Redio zetu zimetawaliwa na vipindi vya michezo

hahahah siku hizi ni Kabumbu tu na uchambuzi wa kijanja kijanja mixer kugoogle kwingi. Media imeona fursa kwenye michezo hasa mpira wa miguu maana hata hivyo vipindi vya michezo unavyosema zaidi ya asilimia 90% ni mpira wa miguu, chache inayobaki ndio michezo mingine ila kupata hata mchambuzi wa masumbwi, mpira wa kikapu, mpira wa pete au wa wavu aisee ni ngumu sana.

karibia wote ni mpira wa miguu tu, unaweza kukuta kipindi cha michezo kimesheheni wachambuzi wanaojiita ‘manguli' ila hamisha swali toa kwenye mpira wa miguu peleka kwenye mchezo wowote ule hata mpira wa kikapu uone jinsi wanavyopoteana hamna wanachojua wote wamemeza mipira tu, na u-Simba na U-Yanga mwingi.

Itoshe kusema kuwa hapa Tanzania tuna vipindi vingi sana vya mpira wa miguu ila tuna vipindi vichache sana vya michezo.
 
Walianzisha clouds segment ya michezo kwenye kila kipindi, kila redio ikaiga.
Any way wanawapa watu wanachopenda.
Mwanzo vipindi vya michezo vilikuwa usiku tu, EFM wakaleta asubuhi kila redio ikaiga sasa hivi si mchana si usiku wala asubuhi ni michezo tu
 
Basi kama Ni hivyo mbona Hakuna vipindi vya michezo saa Tisa usiku kwasababu Kuna watu wanafanya kazi muda huo.


Katika nchi hii working hours ni kuanzia asubuhi Hadi jioni. Wanaofanya kazi usiku Ni idadi ndogo.

Kama asilimia 70 ya wananchi wanajihusisha na kilimo. Ina maana hujui muda wa kujihusisha na kilimo. Au kilimo kwenu mnajishughulisha usiku.

Redio inaweza kusikilizwa hata wakati watu wanafanya kazi na ndio maana hata vijijini jembe linatembea huku redio inapokea matangazo na hii desturi ipo tu mpaka kuna kifaa kimojawapo cha kupokelea mawimbi hayo kilibatizwa jina redio mkulima!!,

vivyo hivyo kwenye maduka, migahawa, sarijala, n.k ni kawaida kukuta redio inatwanga na kazi inaendelea
 
sijui tunaenda wapi.zaman redio ilikuwa na vipindi vya kilimo,.twende shamban,faida za ufugaji.siku hizi ni mpira kutwa nzima pumbavu
 
Back
Top Bottom