Elections 2010 Regia Mtema aongoza kwa 1250, Fomu nyingine zimeota miguu!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Kutoka Kilombero Mgombea wa CHADEMA Regia Mtema anaongoza kwa takribani kura 1250 na jitihada kubwa inatafuta kuweza kupata kura zitakazochakachua hizo. Fomu kutoka baadhi ya vituo zimeota mbawa na kama zile fomu kwenye mji mwingine ambazo ziligoma kuingia kwenye mashine hizi za Kilombero hata kuja hazitaki kuja.

Inaonekana kuna hali ya kukata tamaa na mwisho kama sehemu nyingine itabidi wakubali sauti ya watu isikike. Kama ushindi ungekuwa unakubalika mara moja jimbo la Kilombero lingekuwa ndio jimbo Pekee Morogoro kwenda upinzani..

Tusubiri.. labda hizi fomu zikipatikana zitakuja na idadi ya kuwatosha watani wa Chadema, CCM..
 
aaagrrrrr....hawa watu bana.....ni nini mbona ving''ang'anizi namna hii
 
Tuombe Mungu Dada yetu ashinde pamoja na jitihada zinazofanywa za kuchakachua. Kwa kupata jimbo Mkoani Morogoro itakuwa ni ushindi mkubwa kwa CHADEMA, wanaharakati na wanachi wapenda mabadiliko kwa ujumla. Na muhimu kuliko yote, CHADEMA imeanza kujenga sura ya kitaifa zaidi tofauti na awaki..
 
ukweli ni kwamba wale jamaa kila kitu pale bomani-kibaoni ifakara, dada regia yuko twin wake hapo tangu mapema sana asubuhi kabla ya hata sanduku moja halijaingia mjengoni. Takwimu za mwanakijiji ni za ukweli ila ccm mkoa waliapa na kumhakikishia jk kuwa ulanga magh na kilombero ni salama, jk alinusa harufu mbaya ktk majimbo hayo na kuwatahadharisha, dc mwambungu jana amekuwa akiwahabarisha wadau wake kuwa mkoa wameuchukua wote. Tuliposikia hayo tukahofia kwa regia na professa, bahati mbaya prof hakutaka kudharirishwa na ubabe wa dola akawaacha na kususia zoezi zima.

regia amekomaa na yuko very strong na wananchi wa kilombero wanaamini ni yeye na si vinginevyo.

chadema chonde chonde hamieni kilombero kumsaidia dada regia, dada mlemavu lakinin yuko imara na sasa anataka people's power ili courage iimarike. Jana alizuia mabox matatu yameletwa yakiwa yamechanika, akayagomea mpaka walipoyahakiki na kujiridhisha yana tally na data alizo nazo yeye.

huyu ndie wa kututoa aibu.

mpaka saa mbili usiku walikuwa wako pale bomani ifakara
 
Inabidi Waheshiwa watarajiwa Silinde David na Mnyika John waende kutetea ukombozi wa majimbo yaliyobaki

Jifunzeni kutoka kwa Nyerere, Ukipata ushindi hutakiwi kusherekea kwanza, ni muda wa kuwasaidia wenzetu kwenye mapinduzi
 
FDR inaonekana kuna mtu amewatisha wakuu wa wilaya, na nadhani kule kote upinzani uliposhinda watu watapoteza kazi. Mimi nashangaa kitu kimoja mbona sehemu zote CCM ilizoshindwa matokeo inakuwa magumu sana kupatikana, mpaka inafika sehemu mabomu yanapigwa? Hivi kweli hawa watu wanavalue Amani? ....I seriously doubt!
 
Jk alikuwa wazi kwa viongozi wote pale malinyi na hapo ifakara kuwa wagombea wa ccm maeneo hayo wamepikwa kwa njaa za viongozi hivyo yeye atashughulika na wao. Sikuamini mwanzoni ila baada ya mheshimiwa kutanabaisha kuwa mkoa umebebwa na wao nika recall niliyoyapata malinyi alipotua jk
 
Huu Uchaguzi ulitakiwa kuwa moja kati ya uchaguzi bora katika bara la Afrika , kama sio shughuli za uchakachuaji zilizofanyika baada ya uchaguzi. Ni muhimu kwa viongozi kutambua ya kuwa Tanzania ilikuwepo kabla ya CCM na itaendelea kuwepo even after CCM ...
 
Kweli Mkuu ile chopper inabidi iwe inapeleka wapiganaji fasta fasta katika majimbo yote ambayo yana harufu ya uchakachuaji maana tuko vitani kama vipi Chadema anzisheni Harambee tuchangie mafuta
 
REGIA,Umetuonyesha njia na ninakwambia yule tapeli mteketa na ccm kilombero wanajuta kukutana regia wa mtemanyenja, binti wa kindamba jasiri kuliko mama lwakatere, mahiri zaidi ya celina kombani makini kuliko tunavyodhania.

Tulijange,tulijangee, tulijangi nakaka x2 tulijange,tulijangee, tulijangi nakaka x2 tuwoni ndembu tunyuminyumi!!! Regia wimbo huu ni national anthem kwa mndamba hususani tunapokuwa ktk vita mathalani ya hii kwako. Ktk halilyoyote ya matokeo nakusihi waombe wamama na wazee hapo ifakara muuimbe wimbo, mimi nakuimbia licha ya kuwa niko dar kiroho tupo nawe. Big up mhaja wangu, mulungu akutangi muhumbu. Tili vandu mulungu ka patali ila daima atakupigania.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom