Redio za FM zinaajiri watangazaji wasio na taaluma

Dida ana kipaji gani
Kwakweli sijajua, maana sijawahi kumsikilza kabisa, Ila mie nachomaanisha ni kuwa Kama unakipaji Basi sio mbaya kukiendeleza kwa kusomea, naamini kuna mambo mengine mengi utajifunza juu ya hiyo taaluma. Na ndio maana tunaweza kusema kiongozi anazaliwa na kutengenezwa kwa wakati mmoja.
 
Kuna sababu nyingi, na zote zina mchango tofauti tofauti kwa hizi redio kuwa kama zilivyo leo. Zifuatazo ni baadhi

1. Redio ili iweze kujiendesha inahitaji matangazo, na ili ipate matangazo inabidi iwe inasikilizwa, na ili isikilizwe inabidi ivutie, na ili ivutie inahitaji kuwa na watangazaji ama vipindi vinavyovutia. Sasa, si kila wakati 'mvuto' wa mtangazaji utaambatana na elimu. Kuna watangazaji wanaovutia ila hawana elimu, kuna watangazaji wana elimu ila hawana mvuto kwa wasikilizaji. Ni mara chache sana utampata mtangazaji mwenye mvuto na akawa pia na elimu nzuri. Mfano mzuri ni RTD. Hawa wengi wao walikua na taaluma ila hawana mvuto ndio maana humu ndani wengi wetu tukiulizwa ni lini mara ya mwisho kusikiliza RTD tutajikuta tunajibu ni mwaka 1999! Pia, si lazima kila mtangazaji awe na elimu, ndio maana kuna vipindi vya aina mbali mbali. Mfano, huwezi kumpa mtangazaji mbumbumbu hata kama ana mvuto kiasi gani aende kuchukua ama kuripoti ama kufanya mahojiano katika mikutano muhimu ama ya kimataifa! Ila unaweza kumtuma mtangazaji mbumbumbu mtaani kwa masela akahoji, akaripoti etc.

2.Cheap labour: Radio ni biashara. Kama unaweza kupata usikilizwaji kwa mvuto wa mtanagazaji cheap, why employ the dearer na madigrii yake? Na uzoefu unaonesha kuwa wasio na elimu, hata malipo yao si makubwa ndio maana wanakua wengi katika radio za fm.

3. Market segment: Wakati mwingi, watu hupenda kuwa karibu ama kuwasikiliza wale wanaofanana nao, ama wenye viashiria vya kufanana nao. Ukiwa na masela, watapendelea mtangazaji msela n.k. Ukiwa na serious people, watapendelea serious people. So, majority ya wasikiliza radio ni vijana age ya '15 - 35' ambao pia wengi ya hao elimu na uelewa wao ni huo huo usio wa juu sana. Na katika jamii, hata leo, ingia barabarani ama katika mikutaniko mingi, angalia wenye 'ear phones' ni akina nani na fuatilia wanasikiliza nini! I can assure you, majority watakua vijana wa hiyo age bracket na watakua wanasikiliza miziki ama radio hizo hizo za fm! mara chache utakuta wanasikiliza taarifa za utafiti ama taarifa makini!

4. Kutokuiva kwa wasomi. Wasomi wenye digrii zao za habari hawana ile kuiamini ama mvuto unaotakikana katika soko la leo. Matokeo yake mtu anakuja ana elimu kubwa, anataka mshahara mkubwa ila soko la redio halitaki kumsikiliza. Na soko ni vijana hawa ama wasikilizaji hawa hawa wanaolalamika hapa.

Ndefu, ila ndio ukweli wenyewe!
Uko sahihi sana mkuu
 
Utangazaji ni kipaji,Ila ni vema kipaji hicho kikaenda sambamba na elimu,Mana wanasema kipaji bila elimu ni sawa na bure
Acha ujinga utangazaji hauwezi kuwa kipaji tu, nenda kaangalie watangazaji wa tv za Kenya citizen, KTN, K24 wanavyofanya kazi,vile viwango vina msingi katika Elimu/taaluma, wafundishwa vizuri.
Huwezi kwenda BBC kwa vile tu unasema unakipaji,

Hapa kwetu hawa sio watangazaji ni walopokaji tu, radio za FM ni kama vijiwe vya kihuni, Wewe fikiria baba levo, Zembwela, Didah eti hawa ni watangazaji, wana masauti mabaya, wanaongea kihuni, mwanzo mwisho ni mada za hovyo tu,

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kabisa mtoa mada,yani kuna matangazaji vilaza hadi basi,yani mtangazaji anashindwa kutambua hata nchi za Afrika..Kweli!!!
 
Kuna sababu nyingi, na zote zina mchango tofauti tofauti kwa hizi redio kuwa kama zilivyo leo. Zifuatazo ni baadhi

1. Redio ili iweze kujiendesha inahitaji matangazo, na ili ipate matangazo inabidi iwe inasikilizwa, na ili isikilizwe inabidi ivutie, na ili ivutie inahitaji kuwa na watangazaji ama vipindi vinavyovutia. Sasa, si kila wakati 'mvuto' wa mtangazaji utaambatana na elimu. Kuna watangazaji wanaovutia ila hawana elimu, kuna watangazaji wana elimu ila hawana mvuto kwa wasikilizaji. Ni mara chache sana utampata mtangazaji mwenye mvuto na akawa pia na elimu nzuri. Mfano mzuri ni RTD. Hawa wengi wao walikua na taaluma ila hawana mvuto ndio maana humu ndani wengi wetu tukiulizwa ni lini mara ya mwisho kusikiliza RTD tutajikuta tunajibu ni mwaka 1999! Pia, si lazima kila mtangazaji awe na elimu, ndio maana kuna vipindi vya aina mbali mbali. Mfano, huwezi kumpa mtangazaji mbumbumbu hata kama ana mvuto kiasi gani aende kuchukua ama kuripoti ama kufanya mahojiano katika mikutano muhimu ama ya kimataifa! Ila unaweza kumtuma mtangazaji mbumbumbu mtaani kwa masela akahoji, akaripoti etc.

2.Cheap labour: Radio ni biashara. Kama unaweza kupata usikilizwaji kwa mvuto wa mtanagazaji cheap, why employ the dearer na madigrii yake? Na uzoefu unaonesha kuwa wasio na elimu, hata malipo yao si makubwa ndio maana wanakua wengi katika radio za fm.

3. Market segment: Wakati mwingi, watu hupenda kuwa karibu ama kuwasikiliza wale wanaofanana nao, ama wenye viashiria vya kufanana nao. Ukiwa na masela, watapendelea mtangazaji msela n.k. Ukiwa na serious people, watapendelea serious people. So, majority ya wasikiliza radio ni vijana age ya '15 - 35' ambao pia wengi ya hao elimu na uelewa wao ni huo huo usio wa juu sana. Na katika jamii, hata leo, ingia barabarani ama katika mikutaniko mingi, angalia wenye 'ear phones' ni akina nani na fuatilia wanasikiliza nini! I can assure you, majority watakua vijana wa hiyo age bracket na watakua wanasikiliza miziki ama radio hizo hizo za fm! mara chache utakuta wanasikiliza taarifa za utafiti ama taarifa makini!

4. Kutokuiva kwa wasomi. Wasomi wenye digrii zao za habari hawana ile kuiamini ama mvuto unaotakikana katika soko la leo. Matokeo yake mtu anakuja ana elimu kubwa, anataka mshahara mkubwa ila soko la redio halitaki kumsikiliza. Na soko ni vijana hawa ama wasikilizaji hawa hawa wanaolalamika hapa.

Ndefu, ila ndio ukweli wenyewe!
Uko sahihi sana m
Mpaka sasa nashindwa kuelewa EFM waliwachukua kina Steve Nyerere, Kingwendu, Roma, Mpoki na wapuuzi wengine kwa vigezo vipi. Yaani jamaa kwanza hawajitambui na zéro kichwani na ni wapotoshaji wakubwa. Nchi za wenzetu hii station inachukuliwa hatua kali za kisheria kwa upotoshaji, watangazaji wengi wa hizi redio ni wa kukamatwa na kuulizwa walisoma wapi kama hawana elimu ya utangazaji watiwe ndani.
Kwani ni lazima kuisikiliza hiyo redio si sikiliza radio nyingine, mimi nafikiri elimu inapply kwenye baadhi ya vipindi tena vichache, hivi kina Michael Owen, Garry Neville na wengineo wamesomea wapi utangazaji?
 
Wasomi wamekuwa ni wasomi wa kulalamika lalamika tuu bila hata kuwa na solutions za matatizo yao, sasa kweli mtangazaji uliye bukua adi una PHD au master's degree, lakini kiutangazaji umeachwa mbali na mbwiiga, huna ubunifu, huna mvuto wa utangazaji, yaani ni majanga matupu, leo unalalama ohooo

Akina mbwiiga wanatuzibia riski!!
Kwani mtoa Uzi amesemaje???.
 
Sasa wewe Rogwa anzisha Radio au TV kisha ajiri hao unaowaita Wasomi pekee,
Hasara utakayopiga utaongea pekeyako barabarani.

Wengi tusichokijua,
Hivyo vyombo vinaanzishwa na Wafanyibiashara na lengo lao ni kutengeneza faida,

Kwahiyo, Wahudumu shurti wawe wenye kuleta tija si pungufu ya hivyo.
 
Ishu hapo Ni wizara husika kusimamia miongozo ya uendeshaji wa taaluma husika.

Hata nchi zilizoendelea fuatilia Hadi nyimbo za kufokafoka, wanamuziki wengi Kama siyo wote, wamepitia elimu ya sanaa kwanza, ndipo wakaingia katika kutafuta riziki.

Si hao wachekeshaji tu wanaovuruga taaluma ya habari, Kuna wanaoshika mic viwanjani na kuuliza maswali ya kebehi na kejeli kwa walimu wa vilabu, mpaka unasema wenye taaluma yao wanakaaje kimya katika haya?

Maoni ya mashabiki yenye kuibua chuki,dharau, kushusha staha kwa taasisi Kama vilabu, na viongozi wake, yanaruhusiwa kwenda hewaní, tena yanageuzwa "jingle" kabisa...!

Charles Hillary pamoja na kuwa na kipaji alipokuwa mazoezini RTD miaka hiyo, anakwambia ilimchukua muda mrefu kuruhusiwa kusikika. Na anakwambia alisota sana bila kujua,lini ataruhusiwa kwenda hewaní.

Siku hizi Sasa....!!!!
 
Consumers ndio sisi tunaolalamika hapa
Mbona hauchukui hatua ya kuacha kuisikiliza hizo redio , mimi nawakubali ndio maana nawasikiliza , najua ni ngumu kuwa na opinion moja maana hii sio hesabu 2! = 4 worldwide
 
Back
Top Bottom