REDET Kutafiti Utendaji wa Kikwete toka aanze Awamu ya nne

mkandara unataka kutuambia nini? kwamba ni jukumu letu tanzania inalala hakuna maendeleo na sio kosa la benjamini au kikwete?

inawezekana ikawa hatujui wajibu wetu kwa nchi, lakini nchi pia haijui wajibu wake kwetu, na hilo ndio tatizo kubwa zaidi ya hilo la kwanza. kwa sababu ni kazi ya serikali kutuelewesha kuhusu huo wajibu wetu na sio kukaa tu kulaumu watu hawajui wajibu wao
 
Sio sahihi kuendelea kufikiria kuwa wananchi hawajui majukumu ya viongozi wao.Hayo yalikuwa ni mambo ya zamani sana wakati information ilikuwa haipatikani.Kuna umuhimu gani wa kujua majukumu ya kiongozi wakati unajua wizi wanaoufanya?Haya mambo ya ufisadi yanayoendelea sasa hivi,ingekuwa ni wakati wa Mwalimu nani angejua? Kupata information kama hii was only thru the word of mouth,na hata hapo watu walikuwa wanaogopa kuongea.Sisemi kuwa whats happening now was happening then,ila tu kuwa kama ingekuwa ni wakati ule.Sasa hivi unaweza kupata information yeyote thru internet,leo hii hata uki Google mafisadi wa Tanzania,i'm sure utapata pages nyingi tu za kusoma,mikataba ya Buzwagi,Richmond,list ya walaji wa BoT nk.Bado kuna magazeti mengi tu ambayo yanadiriki hata kutaja jina la kiongozi kuwa ni mla rushwa,tena kiongozi wa juu!Watanzania wamechoka kwa sababu kila siku wanasikia jipya kuhusu serikali hii.Wamechoka kwa sababu maisha bora walioahidiwa hawaoni hata dalili,wao wanaona kiongozi wao anakwenda majuu kila kukicha akiongozana na wafanya biashara wezi.(hivi,where is Dr Shein? The last i heard alikuwa anafungua bucha)
Mpaka inafikia CCM kulipa watu kwenda airport kumpokea JK?
Huko Italy nasikia anawaambia waitaliani waje kuwekeza Tanzania maana 80% ya Hoteli zote Zanzibar zinamilikiwa na wataliani!Yaani sasa nadhani wanataka iwe 100%
 
wana bodi,
jana nilikuwa maeneo ya chuo kikuu cha Dar es salaam nikakuta REDET Wanakamilisha semina elekezi kwa ajili ya utafiti wa tathimini ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne,
kwa kifupi utafiti huo utaanza kesho na utafanyika kwa siku tano eneo lote la TANZANIA..
nilijaribu kuchukua questionaire niilete hapa ila nilinyimwa..
ninafanya jitihada ya kuipata na kesho naweza kuiweka hapa.
kila mtafiti atakuwa analipwa dola 25 kwa siku.
Niice
 
Back
Top Bottom