REDET na Synovate wako wapi baada ya uchaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REDET na Synovate wako wapi baada ya uchaguzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Dec 19, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Tulisema kwamba hawa walikuwa ni watu wenye njaa wakitafuta nafasi ya kula.

  Walianza akina REDET ya Benson Bana. Pole pole! Baadaye ikazuka Synovate. Wote wakijinadi ni watafiti lakini theme yao kubwa ilikuwa taarifa za nani anapendwa na nani hapendwi na wapiga kura.

  Sasa tena hawasikiki kabisa! yaani utafiti wao uliishia tarehe ya kupiga kura?

  Benson Bana, kama mwalimu wa University sasa hivi anajisikiaje baada ya kutumika kama toilet paper chooni ktk kipindi chote cha uchaguzi?
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanakula pension kwa miaka minne, 2015 watarudi tena kuomba kazi kwa waajiri
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mchunguzi nilidhani utaulizia ile sijui hata inaitwaje ilompa slaa kuwa atashinda.hivi ofisi zao ziko wapi sijui
  Leo unaulizia watafiti waliobobea
   
 4. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana bwana paulss. Hili jina sijui ulitaka kuandika kilatini ukachapia? Kilatini ni paulus.

  NA hata hivyo, polekwa swali lako "la kizembe" ulilouliza badala ya kutoa majibu kwa swali lililotangulia. Naona umesahau tafiti za kishabiki kama za REDET na SYNOVATE. Kimsingi...nani muongo kati ya hawa?

  REDET na SYNOVATE walisema uongo mtakatifu....walisema DR SLAA atapata around 10%....maajabu NEC ikampa 26....% baada ya yeye kuwataka waache kutangaza matokeo ya uchaguzi wao badala yake watangaze yale ya wananchi

  Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) ikasema kama kura hazitaibwa na hakutakuwa na udanganyifu... Dr Slaa 45%(akapata 26...%), Lipumba 10% (unajua alichopata).

  Kimsingi...marginal difference kati ya tafiti hizi inatuletea mashaka makubwa ukiangalia utafiti wa REDET na SYNOVATE. Hata baada ya kuiba (TCIB wako close to the answer and therefore tunawaamini zaidiiii)

  Upo hapo? Kwa mda huu SYNOVATE na REDET wanakutana na JK kwa nafasi mbali mbali kuangalia namna ya kuanza kudanganya uchaguzi wa serekali za mitaa miaka mitatu ijayo. Kumbuka CCM huwa wanaanza kufikiria uchaguzi imediately baada ya wa awali kumalizika maana wanajua watarudi kwa wananchi kuwadanganya kama walivyozoea..

  VURUGU za ARUSHA NI EVIDENCE. Lukuvi ameonyesha uelewa kwa kujibu kuwa "hatacoment kitu maana issue imekaa kisheria kuliko kisiasa....akijua UCAHGUZI WA MEYA NI BATILI, akijua FORAM haikutimia akijua CCM iMEHUSIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KUPIGWA KWA LEMA...

  Akafu kosa CCM wanalofanya...ni kama walivyofanya kule karatu KUMTEUA mwenye jina la SLAA ili wananchi wachangayikiwe....hapa ARUSHA kwa kujua Godbles na ni mchaga basi wakaleta meya wao mchaga wakidhani itasaidia maana wataongea lugha moja...

  HApa ni kuruka maji na kukanyanga...........

  Ule
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Yote katika yote ukweli si umeshawekwa wazi? Dr Slaa 62% na kikwete ngapi vile?
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa unataka wafanye nini! kazi yao ilikuwa kuandaa umma wa watanzania kuyakubali matokeo yaliyochakachuliwa. Hawakuweza kufanikiwa kwa hilo kwasababu waligundulika mapema. Inavyoelekea, hivi sasa wako kwenye harakati za kujitokeza katika sura nyingine.
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  REDET na Synovate wanaweza kuwa ni watafiti wazuri, tatizo lao ni kukubali kulawitiwa na wanasiasa bila hata kinga ya kulinda utu wao. Nasi hatuna njia nyingine ya kuwaelewa mbali na yale waliyokuwa wakiyasema hadhalani.

  Mimi naweza kwenda kinyume na maadili ya kazi yangu na nikafahamu hivyo na kuona aibu kwa hayo. Hawa REDET na Synovate hapana.

  Nilikutana na Benson Bana hapo UD, sikuamini kama kweli kichwani ziko fiti na ikabidi nigeuke kuangalia kama suruali yake inafunika makalio. Maana tunaweza kusumbuliwa na kichaa eti!
   
 8. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hiyo nimeipenda
   
 9. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hawa wamekiuka ethics za utafiti wanatakiwa kufungiwa na wanataaluma (katika association yao) la sivyo wanaidhalilisha taaluma. Kwa vile ni jambo limelalamikiwa sana na wadau inatakiwa association ichunguze uhalali wa research yenyewe na kisha waje na jibu la kuwa acquit au kuwa convict otherwise basi hakuna profession. Na kila profession ina ethics zake!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. k

  kibunda JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanajamii, mbona zile kura za maoni hawatoi tena? Au ni kutokana na makuwadi wao kuwa katika hali mbaya? Tumeona Kenya, rais aliyeko madarakani amekuwa wa tano kama uchaguzi ungefanyika jana. Kama wakisurvey kura ya maoni hapa kwetu hali itakuwa mbaya zaidi. Mnalionaje wadau?
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  kuhusu nini? usiwashtue maana hawana update! utashangaa wanakuibulia kura ya maoni ya loliondo.
   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Nahisi kuna sababu kadhaa ambazo zinafanya wasifanye utafiti kwasasa hapa Tanzania:

  1. Kipindi cha kula na kukusanya mauzo ilikuwa kipindi cha uchaguzi,maana hapo walipewa pesa za kusambaza propaganda kuwa watu wanaipenda CCM(napata kichefuchefu nikitamka hichi chama)
  2. Wakifanya utafiti sasa hali itakuwa yakutia majonzi kwa JK na uongozi wake
  3. Wanaogopa wakichakachua kwasasa watanzania wanahasira watawapiga mawe...
   
 13. e

  emalau JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  They are proxies so they are waiting for instructions from Salva Rweyemamu
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawajaambiwa na mkuu wao,JK
   
 15. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Wakuu,

  Redet walikua mstali wa mbele kutoa tathmini ya hali ya kisiasa kipindi cha uchaguz wakijinadi kwa chama cha magamba kuwa kinamvuto... Tunaomba wafanye tathmin ya hali ya kisiasa kipindi hiki ccm na 'kujivua gamba' Vs CDM Operation twanga kote kote.!
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hizo tathmini zao huwa siziamini maana sijasikia hata mtu mmoja ninayemjua amehojiwa na hao jamaa.

  Pili sidhani kama wana Statisticians wa ukweli kutoa conclusion za maana watakuwa kama maswali ya vipima joto tu:biggrin1:
   
 17. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waholanzi wamesitisha msaada kwa redet baada ya kugundua kuwa pesa hizo zinatumika kuwapamba chama cha magamba badala ya kufanya kazi iliyokusudiwa ya kukuza demokrasia.

  Lakini hata kama wangekuwa na uwezo wa kufanya huo utafiti, kwa jinsi wasivyo na aibu huyu Mkandara na mafisadi wenzie wanaweza kufanya tathmini leo na bado wakakwambia Magamba bado wanapendwa kwa zaidi ya 90%.
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280

  au kwenye red wakashusha kidogo hadi 70%
   
 19. i

  ibange JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kungekuwa na taasisi huru ifanye tathmini si REDET
   
 20. Y

  Yetuwote Senior Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana pesa ya kufanyia utafiti
   
Loading...