Redet blah blah again! Kikwete anakubalika mawaziri hawakubaliki!

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,534
8,619
DR Lillian killiAn ...MTAFITI wa REDET Kaja na utafiti wake ..tena ..at this time ,utafiti ni wa mwaka jana november 2008...

HABARI zaidi zitapatikana magazeti ya kesho....
 
UPUUZI MTUPU! :( Kawahoji Watanzania wangapi mpaka kufikia conclusion hiyo!? Mawaziri wameteuliwa na Kikwete kama wao hawakubaliki ina maana na yeye pia kazi imemshinda maana anateua mawaziri wabovu.
 
UPUUZI MTUPU! :( Kawahoji Watanzania wangapi mpaka kufikia conclusion hiyo!? Mawaziri wameteuliwa na Kikwete kama wao hawakubaliki ina maana na yeye pia kazi imemshinda maana anateua mawaziri wabovu.


Kura za REDET zinatumika kisiasa ..NA mara zote huwa wanatangaza matokeo ktokana na hali ya siasa ya wakati uliopo..kama sasa bwana mkubwa ameelemewa ..wanafikiri zitamsaidia..

kitu kimoja cha ajabu ambacho sijapata kukiona kwenye serikali nyingine zaidi ya za kifalme...huwezi tenganisha ...utendaji wa serikali na rais kwenye nchi yetu ambayo yeye ndio mkuu wa nchi na serikali..

Uingereza au nchi za mfume wa ufalme wa aina hiyo ndiko ambako utendaji wa WAZIRI MKUU hauendani na UFALME ...hapo unakuta waziri mkuu anaweza kuwajibishwa bila kuharibu ufalme......

simply kama mawaziri ni wabovu ....na rais pia ni mbovu!!!....waache kuwaonea mawaziri..kuna mawaziri wengi wazuri tu ...wasitake kuwaharibia sifa!!
 
Subiri aibu wataipata 2010, kwani nahisi hata kikwete akigombea na jiwe pembeni, kama hatoiba kura 50% hapati ng'o!
 
Utaifiti wa REDET waonyesha umaarufu wa Kikwete waporomoka

Na Boniface Meena

Mwananchi Newspaper

UMAARUFU wa Rais Jakaya Kikwete unaonyesha kuendelea kuporomoka, kwa mujibu wa ripoti ya matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia nchini (Redet).

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa utendaji kazi wa Rais Kikwete, ambaye aliingia madarakani mwaka 2005 kuongoza serikali ya awamu ya nne, umeshuka kwa asilimia 28 mwaka jana ukilinganisha na matokeo ya utafiti ya mwaka 2006.

Pamoja na kushuka kwa asilimia hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi waliohojiwa wanaridhika zaidi na utendaji wa Rais Kikwete, kuliko wanavyoridhishwa na utendaji kazi wa baraza lake la mawaziri ambalo utendaji wake umekubaliwa na asilimia 18 tu.

Kwa mujibu wa utafiti huo, watu wanaoridhika sana na utendaji kazi wa Kikwete ni asilimia 39.5 tu kulinganisha na asilimia 69 iliyoonyesha kuridhika naye sana mwaka 2006.

Akitoa taarifa ya utafiti huo jana kwa waandishi wa habari, mtafiti mkuu wa Redet, Dk Benadetha Killian alisema kuwa ukilinganisha takwimu za Oktoba 2006 na Oktoba 2007, asilimia ya wale wahojiwa ambao wanasema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Rais Kikwete imepungua kutoka asilimia 69 Oktoba 2006 hadi asilimia 44 mwezi Oktoba 2007 na sasa imefikia asilimia 39.5 hadi Novemba mwaka jana.

Dk. Killian alisema kuwa ukichambua undani wa mwenendo huo utaona kwamba wakati idadi ya wanaosema wanaridhika sana iliteremka kwa tofauti ya asilimia 23, kati ya mwaka 2006 na 2007, kasi ya kutoridhika sana imepungua ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2007/08 wakati idadi ya wahojiwa ambao walisema wanaridhika sana ilipungua kwa tofauti ya asilimia 4.5 tu.

Kwa mujibu wa Dk. Killian, ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya utafiti huo ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na sampuli ilichaguliwa katika ngazi tatu ambazo ni wilaya na vijiji/mitaa na katika kila ngazi sampuli ilipatikana kwa kutumia mtindo wa sampuli nasibu.

"Katika kila wilaya, watafiti walitakiwa kuchagua vijiji viwili (kwa maeneo ya shamba) au mitaa miwili (kwa maeneo ya mjini) kwa kutumia njia ya sampuli nasibu. Katika kila wilaya, jumla ya watu 50 walichaguliwa kwa ajili ya kuhojiwa, 25 kutoka kila kijiji/mtaa," alisema.

"Na kati ya watu 50 waliohojiwa katika kila wilaya, 25 walitakiwa wawe wanawake na wengine 25 wawe wanaume na uchaguzi wote wa wahojiwa ulifanyika kwa kutumia njia ya sampuli nasibu."

Alisema ukiacha masuala mengine ya utendaji wa mawaziri, waliohojiwa walitakiwa kutoa tathimini yao kuhusu utendaji kazi wa Rais Kikwete katika kipindi cha takriban miaka mitatu ya utawala wake kwa kutoa maoni yao kama wanaridhika sana, wanaridhika kiasi au hawaridhiki.

Dk. Killian alisema kati ya wote waliohojiwa, asilimia 39.5 walisema wanaridhishwa sana na utendaji wa Rais Kikwete, asilimia 39.0 walisema wanaridhika kiasi na asilimia 19.3 walisema hawaridhiki na utendaji kazi wa mkuu huyo wa nchi.

Alisema hata hivyo kwa ujumla, matokeo ya utafiti wa Novemba mwaka jana yanaashiria kwamba, utendaji kazi wa Rais Kikwete bado unaonekana kuridhisha idadi kubwa ya watu pale ambapo makundi mawili ya wahojiwa yanapojumlishwa pamoja yaani wale wanaosema wanaridhika sana asilimia 39.5 na wale wanaosema wanaridhika kiasi asilimia 39 ikiwa inafanya idadi hiyo ya wahojiwa wote kufikia asilimia 78.5.

Dk Killian alisema sababu za kuridhika au kutoridhika na utendaji kazi wa serikali ya Rais Kikwete ni kutoridhishwa na ahadi yake ya kuboresha hali ya maisha. Asilimia 31.0 ya waliohojiwa walisema ameshindwa kuboresha hali ya maisha, wakati asilimia 24 walisema hajatimiza ahadi na asilimia 12.2 walisema hafuatilii utekelezaji wa ahadi zake.

"Sababu nyingine zilizotolewa na wahojiwa ni kuchagua viongozi wasiofaa asilimia 10.8, ameshindwa kupambana na rushwa asilimia 8.0, lakini pamoja na kwamba utafiti huu ulifanywa kipindi ambacho "vigogo" walikuwa wanapelekwa mahakamani kuhusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na wengine kutuhumiwa na wizi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA), ni asilimia 6 tu ndiyo waliotaja moja kwa moja suala hili kama sababu ya kutoridhishwa au kuridhishwa kiasi na utendaji kazi wa rais," alisema.

Alisema sababu za wananchi kutoridhika na utendaji wa serikali iliyo madarakani ni kutofuatilia utekelezaji asilimia 30.7, serikali kujihusisha na rushwa asilimia 29 na inapitisha mikataba mibovu asilimia 10.0.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa bunge ndio linaongoza kwa kutoridhisha wananchi baada ya asilimia kubwa ya waliohojiwa kueleza kuwa hawaridhishwi na taasisi hiyo ya kutunga sheria.

Bunge limeonekana kutoridhisha wengi tofauti na taasisi za serikali kama polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, serikali za mitaa na kadhalika.

Dk. Killian alisema bunge linaongoza kwa kuwa na asilimia kubwa ya kiwango cha kutoridhika ambacho ni asilimia 77.4, ikifuatiwa na serikali za mitaa asilimia 75.6 wakati baraza la mawaziri linashika nafasi ya tatu kwa asilimia 63.

Kwa upande wa utendaji kazi wa Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 44 tu ya wote waliohojiwa wanaridhika sana, wakati asilimia 24 wanaridhika kiasi na asilimia 26 walisema hawaridhiki. Alisema kiwango cha utendaji wa Rais Karume kimeonekana kupanda kwa asilimia 9 ukilinganisha na utafiti wa Oktoba 2007 wakati asilimia 35.5 tu ilimkubali baada ya kuporomoka kutoka asilimia 47.8 aliyopata kipindi cha hadi Oktoba 2006 na baadaye kupanda kutoka asilimia 35.5 Oktoba 2007.
 
REDET wanasiasa na mafisadi watupu! Nawajua vigogo wawili wa REDET ambao wamepewa ulaji na mkuu wa nchi; Prof. Mukandala kapewa u VC UDSM na DR. L. Ndumbaro ambaye kateuliwa kama mshauri wa rais wa mambo ya siasa. Besides, REDET has been commissioned several times by CCM to undertake research. What do you expect. Ufisadi is everywhere. CCM out 2010 watake wasitake.
 
REDET wanasiasa na mafisadi watupu! Nawajua vigogo wawili wa REDET ambao wamepewa ulaji na mkuu wa nchi; Prof. Mukandala kapewa u VC UDSM na DR. L. Ndumbaro ambaye kateuliwa kama mshauri wa rais wa mambo ya siasa. Besides, REDET has been commissioned several times by CCM to undertake research. What do you expect. Ufisadi is everywhere. CCM out 2010 watake wasitake.

REDET has

1. A conflict of interest
2. No objectivity
3. no moral authority
 
I see another George Bush in the making. What we need now in Tanzania is a Barack Obama. A man with a vision.
 
I see another George Bush in the making. What we need now in Tanzania is a Barack Obama. A man with a vision.

O'Bummer haja accomplish chochote na wewe...ushabiki wako una cloud kabisa judgement yako na kusahau kuwa huyu jamaa hata siku 100 hajamaliza. Nini alichokifanya mpaka sasa zaidi ya kusoma hotuba kwenye teleprompter?

What we need is a transformational figure like Ronald Reagan.
 
Well, sishangai kitu hapa kwani NDIVYO TULIVYO!..
wakuu zangu inabidi tusome taarifa hii kwa makini sana kwani binafsi naamini kabisa kama kweli utafiti huu ulifanyika wakati vigogo wanakamatwa inawezekana maelezo haya kuwa yana ukweli...

Akitoa taarifa ya utafiti huo jana kwa waandishi wa habari, mtafiti mkuu wa Redet, Dk Benadetha Killian alisema kuwa ukilinganisha takwimu za Oktoba 2006 na Oktoba 2007, asilimia ya wale wahojiwa ambao wanasema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Rais Kikwete imepungua kutoka asilimia 69 Oktoba 2006 hadi asilimia 44 mwezi Oktoba 2007 na sasa imefikia asilimia 39.5 hadi Novemba mwaka jana...
 
Well, sishangai kitu hapa kwani NDIVYO TULIVYO!..
wakuu zangu inabidi tusome taarifa hii kwa makini sana kwani binafsi naamini kabisa kama kweli utafiti huu ulifanyika wakati vigogo wanakamatwa inawezekana maelezo haya kuwa yana ukweli...

Akitoa taarifa ya utafiti huo jana kwa waandishi wa habari, mtafiti mkuu wa Redet, Dk Benadetha Killian alisema kuwa ukilinganisha takwimu za Oktoba 2006 na Oktoba 2007, asilimia ya wale wahojiwa ambao wanasema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Rais Kikwete imepungua kutoka asilimia 69 Oktoba 2006 hadi asilimia 44 mwezi Oktoba 2007 na sasa imefikia asilimia 39.5 hadi Novemba mwaka jana...

kuna watu wanaitwa STEADMAN RESEARCH FOUNDATION ...wapo nchi nyngi ,..hapa pia wapo...huwa wanaendesha kura za maoni kitaalamu na wana uwezo wa kutoa matokeo yanayoreflect ...most recent situation ..kwa mfano hapa wangeweza kutoa reflection ya wananchi hadi kufikia mwisho wa mwezi wa MARCH 2009....

sasa shangaa REDET matokeo ya utafiti wa mwaka jana NOV 2009....wameyakalia hadi leo ndio wanayatoa kwa umma ....walikuwa wana time nini??????....kwenye siasa muda ni jambo la muhimu sana kwenye rating..kuna mambo mengi yametokea kati kati ...yanayoweza kuharibu uhalisia wa matokeo yao.....wao ni wataalamu wa siasa wanajuwa kuwa utafiti wao umeshapitwa na wakati...nadhani wangetoa matokeo as of 31 st march ...hali ingekuwa mbaya zaidi...
 
Polls kama hizi wasiachiwe Redet tu. Ni vigumu kupata picha sahihi. Vyombo vya habari, vyuo vingine, n.k. pia wajitokeze.
 
Phillemon Mikael,
Mkuu nimekusoma.... kweli kabisa hawa jamaa walitakiwa kutoa taarifa hii mapema kwani binafsi nimejiuliza kwanza.. hivi wakati ule kina Jeetu walipokamatwa mimi nilikuwa namtazama vipi JK...kusema kweli nilianza kujenga matumaini na Uongozi wa Kikwete na nikafikira kwamba wakati umefika baada yaa..Na kama ningeulizwa wakati ule ningekuwa ktk kundi la kati..

Lakini hata hivyo mimi naamini kabisa kwamba yawezekana ameshuka hadi asilimi 39.5 kama ilivyo..hakuna cha kati, kwa sababu kama utasoma kwa makini lile neno Wanaoridhika kiasi limeundwa ili kupata sehemu ambazo wananchi hawaridhiki badala ya sehemu ambazo wananchi hao wanaridhika kiasi..
Kifupi, kama utafiti uliopita bado napata matumaini na namba hizi kwa sababu binafsi huenda nje ya box zima la Takwimu kama hizi na kuweka vitu kama Ushabiki, Udini, Ukabila na mengineyo mengi ambayo yanampa kura hata kama anaharibu.

Mkuu wangu, sisi Ndivyo Tulivyo - Tusisahau tu kuwa hata huyo Mugabe ana washabiki kibao pamoja na madudu yake yote, hadi hivi tunavyozungumza mzee ni rais wa Zimbabwe!..Only in Afrika..
Ni lazima tukubali kuwa wapo wajinga kati yetu!
 
Hizi zote ni mbinu za kisanii za kuwavuta wananchi wapigie kura Vasco mwakani, cha kusikitisha ni kuwa lazima atawapata wengi tu,.... Huwa ni mjuvi sana wa kampeni za kisanii huyu.
 
DR Lillian killiAn ...MTAFITI wa REDET Kaja na utafiti wake ..tena ..at this time ,utafiti ni wa mwaka jana november 2008...

HABARI zaidi zitapatikana magazeti ya kesho....

hivi huyu ni Dr. Lillian Killian au Dr. Benadeta Killian? nafikiri mwandishi kakosea. na hivi ni huyu ambaye amapewa ukuu wa School of Journalism and Mass Communication na Mkandala? kwikwikwi kazi ipo anapewa cheo baada ya kufanya kazi nzuri REDET?
huu ni wizi mtuuuupuuuu kwanza ni aibu kwa wasomi, ripoti ya nov 2008 isomwe april mwishoni.
 
Back
Top Bottom