Regia adai kiwango cha elimu kimeshuka; PhD bungeni sawa na BA?

phD siyo Omniscience bali ni reductionists kwa hiyo ufahamu wao ni wa kitu kidogo kati ya vingi kwa upana wa hicho kidogo.Ukweli ni kwamba knowledge ya phD holder imefungwa kwa kile alichosoma na tusidanganyane wanajua saaana

Inabidi uingie google utafute why is it called PhD kabla ya kusema haya! Kwanini hivi wote wana end up kuwa PhDs holders na hawapewi jina based on specific fields.....

Ukiwa trained in fine art hawakutegemei uchore tu picha zile ulizo zichora wakati wa training....They teach you an art of doing fine art; Tutoe uzito kwenye mambo yanayopashwa kupewa uzito ama sivyo tutapoteza mwelekeo. Kumbuka impact yake ni kubwa sana kwenye inspirations za watoto/vijana katika kusoma.

Watu wanapo abuse the means of adding value to materials haimaanishi inaondoa maana ya hiyo value katika ku qualify materials. Ningemshauri Mheshimiwa aangalie katika means zaidi ambayo ni determinant ya end value kuliko kuilaumu end value yenyewe, kwani pamoja na yote bado hiyo value bado ina hold water kwa many of the market products zilizopo. Generalization would lead to disappointments za wale ambao bado wanajali the end values.
 
Alikuwa na maana pana zaidi ya wengi wanavyofikiria
Watu wananunua paper kuanzia olevel hadiphd wananunua!c tunawajua au mmewasahau?phd chache za maana kama za madr. Na maprof walioko ccm wanaziacha dar kwa makamba ,bungeni wanakuwa mazuzu tu!!!

Hahahahahaaahahaaaa.., Sory guyz najua hili ni jukwaa serious kidogo, but hizi comment duh! mkuu hii comment imekaa ka joke/utani flani vile.., shauri yako ngoja akina dakta Alaj Mak'amba akusikie..:bump::bump:
 
msimwewekee regia maneno mdomoni kwake ambayo hakuyasema.alisema mwenye degree sasa ni sawa na mwenye phd,hakutofautisha mwenye kuhold hiyo degree wala fani which is very embarrasing to herself.how can you just compare a normal doctor who has one degree and a consulting doctor kwamba wako sawa? Examples can go to other fields as well.anayemuunga regia mtema katika hili inabidi akiriview kichwa chake kwanza

Mkuu mbona umemind sana? vp au na ww ni mmoja kati ya ma Pechede olders wa mjengoni nini???
 
wacheni kujistify pumba na hoja za kikuku kwa sababu ya itikadi za chama.thinking capacity ya phd holder haiwezi kuwa kama ya degree holder.never!

Usikasirike rafiki. Angalia hata mpangilio wa sentensi zako. Inaonyesha umekasirika sana. Mwanzo wa sentensi anza na herufi kubwa; Punctuations, etc....!
 
Mtu kuwa na elimu ya Phd si uhakika wa kuwa na big thinking capacity. Ni sawa na waendao shule kuna wanaofaidika baada ya kuhitimu na wengine wanaishia kupata vyeti vya kuhitimu bila kunufaika na elimu, ingawa inasaidia kupanua wigo wa kufikiri. Ila ninachoshangaa wenye PHD kushindwa kutema cheche wakati elimu ya PHD vyuoni ni ya mfumo wa ushindani wa kujenga hoja.
Ukiona baadhi waliopitia elimu ya vidatu na diploma unaona wana big thinking capacity waliyopata katika masomo yao ya fasihi kuliko waliopitia huko kwenye PHD na tesis zao. Nashangaa ni rhytoric gani walikuwa wanasomea huko ukilinganisha na pumba wazotoa. Afadhali ya fasihi ya diploma na bachela waliyopata toka english composition and effective speaking kuliko rhytorics ya phd. Kabla ya kujiunga na graduate college nilifikiri kama wengi wanavyodhani, kumbe nimegundua inategemeana na mtu na wengine wanamaliza kwenye makaratasi na wanapotoka nje ya chuo kila walichosoma kimeishia ndani ya majengo ya chuo.

Ukisoma historia ya wagunduzi wengi kama akina Thomas Edson mvumbuzi wa bulb za umeme kwa mfano tu hawakuwa na PHD ila elimu ya kawaida tu.
 
Usikasirike rafiki. Angalia hata mpangilio wa sentensi zako. Inaonyesha umekasirika sana. Mwanzo wa sentensi anza na herufi kubwa; Punctuations, etc....!

Kwanza siyo siri? Mbona kuna wabunge mle ndani walifutiwa matokeo ya mitihani ya sekondari sababu ya udanganyifu, sasa alichosema Mheshimiwa Regina hakuna kosa ni sahihi kabisa. Juzi juzi tumetoka kujadili habari ya mheshimiwa January Makamba aliyefutiwa matokeo ya sekondari sababu ya udanganyifu, na leo ni mbunge aliyepita bila kupingwa.
 
Richmond /Dowans iliidhinishwa na baraza la mawaziri ona Dr's sijui ndiyo na Ma-Prof. waliokuwepo katika hicho kikao (Kapuya, Kawambwa, Maghembe, Magufuri, Nagu, Mwakyusa, Mwandosya na wengine utaongeza,) Mwenyekti wa kikao hicho alikuwa Dr, Dr, Dr, JK wa ukweli!! hahahahaha wakaidhisha kampuni hewa ambayo mwenyekiti amesema hata wamiliki hawajui.
Sasa nambieni ubora wa PhDsssssssssssssssssssssssssssss za Bongo.
 
Ukifuatilia majadiliano haya kwa wanajf utajifunza mengi juu ya Elimu kwa ujumla na wasomi wetu na Uwezo wakufikiri na kutafakari - NI KWELI IPO SHIDA.

BOTTOM LINE - ELIMU NIJUAVYO MIMI siyo papers ulizo nazo good names za ulikopitia ni uwezo demonstrated having had what you had or having gone through where you went. Ndiyo maana A. EINSTEIN alisema "Education is what is left after you have forgotten what you learned in school"
 
Mh.Regia Mtema mbunge wa viti maalum wa CHADEMA wakati akijadili hotuba ya Rais katika kipaumbele cha Elimu amezungumzia kushuka kwa elimu nchini Tanzania.

Akitoa mfano wa kushuka kwa elimu amedanganya kwa kusema eti hakuna tofauti kati ya mtu mwenye PhD na mwenye digrii ya kwanza katika 'thinking capacity'.

Nawasilisha..

Siyo amedanganya, huo ndiyo ukweli. Ebu mfikirie Makongoro Mahanga na Emmanuel Nchimbi, Mary Nagu. Unasemaje ukiwafananisha na kijana Mnyika?
 
Siyo amedanganya, huo ndiyo ukweli. Ebu mfikirie Makongoro Mahanga na Emmanuel Nchimbi, Mary Nagu. Unasemaje ukiwafananisha na kijana Mnyika?
Naona wengi mnamtetea,Mods wamemtetea kwa kubadilisha heading,wengine wanazungumzia PhD feki,mnamfanya Regia kama malaika.
Ukweli ni kwamba Regia amedanganya na kuidhalilisha taaluma ya PhD kwa kusema thinking capacity ya mtanzania mwenye PhD ni sawa na ya mtu mwenye first degree.Tunamtaka awe mwangalifu kwa maneno anayoongea,naomba msimfanye yeye ni Malaika.Kama ni chama hata mimi ni mwana CDM ila siwezi kuvumilia utumbo.
 
Tunamuomba atuwekea utafiti alofanya au alonukuu kufikia kusema maneno hayo.
 
msimwewekee regia maneno mdomoni kwake ambayo hakuyasema.alisema mwenye degree sasa ni sawa na mwenye phd,hakutofautisha mwenye kuhold hiyo degree wala fani which is very embarrasing to herself.how can you just compare a normal doctor who has one degree and a consulting doctor kwamba wako sawa? Examples can go to other fields as well.anayemuunga regia mtema katika hili inabidi akiriview kichwa chake kwanza
kwa mfano huo, tunawajuwa madaktari general practitioners au registrars wenye uwezo wa kuchambua mambo kuliko hata hao unaowaita consulting Doctors. Kinachosemwa hapa ni uwezo kufikiri, na hili linatokana na kuushughulisha ubongo zaidi kuliko kumeza maandishi na maprocedure.
 
Tunachouliza, alifikiaje conclusion hiyo?
Sample yake ilikuwa na Ph.D holders wangapi na wenye degree za kwanza wangapi? Alitumia vigezo vipi kupima uwezo wa kuchambua au wa kufikiri wa hao aliowalinganisha.

Dah mwalimu maswali yako hayo sijui kama yatapata majibu...!
 
Ni vyema tukaelewa kuwa PHD inabidi iwe kichwani mwa aliyeisoma na kuipata na inabainishwa kwa performance, Hoja, utoaji wa Analysis za matatizo na solution zake, uwezo wa PHD Holder kuisaidia jamii iliyomzunguka kuondokana na matatizo yaliyo ndani ya nyanja yake ya kitaaluma. PHD si kitendo cha kuwa na cheti pekee ambacho unaweza kukining'niza ukutani ili kila mtu abaini una PHD au kitendo cha watu kukuita Dr. Vilevile mwenye PHD akifa anakufa nayo, lakini cheti cha PHD huwa akifi labda kiteketezwe au kupotea.

Regia alimaanisha uwezo wa watu wenye PHD Bungeni au reflect PHD zao bali nao wapo kama watu wa First Degree, kimsingi haoni tofauti yao, ina maana mchango wao si dhabiti kama alivyotegemea. Kwake ameona hali hiyo inasababishwa na kushuka kwa kiwango cha elimu, yaani watu wanasoma wapate cheti na si kuelimika.

Uwezi ukawa PHD holder unaburuzwa na wanasiasa wajingawajinga wasio na mtazamo wala maono kwa taifa na chama chao wewe unakubali eti kisa wasije wakanitimua ktk chama chao, au usije kosa ubunge au uwaziri.Wasomi wamekuwa watumwa wa wanasiasa na fedha yaani wasomi hawajaelimika bado wameshindwa kuelewa kuwa MONEY IS THE CHAIN OF SLAVE
 
Kwa hiyo yote ni intuition yake tu?

Mheshimiwa Regia mtema amesoma SUA ninamfaham sana. Huo uwezo wa kuongea na kuchambua mambo ametengenezewa na maproffessor wa SUA wamechangia kwa kiasi kikubwa kumfanya awe kama alivyo. Mimi ninafikiri ameteleza kidogo kwa hilo.

Precisely!kipimo alichotumia hakiwezi kutupa majibu sahihi!kwa hili ameteleza!!
 
Naona wengi mnamtetea,Mods wamemtetea kwa kubadilisha heading,wengine wanazungumzia PhD feki,mnamfanya Regia kama malaika.
Ukweli ni kwamba Regia amedanganya na kuidhalilisha taaluma ya PhD kwa kusema thinking capacity ya mtanzania mwenye PhD ni sawa na ya mtu mwenye first degree.Tunamtaka awe mwangalifu kwa maneno anayoongea,naomba msimfanye yeye ni Malaika.Kama ni chama hata mimi ni mwana CDM ila siwezi kuvumilia utumbo.

Inaonekana umeguswa! Pole lakini huo ndiyo ukweli.
 
Back
Top Bottom