Refa apewa mkong'oto na mchezaji baada ya kumpatia kadi nyekundu England

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Refa akionesha kadi nyekundu

Maelezo ya picha: Refa akionesha kadi nyekundu
Refa mmoja amepigwa ngumi usoni katika mechi ya kandanda ya kirafiki baada ya kumpatia kadi nyekundu mchezaji wa klabu ya Sporting de Mundial mjini London siku ya Jumapili.

Maafisa wa polisi na wale wa huduma ya ambyulansi waliitwa ili kuingilia kati. Refa huyo kwa jina Satyam Toki, 28 anafanya uamuzi wa kuwasilisha mshtaka mahakamani.

Klabu hiyo ya Sporting de Mundial inasema kwamba mchezaji huyo ameondolewa katika klabu hiyo na kwamba atapatiwa matibabu ya kiakili.

Satyam Toki

SatyamToki ni mkufunzi na refa

''Tunashutumu kitendo hicho cha kutisha'', waliongezea katika mtandao wao wa Twitter.

Toki alisema kwamba alimuomba mchezaji huyo mara kadhaa kutumia lugha nzuri na kuwacha kulalamika, kabla ya kumuonya.
Alianza kutoka na kuelekea katika eneo la wachezaji wa ziada wa timu yake na alipokuwa akiondoka alinitishia kwamba ataniona baada ya mechi, Toki alisema.

''Ni wakati huo ndiposa nilimpatia kadi nyekundu na kunipiga ngumi usoni''.
''Karibu anasisababishie upofu kwa sekunde chache, na baadaye nilianza kutokwa damu.

Satyam Toki

Kushambuliwa kwa Satyam Toki kulinaswa na kamera ya uwanjani
Toki anasema kwamba ana wasiwasi kwamba iwapo atamshtaki mchezaji aliemshambulia, huenda akapoteza kazi yake, lakini akaongozea: kwa upande mwengine, iwapo sitamshtaki, katika siku za usoni huenda akamfanyia kitendo hicho refa mwengine.
 
Back
Top Bottom