REDUX: CCM Ilivyo Sasa Haiokoleki

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
CCM kama ilivyo sasa haiwezi kuokoleka

picture-12.jpg

Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 18 August 2009

Gumzo

KUNA watu ambao kwa makosa ya fikra zao na kiburi cha utamu wa madaraka, hasa wale waliopigwa ganzi ya "utukufu wa kisiasa," wanaamini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitadumu madarakani milele.
Hawa, wamejiaminisha katika upotovu wao kuwa CCM kitadumu milele na kitaendelea kuwa kama kilivyo sasa. Hawa ni wa kuwekewa mikono na ikibidi kupepewa huku wanavutwa masikio.
CCM ni mazao ya binadamu, ni chombo kilichoundwa na wanadamu; kimeongozwa na kinaongozwa na binadamu na kutokana na hilo tu peke yake, CCM kinakuwa ni chombo kinachoweza kuharibika, kuvunjika, kuporomoka na kwa hakika kabisa chaweza kuzama.
Hakuna ustadi wa mwanadamu unaoweza kufanya kazi zake zisiwe na makosa milele. Katika uelewa wetu huu mdogo wa kibinadamu ni kazi za Mungu tu ambazo hazina makosa.
Hivyo ninaposikia mtu anasema kwamba CCM itatawala milele, na kumtumbulia macho kama mjusi aliyekoswakoswa na mlango. Na pale ninaposikia kuna wana poropaganda wa CCM ambao "wanaitetea CCM kuwa ni chama safi na kina mafisadi wanne tu," ninafumba macho yangu kwa mshtuko.
Kama ningekuwa karibu na mtu huyo, ningemtingisha ili atoke katika usingizi wake uliochanganyika na ulevi wa madaraka.
Malumbano tunayoyasikia sasa na kugongana kunakoendelea hivi sasa ndani ya chama hiki na tutashuhudia zaidi miezi michache ijayo, yanatoa ushahidi wa jambo moja kubwa kuwa CCM kiko matatani na hakuna mtu wa kuiokoa.
Wale wanaogongana ndani ya CCM leo hii, hawagongani kwa sababu ya tofauti za kiitikadi (karibu wote hawana); wanagongana zaidi kuhusu maslahi yao ndani ya chama. Makundi yote yaliyopo ndani ya CCM leo yanatuhakikishia kuwa hayawezi kudumu ndani ya chama hichohicho yakiendelea kuongeza upana, ukali na uzito wa tofauti zao.

Gazeti toleo na. 150
 
kolimba alisema 'chama kimepoteza dira' wakamfanyizia.

asa hivi sjui watamfanyizia nani?
 
lol

We will see.

InshaAllah tuombe uzima. We will be here November 2016. Hopeful this thread will be around.
 
Kwa hali ilipofikia sasa na hasa ukiangalia chama cha ushindani kinavyozidi kujipanga kuchukua nchi naamini ni kweli kabisa 2016 tutakuwa tukidiscuss vitu vingine kama state restructuring na siyo kudiscuss el na ra kila kukicha.
 
Mwanakjj.
Nakubaliana na wewe kabisa. SISIEMU hapa inachezea tu akili za wana-SISIEMU. Huwezi kusema unavua chama gamba wakati huyo anayeendesha vikao na kutoa maamuzi ni sehemu ya hilo gamba. SISIEMU ilitakiwa kufanya mabadiliko kuanzia kwenye ngazi ya Mwenyekiti hadi mwisho.

Hapa hakuna kuvua gamba bali naona ni kupaka gamba rangi. Hakuna atakayefukuzwa uanachama ndani ya mafisadi, wakifukuzwa maana yake JK naye afukuzwe uanachama maana ya yeye ni sehemu ya huo ufisadi. Na kama akifukuzwa uanachama, that means uchaguzi mkuu lazima uitishwe, maana JK atakuwa amepoteza sifa kuongoza nchi kupitia SISIEMU. Sina hakika SISIEMU wako tayari kujivua hilo gamba.
 
Mwanakijiji bado anaamini haya aliyoyaandika mwaka 2009? ofkoz hii ilikuwa kabla ya CCJ au sio nabii?
 
lol

We will see.

InshaAllah tuombe uzima. We will be here November 2016. Hopeful this thread will be around.

hiyo article ilichapwa August 2009, kila kitu kinatokea sasa, yaani mzee MM aliona mambo ambayo wanaCCM wanayona leo na kuanza kutimuana, we unaongea hadithi za 2016....we mwenzetu wa wapi? seems hauko connected, 2009 MM kaandika, 2011 CCM washajua hali mbaya we mwezetu bado unasubiri 2016? kha! lakini endelea kusubiri dogo nisikukatishe tamaa bure!
 
..muda wote nimekuwa nikifikiri kwamba tatizo ni UTENDAJI WA RAISI na BARAZA LA MAWAZIRI ndiyo unaoathiri UMAARUFU WA CCM.

..kama kweli JK yuko serious, sambamba na haya mabadiliko ya sekretariet ya CCM, avunje baraza la mawaziri na safu nzima ya viongozi wa juu serikalini na kuiunda upya.
 
Back
Top Bottom