REGIA MTEMA: Mbunge aliyepania makubwa Kilombero pia awataka W'Nchi kuepuka Watu Wenye Siasa Chafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REGIA MTEMA: Mbunge aliyepania makubwa Kilombero pia awataka W'Nchi kuepuka Watu Wenye Siasa Chafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  Danson Kaijage


  “NI lazima Wilaya ya Kilombero iwe na heshima ya kimaendeleo, haiwezekani wilaya yenye vyanzo vya kuzalisha umeme na yenye kulima mpunga kwa wingi, wananchi wake wawe nyuma kimaendeleo,” anasema Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Regia Mtema.

  Regia ambaye ameingia kwa mara ya kwanza bungeni mwaka 2010, anasema kutokana na nafasi yake ya ubunge, elimu yake, ujasiri, uzalendo na ujana wake ameazimia kutetea maendeleo kwa Watanzania hususan vijana, wazee, watoto na wanawake wa Wilaya ya Kilombero.
  Mbali na hilo, anasema kinachomfanya aamue kujitoa ili kuhakikisha wilaya hiyo inapata maendeleo ni kuona vijana wengi wakishindwa kujiendeleza kutokana na kukosa ajira.

  Anasema pamoja na kuwapo kwa fursa mbalimbali kwa ajili ya mikopo kwa makundi mbalimbali lakini bado mikopo hiyo imeshindwa kuwafikia walengwa hali inayosababisha vijana kutopata mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

  Regia anasema kitendo cha fursa hizo kutowafikia walengwa katika kupata mikopo kunasababisha vijana wengi kuendelea kukaa vijiweni bila kazi yoyote ya kujiongezea kipato.

  Mbunge huyo mwenye ulemavu ambaye ni kijana wa kwanza kuonyesha uthubutu wa kuwania ubunge wa Jimbo la Kilombero hivyo kuandika historia, anasema lengo lake kubwa ni kuhakikisha jamii inatambua kuwa ubunge siyo kukaa bungeni bali ni kuwa mtumishi wa wananchi.
  Anasema kuna makundi mengi ndani ya Wilaya ya Kilombero yamesaulika hivyo ni lazima ufumbuzi upatikane ili kuwawezesha kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

  Anasema matatizo hayo yatapatiwa ufumbuzi kwa kuyaibua kwanza na kisha kupanga mikakati ya kuhakikisha kuwa yanatatuliwa.
  “Ni lazima nijitose kuwakomboa wananchi kwa kutumia nafasi yangu ya ubunge na pia ya waziri kivuli wa Kazi na Ajira, ni lazima nishughulikie matatizo ya wananchi hususani walioachishwa kazi bila malipo yao ili waweze kupatiwa haki zao kama walivyo Watanzania wengine,” anasema Regia.

  Regia ambaye kuanzia mkutano wa pili wa Bunge amekuwa akilalamikia bungeni kushushwa kwa bei ya sukari hasa katika maeneo inapozalishwa, anasema anapofanya kazi ya mageuzi ya kimaendeleo hafanyi mageuzi kwa ajili ya kulinda watu fulani ama kuwafaidisha watu wa chama fulani bali anafanya kazi hiyo kwa manufaa ya Watanzania wote, hasa wana Kilombero.

  Hata hivyo, anasema anatamani kuona Watanzania wote wanatambua umuhimu wa kubadilika kimaendeleo, kuachana na tofauti za itikadi na kujikita katika kutafuta maendeleo.

  Mbunge huyo anaeleza kuwa amejipanga kuiletea maendeleo Wilaya Kilombero na katika kipindi kifupi tangu ashike nafasi hiyo ameanza kuonyesha kwa vitendo juhusi hizo kwa kuezeka chumba cha cha darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Msufini ambayo ilikuwa imetelekezwa na halmashauri ya wilaya hiyo.

  Ameweza pia kutoa misaada kwa ajili ya kufufua miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji ambayo ilikuwa imekufa na kusababisha wananchi hasa wanawake kutembea mwendo mrefu tena wakati wa usiku, kufuata maji.

  Miongoni mwa vijiji ambavyo awali kabla ya kufufuliwa kwa miradi ya maji vilikuwa vikikabiliwa na kadhia hiyo ni Michenga kilichopo katika wilaya hiyo ambayo ni maarufu kwa kilimo cha miwa na mpunga.

  Wanakijiji hao wanasema pamoja na kuwa na mradi wa maji lakini mradi huo uliharibika na kusababisha wananchi kuchangishana fedha ili waweze kufufua.

  Hata hivyo, wanasema kutokana na hali ya ugumu wa maisha, walishindwa kupata fedha za kutosha za kuwezesha mradi huo kufufuka.

  Regia anasema malengo yake si kuangalia miradi ya kiuchumi na kijamii pekee bali jicho lake litaiangalia pia sekta ya michezo ambayo kwa muda mrefu imesahaulika wilayani humo.

  Anasema kwa kuangalia sekta hiyo ya michezo kwa jicho la pekee, vijana wataweza kushiriki katika michezo mbalimbali na hivyo kuwaepusha kukaa vijiweni.

  Anasema katika kuwawezesha vijana wa jimbo hilo kushiriki kikamilifu katika michezo, ametoa jezi za mpira wa miguu na mikono katika kata mbalimbali za wilaya hiyo.

  Anasema huo ni mwanzo wa kuhakikisha kuwa mikakati ya kutekeleza sera ya michezo nchini inafanikiwa.

  Anasema kwa kutumia nafasi aliyonayo atahakikisha vijana wanajikusanya na kuuda timu ya mpira wa miguu na ya mpira wa mikono ambayo itakuwa na nguvu kubwa itakayowawezesha kuingia ligi kuu.
  Kwa mujibu wa mbunge huyo, anachoaamini ni kuwa mageuzi ya Kilombero yataletwa na wana Kilombero wenyewe kwa kushirikiana na wana mageuzi wa maendeleo na wala si mtu mmoja mmoja.

  Anasema ili kuweza kuondokana na umaskini ni lazima kukawepo watu ambao watakuwa ni chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Morogoro.

  Anaeleza kuwa kutumia nafasi yake ya Uwaziri Kivuli wa Wizara ya Kazi na Ajira, atahakikisha anatafuta taarifa za kina ili kuweza kuwasilisha hoja binafsi bungeni.

  Anasema hoja yake italenga kutaka kufahamu ni kwanini serikali imekuwa na ikiwanyima haki watumishi wastaafu kwa kutowalipa fedha zao kwa wakati mara tu wanapostaafu.

  Regia anasema jambo jingine ambalo linamnyima usingizi ni kuona ubovu wa barabara uliokithiri katika wilaya hiyo ambapo maeneo mengi hasa katika kipindi cha mvua hazipitiki.

  Mbunge huyo anasema jimbo hilo limekuwa kama shamba la bibi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali, kuanzia vitongoji, vijiji na halmashauri.
  Anaziainisha kero za jimbo hilo kuwa ni miundombinu mibovu na ukosefu wa maji safi na salama ingawa wilaya hiyo ina vyanzo vya kutosha vya maji.

  Anavitaja vyanzo vya maji katika wilaya hiyo kuwa ni pamoja na Kihasi, Kiburubutu, Sanje na Kidatu ambavyo utililisha maji kwa kipindi cha mwaka mzima.

  Pamoja na ukosefu wa maji, anasema tatizo jingine la ukosefu wa umeme katika kata ya Kidatu, wakati kuna vyanzo viwili vya kuzalisha nishati hiyo ikiwemo Bwawa la kuzalisha umeme la Kihansi linampa shida.

  Anasema pamoja na mipango yote aliyonayo ni vigumu kwa wakazi wa wilaya hiyo kufanikiwa katika maendeleo bila kuwa na elimu ikiwemo ya ujasiriamali.

  Anasema jambo jingine la kuzingatia ni wakazi wa wilaya hiyo kujitambua na kujithamini wenyewe hasa katika kudai haki zao za msingi badala ya kulalamika ama kuacha waendelee kuonewa.
  Anasema kamwe amani haiwezi kuwekwa kando na hivyo atatumia nafasi yake kuhakikisha anahamasisha vijana na watu wengine kulinda tunu hiyo na vilevile kudai haki zao za kimsingi.

  Anasema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiingiza siasa chafu nchini kwa kudai kuwa baadhi ya vyama vya upinzani ni vyama ambavyo vinamlengo wa kuleta vurugu, jambo ambalo si la kweli. Anawataka wananchi kuwaepuka watu hao kama ukoma kwa kuwa wameishiwa kisiasa
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thank you very much..... Now what is your take home message?:A S 39:
   
Loading...