REDET nyingine? .... Utendaji wa Serikali kuchunguzwa tena

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Utendaji wa Serikali kuchunguzwa tena

BARAZA la Kitaifa la Usimamizi wa Mpango wa Umoja wa nchi za Afrika wa kutathmini utendaji wa serikali zake (APRM), limeandaa utafiti mwingine kuchunguza utendaji kazi wa serikali.

Katibu Mtendaji wa APRM, Profesa Daudi Mukangara aliliambia gazeti hili jana kuwa utafiti huo utagharimu Sh400 milioni na unatafarajiwa kukamilika Mei mwakani.

Alisema zaidi ya watalaam 20 wameanza kazi ya kuzungukia makundi mbalimbali ya watu kupata maoni kuhusu utendaji wa serikali, maoni ambayo yatatumika kutoa tathmini ya jumla ya uwajibikaji wa serikali ya awamu ya nne kwa wananchi wake.

"Utafiti peke yake utagharimu Sh400 milioni lakini mradi wote wa APRM utagharimu Sh2.5 bilioni. Tayari utafiti umeanza na wataalam wanapita maeneo mbalimbali kupata maoni ya watu," alisema. Akifafanua kuhusu utafiti huo, alisema lengo ni kupata maoni ya watu kuhusu utendaji wa serikali ili kuipa changamoto na fursa ya kujisahihisha katika maeneo yatakayobainika kuwa na mapungufu.

Alisema wakati utafiti huo unatarajiwa kukamilika Mwezi Mei mwakani, mradi mzima wa APRM utakamilika kati ya mwaka 2009 na 2010. Alisema watalaam wa utafiti huo wanapita kuuliza masuali kadhaa kuhusu utendaji wa serikali katika sekta zote na kupata maoni ya JINSI serikali inavyoweza kujisahihisha na kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Akizungumzia faida ya utafiti huo kwa mwananchi wa kawaida, Profesa Mukangara alisema utamsaidia kuongeza uelewa wa utawala na utawala bora nchini mwake, kushiriki kwa uelewa na kutathmini mwenendo wa nchi yake kiutawala.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walioshiriki semina ya uelimishaji wa APRM walionyesha wasiwasi wao juu ya utafiti huo, wakisema kuwa bila maandalizi ya kutosha unaweza kuwa ni moja ya sehemu ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Juma Duni Haji wa Chama cha Wananchi (CUF) alisema Baraza la Usimamizi Kitaifa la APRM linatakiwa kuendesha utafiti huo kwa uwazi na kuwahusisha watu wengi zaidi ili kupata maoni ya watu mbalimbali kuhusu utendaji wa serikali.

Joseph Selesini wa NCCR-Mageuzi alisema kuna haja ya kuangalia mtazamo wa utafiti huo kabla ya kuunza ili kukwepa kufanya utafiti wenye lengo la kuijenga serikali badala ya kueleza upungufu uliopo na kuisaidia kujisahihisha.

"Kazi ni nzuri lakini tuangalie watu wanaoifanya ili kujiridhisha kwamba inafanyika kwa maslahi ya taifa kwani tafiti nyingi zimekuwa zikifanywa kuisafisha serikali," alisema. Naye Nathaniel Mlaki wa Chama kisichokuwa na usajili wa kudumu cha Social Demokratic alisema washiriki katika utafiti huo, wanatakiwa kuwa wazalendo ili kuufanya kiusahihi kwa maslahi ya taifa.

Alisema uzoefu unaonyesha kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wajumbe katika tafiti na kamati mbalimbali zinazoundwa kuchunguza mambo ya kitaifa kukosa uzalendo kwa kushindwa kusema ukweli jambo ambalo kama halitadhibitiwa litaathiri dhana nzima ya kuendesha utafiti huo.

"Nchi hii tuna utamaduni wa kutosema ukweli, watu wanafanya kazi kwa kulindana badala ya ukweli na hii ni hatari kwa matokeo ya utafiti huo endapo halitadhibitiwa" alisema.

Salum Msabaha wa CCM alisema Chama cha Mapinduzi kinasubiri matokeo ya utafiti huo ili kujua mapungufu ya serikali yake na mafanikio na kuweka mikakati ya kuboresha huduma.

Hivi karibuni Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (Redet) wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ulitoa ripoti ya utafiti wake juu ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne ambayo ilionyesha kuwa utendaji wa Rais Jakaya Kikwete bado uko juu lakini mawaziri na taasisi za serikali hazikufanya vizuri katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
 
Naambiwa kwenye mkutano huo wa jana kuwa Tambwe Hizza alitia aibu sana kwani kumbe hajui kuzungumza kiingereza na ilimuwia vigumu kuzungumza hadi pale walipoanzisha kuzungumza kiswahili ndipo akawa wa kwanza kunyoosha kidole kwa wale wanaomjua huu ni ukweli ama ni udaku?
 
Wakulu, ambacho sijui hayo mabilioni yote ya Tafiti hizi, ni kodi zetu? ama kuna sehemu wanayachota??
 
Naambiwa kwenye mkutano huo wa jana kuwa Tambwe Hizza alitia aibu sana kwani kumbe hajui kuzungumza kiingereza na ilimuwia vigumu kuzungumza hadi pale walipoanzisha kuzungumza kiswahili ndipo akawa wa kwanza kunyoosha kidole kwa wale wanaomjua huu ni ukweli ama ni udaku?


Kama ni kushindwa kuongea kiingereza tu hiyo sio aibu. Sio lazima ajue hiyo lugha. Cha msingi aliongea nini hasa baada ya kupata nafasi ya kuongea kiswahili, then hapo tunaweza ku-judge kama alichemsha au la. Lakini hatuwezi kum-judge kwa kushindwa kuongea kiingereza ambayo ni lugha ya malkia na watu wake!
 
Wakulu, ambacho sijui hayo mabilioni yote ya Tafiti hizi, ni kodi zetu? ama kuna sehemu wanayachota??

Mapesa ya wazungu haya baba! Serikali yako haijawahi kuona utafiti kama ni jambo la muhimu. Ndio maana wazungu tutawabeza sana lakini ukweli ni kwamba tunajibeza wenyewe madamu tunaendelea kuishi kwa hela zao.
 
Naambiwa kwenye mkutano huo wa jana kuwa Tambwe Hizza alitia aibu sana kwani kumbe hajui kuzungumza kiingereza na ilimuwia vigumu kuzungumza hadi pale walipoanzisha kuzungumza kiswahili ndipo akawa wa kwanza kunyoosha kidole kwa wale wanaomjua huu ni ukweli ama ni udaku?

?????????
huko siko,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom