, bonde ambalo kama zikipatikana milioni 650 kuna watu watakaokimbia Dar kuja kufanya shughuli nyingine Liwale za kuendeleza libeneke la maisha. Watu wanataka kulima, miaka miwili hii imewafanya watu watambue kwamba wao si kisiwa wanaweza kutengeneza fedha kwa jinsi wanavyotaka.Na kuja kwa miradi mingine inayolenga kunyanyua uwezekano wa soko kunafanya idadi ya wageni wanaotaka kuanzisha shughuli kuanza kuongezeka.

Kwa watu ambao walizoea kula nyara za serikali na kutojali kufuga sasa hivi wanafuga hata nguruwe, hali ambayo usingeliweza kuamini kutokana na mfugo huo kuwa na mushkeri na taratibu za kidini. "Ndio mimi nafuga na nimeanza mwaka huu. Naona inalipa. Tunafuga kwa kikundi na tumeomba msaada wa mbwana mifugo kuona tunaendelea," alisema binti mmoja ambaye aliwakilisha kundi lake katika mazungumzo yake na yangu lakini hakupenda kuandikwa gazetini.

Bwana kilimo na mifugo (Daldo), John Mwakula alithibitisha kuwapo kwa makundi kadhaa ya wananchi walioanza kufuga ng'ombe, nguruwe, kuku na mbuzi pamoja na tishio la mdondo na ndorobo.

Amesema kumekuwapo na mabadiliko makubwa ya msimamo na mtazamo na watu wanaonekana kupenda maisha mazuri na hata mahudhurio ya shule yanakuwa yanaongezeka kutokana na upeo kuanza kuwa mkubwa kwa nini mtu anataka kwenda shule au kwanini mtu awe shuleni.

Ukiachia mbali mabadiliko katika kilimo na ufugaji miradi ya Tasaf ambayo kwa ujumla huwa inaibuliwa na wananchi wenyewe inaonyesha ni kwa namna gani wananchi wa hapa wanataka kuondokana na dhana ya kutegemea serikali na wahisani wengine kufanikisha maendeleo yao. Zipo simulizi na wala sina sababu ya kuamini ni za uongo, kwamba wakati wilaya hii inaanzishwa Mzee Rashidi Kawawa alikuwa na kazi kubwa ya kubadili maisha ya watu kwa kupeleka msaada wa moja kwa moja.

Pamoja na juhudi zake za kuwapelekea wananchi matrekta, kuwaonyesha ujenzi wa nyumba bora za kisasa na kuwa na mji wa Liwale wenye hadhi kubwa na heshima yake, kuondoka kwake madarakani wakati wa kustaafu wake kuliirejesha Liwale miaka 50 iliyopita. Inadaiwa kwamba huenda mwamko wa wananchi ulikuwa mdogo na walikuwa wanatarajia kwamba serikali ndio mfanye kila kitu.

Ndio wakati wa Mzee Kawawa serikali ilitaka kuwabadilisha watu kwa kuwekea msingi, wazee walipoondoka na miradi mingi ikafa kwa kuwa wananchi waliokuwa wanaona kama kitu cha kigeni, waharibifu na baadhi ya miundombinu kwa dhana ile ile kwani yao si ya serikali tu.

Ukichanganya na tatizo la usafiri wakati huo Liwale ilikuwa kama imesimama baada ya kuondoka kwa Mzee Kawawa kama mbunge wao.Akiwa serikalini Mzee Kawawa alitumia muda wake mwingi kukaa na wapiga kura wake kuwafundisha kwa mfano. Katika ofisi za TASAF Liwale unakutana na taarifa za miradi 80 ambayo thamani yake ni bilioni 2.2 na hii si haba ukizingatia huko nyuma kulikuwa na nini na masuala yote yalingoja serikali kuu kwa maelekezo.

"Yapo maneno kaka huku kwamba serikali kazi yake ndio kama hiyo ya kuweka miundo mbinu inawajengea wananchi nyumba na kuwatibia.." imani ambazo si tu zinaingia na kujengeka kwa Liwale bali pia inakuwa ni kikwazo kwa maisha ya kawaida. Miradi ya Tasaf ambayo imeibuliwa na wananchi imelenga kuweka msingi mzito kwa maendeleo ya watoto na wakulima kama ujenzi wa barabara za vijijini, shuleni, maghala na pia ile ya kijamii.

Pia wakati zamani serikali ilikuwa ikiwafuata mashambani kuanzisha shule za setelaiti kutokana na kilimo cha kuhama hama kuwapo kwa shule kamili baada ya watu kulowea maeneo hayo kunafanya sababu nyingine ya kuamini kwamba Liwale inabadilika ikiwa na muonekano wa kisasa zaidi katika masuala mengi.

Na kwa muonekano wa sasa Liwale imepiga hatua kubwa kwani miradi ya Tasaf ikichanganywa na ile ya serikali kuu hasa katika miundombinu inafanya hata kazi ya kuhakikisha kwamba barabara zinapitika mwaka mzima kuwa na hoja ya msingi, kwani kwa msemo wa watoto wa mjini inalipa.

Mkulima mmoja alininong'oneza kuwa barabara zao zinapitiwa kwa nadra sana na magari na kwamba wafanyabiashara wangelileta magari yao na kufika hadi katika minada ya vijijini kununua mazao na hivyo kuyaongezea bei na kumsaidia mkulima asifike mjini bila sababu.

Mradi wa ufugaji unavyowadondosha mate Mama Zainab Aziz anataka wanawake wawezeshwe kuwa na mifugo yao kwa ajili ya kuinua vipato vya wanafamilia, lakini pia alisisitiza haja ya wanawake wa Liwale kujenga mazizi huku wakisubiri mpango wa halmashauri wa kuongeza ng'ombe katika mpango huo maalumu wa kufuga ng'ombe wa maziwa.

Mpango huu wa halmashauri ambao hauna muda mrefu umeshaanza kuwafanya wanawake kuanza kuangalia kwa jicho la wivu hasa wale ambao walifanikiwa kupata ng'ombe na kuthubutu baada ya mafunzo. "Mimi nayaona mafanikio yake nawataka wanawake wenzangu wajiandae kabisa si kama mimi nilivyoanza, wajenge mazizi wajikomboe na hali ya kuwategemea wababa," alisema Zainabu katika mahojiano nyumbani kwake.

Hakuwa peke yake pale nyumbani kwa mahojiano alikuwapo mume wake Omar Mshamu Libuka na diwani wa viti maalum ambaye alifika eneo hilo baada ya kumuomba tufanye mazungumzo ya pamoja kuonja mustakabali wa ng'ombe Liwale.

Halmashauri imeongeza ng'ombe kumi tu na kuwagawa katika awamu ya kwanza na kwa uzoefu mfupi wakiwa nao inaonekana kuwa mifugo ya ng'ombe inalipa. Lita ya mawazi Liwale kutoka kwa mkulima kwa sasa ni Sh 600 na Zainab na mumewe wanatoa takribani lita tisa hadi kumi kwa siku kwa mzao wa kwanza na wanatarajia kupanda zaidi. "Alhamdullilah ng'ombe inatuokoa na tumepanga mambo mengi ya kufanya kutokana na kipato kinachotokana na maziwa."

Anasema Zainab akiwa beneti na mume wake Omar. Amesema nyumba yao yenye watoto 10 sasa wanaweza kula asubuhi na jioni bila kusahau mchana na pia wanampeleka binti yao mmoja tuisheni kumnoa zaidi kwa masomo na pia wanalima mashamba kwa fedha wanazopata.

\"Majuzi tu nimempelekea mama mkwe fedha za kulima. Mama mkwe alikuwa na shida hakuweza kulima (mgonjwa) lakini kutokana na kupanda kwa uwezo tukamtia mtu shambani na jana mke wangu ameenda kumlipa mtu huyo," alisema Omar. Ni wazi hata kama ng'ombe huyo ni wa mkewe lakini kutokana na mapato ya ng'ombe huyo wanafikiria kujenga boma zuri la matofali ya saruji na pia kuongeza ng'ombe mwingine.

Anasema tangu arejee katika ardhi ya Kingindo mwaka 1956 hakuwahia kupata fedha kama anazopata leo wakati yeye kumeshaanza kuwa jioni. "Naiona fedha nikiwa mzee na lazima nichakarike nihakikishe kwamba tuna ng'ombe wawili ili tuendeshe vyema maisha yetu. Kwa wao wamepangiana majukumu namna ya kumlea ng'ombe wao wakikumbuka la msingi kwamba ng'ombe hastahili kulia bila sababu na zizi lake lazima liwe safi daima na chakual si cha kubahatisha.

Binti wa Omar Salma anakiri kwamba tangu wampate ng'ombe huyo maisha yao yamebadilika sana. Pia na yeye anapata nafasi ya kwenda shule katika masuala ya tuisheni na wala asubuhi haondoki mweupe tumboni kama zamani. Kwa sasa na hata baadaye maziwa yana soko kubwa sana mjini Liwale na kwa sifa ya maziwa yake kuwa matamu hatarajii kukosa soko hata siku moja.

Hata hivyo Daldo John alisema kwamba hatarajii wafugaji wachache hao kama wataweza kujaza soko la maziwa lakini kama wakiendelea kutanuka na kuweza basi kampeni nyingine ya kusindika maziwa lazima iingizwe kwa wananchi.

Diwani wa Liwale B, Anna Simba pamoja na kukubali kwamba Liwale kumepambazuka kabisa alisisitiza kwamba maisha bora yanapatikana kwa mtu kuthubutu kujituma kama alivyofanya Zainab na mume wake. Aidha alisisitiza kwamba kama unapewa nafdasi na unashindwa kuitumia usilaumu wengine, akimaananisha kwamba wengi wa wanawake waliopewa nafasi ya kufuga wamekuwa wakijitahidi sana kwa kuzingatia kwamba ni nafasi waliyopewa katika kujinasua kwenye umaskini uliokithiri.

Liwale ni sehemu moja ya Tanzania ambapo kipato cha wanawake ni cha chini mno. Diwani huyo amesema kwamba hata yeye anasubiri awamu nyingine ili aanze kufuga kwani anajisikia fahari sana anapomuona mwanamke mwenzake anasonga mbele. Amesema anaamini kwamba kama wanawake wakiwezeshwa zaidi kutakuwa na nafuu kubwa kwa kaya nyingi duniani hasa kwa kuzingatia kwamba nyingi ya kaya hulishwa na mwanamke.

Wanawake wa Liwale wameanza kuwezeshwa kwa mifugo ambayo inaangaliwa si tu na wakopaji wenyewe bali na halmashauri na watu wengine kuwapo kwa soko kunafanya juhudi kubwa kupata ng'ombe wa maziwa. Mama Mark ambaye alikuwa anachambua mbaazi kwa ajili ya m lo wa jioni wakati akizungumza na mwandishi alisema kitu kinachomkera ni mradi huo wa ng'ombe wa maziwa kuwa na mifugo michache zaidi.

Kuwapo kwa usafiri wa kuaminika kunaelezwa kuchangia sana ustawi wa mifugo hiyo kutokana na kupatikana kwa dawa muda wote. Liwale kama maeneo mengi ya kusini, ndorobo na kupe ni tatizo kubwa. Pamoja na ng'ombe kwa sasa yapo makundi yanafuga nguruwe na mbuzi na kwamba japo kwa idadi kidogo kuku pia wapo. Kama mzee Omar na watoto wake 10 wanajidai, ukizidisha hesabu kwa idadi ya watu watakaofurahi ni dhahiri kuwa sasa kunawezekana kuishi.

Fikiria kutoka hakuna ng'ombe wala mbuzi hadi vijiji 7 kuanzishwa mradi wa ng'ombe na matokeo yake ndiyo hayo yanayofurahisha mno. Mradi huo una ng'ombe jike10 na dume moja. Pamoja na kwamba kuna mbuzi za nyama 680 na wa maziwa wasiozidi 50 Liwale ina haki ya kujivunia kufunga kwake.

Miradi kingine inayoonyesha uhai mkubwa ni kule kutambua tatizo la kitaifa na kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi ambapo pia kuna kazi zinafanywa kwao ili kuwapatia nafuu manake makundi ya Ukimwi yamepewa mashine za kusindika muhogo na pia wanambuzi 60 na washauri wanaingia Liwale bila hata kuwa na mashaka ya kurejea nyumbani baada ya kazi. Makundi hayo pamoja na kupewa mradi huo wa kusindika muhogo pia wamefundishwa pia kuhakikisha kwamba wanaweza kuandaa chakula cha muhogo kwa kisasa zaidi na ndicho wanawake wa hapa wanmachotaka desturi ya kuanika kupata bada jeusi imepitwa na wakati. Machinjio ya kisasa Huwezi kuanza kuwa na mifugo bila kukumbuka minada na pia machinjio.

Ujenzi wa machinjio upo mbali kiasi ya kwamba wakati wowote mwaka huu machinjio hayo huenda yakaanza kazi. Machinjio si tu yatatoa nyama safi bali pia kuanza kuwezesha kutafuta utaratibu wa kuwa na kiwanda cha nyama na kuanza kuzisindika. Yapo machinjio ya nguruwe yanayojengwa chini ya usimamizi wa masisita wa Kanisa Katoliki Mikukuyumbu. Halmshauri siku hizi imeshaanza kuwa na uwezo kama ilivyokopesha mradi wa ng'ombe, halmashauri ya Liwale ilichangia milioni mbili ili kazi imalizike na pia kuwezesha wananchi kutambua wanakula aina gani ya mlo na kama imezingatia shauri zima la mimani zao kwa wakat.

Pia halmashauri nayo inajenga machinjio yake ya ng'ombe na mbuzi na kondoo. Tayari ujenzi upo kwenye hatua nzuri na zaidi ya milioni 15 imeshatumika. Ukiangalia uhaba wa mifugo ambapo kwa sasa kuna ng'ombe 300, mbuzi 4,800, nguruwe 97 na huku kuku kafikia laki moja na zaidi hatua zinachukuliwa zinaonyesha kwamba upo uhai mkubwa katika maisha ya Jimbo la Liwale. Sasa ni rahisi kupiga simu na wale huendi mbali kupata fedha yako hivyo haja ya kuondoka hapa haipo au labda uwe hujui nini maana ya maisha.

Mradi wa kopa mbuzi lipa mbuzi nao unaendelea katika viji vitano vya Liwale na ingawa ulidorora sasa umeanza kushamiri upya. Inapashwa kukumbuka wkamba mradi wa ng'ombe umeanza mwaka juzi na kutekelezwa mwaka huu wa fedha na hasa kwa wafugaji wa Liwale B. Kama mtu huwezi kuamini jinsi mipango ya serikali inavyoanza kuwatoa wana Liwale hasa baada ya kuachana na tabia ya zamani ya kutumia vifaa vya serikali na kuvitupa, basi unapaswa kufika Liwale na kuzungumza na wanavijiji vya Liwale B na sasa ukaangalia maandalizi ya kuwa na mradi huo pia katika kijiji cha Likombora.

Wakiwa na mafunzo na mazizi tayari kijiji hicho sasa kimeitisha zabuni kutambua nani atawaletea ng'ombe hao na wana sifa gani. Ushirika Kwa sasa kuna saccos 11 za wakulima na mbili za wafanyakazi wa Boma. Kuwapo kwa saccos hizo ambazo zina fedha za kutosha kukopesha ni dalili nyingine ya kufunguka kwa jimbo hilo.

Wananchi wanapoweza kuoanisha mitaji ni dhahiri kwamba kazi zilizobaki za kushawishi wengine kutambua nyenzo ya maisha bora ni pamoja na ushirika wa saccos zitakuwa zinazaa matunda. Halmashauri mwaka huu imetoa milioni 7.5 kama sehemu yake ya kuimarisha saccos hizo. Kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba elimu zaidi inatolewa ili wananchi wengi kufikia upeo wa kufikiri na kufanya kazi, hali ambayo itasaidia kupunguza umaskini.


Lakini kwa kufunguliwa kwa barabara, ujenzi wa nyumba za kisasa na kukua kwa mji wa Liwale kwa kasi inayostahili ni wazi kuwa Liwale ya sasa si ile ya zamani kwani maji bwerere, nishati yenye uhakika japo ni ya jenereta inafanya mji kuwa na mwanga hata usiku. Labda kuna shida ya maji Haipo kwani kwa mjini, mto Liwale unalindwa na kuhamiwa ili uendelee kulisha mji wa Liwale na katika vijiji ndani ya jimbo uchimbaji wa visima na malambo unaendelea.

Mbunge amesema kwamba pamoja na uhaba wa maji katika jimbo lake bado anadhani kuwa kila mtu atapata maji salama hivi karibuni. Upatikanaji wa maji vijijini si mzuri sana kutokana na maeneo kuwa na visima vifupi vilivyochimbwa nyakati hizo, lakini miradi kama ya Kibutuka na Kingara wa visima virefu viwili vitafanya maisha kuwa ya raha peke yake .

"Najaribu kushawishi miradi zaidi, lakini cha msingi ni mabasi zaidi kufika Liwale na kupishana hilo ndilo la maana barabara zipo basi njia zifunguke ili soko la Liwale likue," anasema mbunge Kigwalilo. Kila kitu kipo safi kwa Liwale, Liwale ile ya zamani si ya sasa na hata ukitaka disko lipo na nini tena ambacho unadhani unaweza kukikosa? Hamna nakuhakikishia hamna.
 
A most interestingly original post from a distinguished member. Although that comment about Mtwara lacking educated people, apart from being unnecessarily cryptic and unwarrantedly provocative, was incosiderately unfortunate, even under the veil of brutal honesty.

I should like to analyze this issue from a different perspective.It is possible to catalyze development by using the media, but it is easier to develop a region either simultaneously with the development of it's media, or before the development of it's media.

For me, an economic backward region is not a viable market for media businesspeople and more than that, even humanitarian / grassroot efforts and NGOs may end up frustrated by the prevailing economic conditions.How can you tell a mother to sit down and read while she has to walk 20 km to fetch water or firewood?

The lack of regional newsparer/ media outlets is only a tip of the iceberg. The reason why places like Sumbawanga and Mtwara are hardly covered is staring us in the face, our country is disproportionately centralized, with everything in Dar, places like Moshi/ Arusha and Mwanza come a distant second, and after that you have a totally different country.The rural/ urban divide is nothing unique to Tanzania, but with the advent of globalization the common trend is the narrowing of this divide, with us it is almost like the divide is widening, with some people in Dar living like they are in Malibu, while some folks in Mpanda are moving back to the days of "Dr. Livingstone I presume".

The free market - with all the current afflictions- still follows the law of money gravity, supply will almost always go where there is demand. If there are enough development projects, enough income generating employment, enough disposable income, enough educated people, enough time for recreation and consumption of news, surely there will be a natural demand for news and the Mengis of Tanzania will quickly snap the opportunity.

Currently most of the able bodied young people from Mtwara are hustling in Dar, and the ones back in Mtwara are under a budget (primarily monetary but in some cases timewise too) which cannot afford them the "luxury" of reading.

With a few exceptions, unless you are interested in one of these do gooder's money sinkers, which would come up with a nice top down write up about starting a magazine for an uneducated- possibly uncaring too - population, simply because some idea may sound too far fetched, too top down and too removed from their reality.

When I was a primary school kid, in the height of the cold war, a lot of my friends used to go to a Russian embassy propaganda centre to collect their communism propaganda books.The Russian diplomats were very happy to see such young schoolkids interested in their propaganda books by the volumes, what they did not understand was that the young Tanzanians were only interested in the books because they were going to give the books to "Mzee mkaanga mihogo" who would then give them a few mihogo per a bundle of Russian propaganda books.At the end of that entire transaction, the carefully prepared and expensively printed Russian propaganda books ended up as some sort of paper plates for primary schoolkids who were not interested in neither Lenin nor Gromyko.

The moral of this little story down memory lane is that whatever plans are to be adopted in order to stimulate the level of media coverage and establish regional media outlets must be focused on the grassroot, must reflect the level of economy and therefore be self sustaining (no sense starting a TV station covering a radius of 200 miles while you only have 20 TVs in the entire area, it is simply uneconomic) and must come as a result of a collective elevated social consciousness that will balance in harmony with purely economic interests (you want an economic structure, you don't want a vulture to exploit people because of the possible naivette and lack of exposure).
 
Last edited:
For me, an economic backward region is not a viable market for media businesspeople and more than that, even humanitarian / grassroot efforts and NGOs may end up frustrated by the prevailing economic conditions.How can you tell a mother to sit down and read while she has to walk 20 km to fetch water or firewood?

...Currently most of the able bodied young people from Mtwara are hustling in Dar, and the ones back in Mtwara are under a budget (primarily monetary but in some cases timewise too) which cannot afford them the "luxury" of reading.
The potential is right there.
Umewasahau wenyeji wa Mtwara waliohamia Dar; wao ndio watakuwa wasomaji walengwa namba moja!

Kama ambavyo imeonekana kwenye hii thread, wasio wenyeji wa Mtwara know so little about the place. Hawa wasio wenyeji wa huko, pale waendapo kusoma UK, Uchina, USA n.k., watafaidika mno kupata exposure ya Mtwara. Tena wanaihitaji kuliko aliyeko bongo.
 
Back
Top Bottom