Recruiting Agent wanakera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Recruiting Agent wanakera

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Llio 002, Feb 16, 2017.

 1. Llio 002

  Llio 002 JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 650
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 80
  Habari wana jf, kila ninapoomba nafasi za kazi huwa nina dondokea kwa hawa jamaa recruiting agent.

  Sio siri hawa jamaa wanakera wanakupigiya simu one day before day of usahili kisha wanakwambia usahili ni mapema sana let say saa tatu kwa hiyo kwa mtu kama mimi ninayekaa Mbagara rangi tàtu natakiwa nitoke nyumbani saa moja asubuhi halafu nafika kwenye usaili then unaingia kwenye chumba cha usaili unaulizwa maswali mawili tu ambayo yanatumia kama dakika tano tu kujibu yote baada ya hapo unaambiwa uondoke kisha utapigiwa simu.

  Sasa kama mnajuwa maswali yenyewe ni mawili si nibora tu mkanipigiya simu mkaniuliza nikiwa nipo nyumbani tu kuliko kuja huko nikapoteza nauli yangu pamoja na muda wangu,hii ni kero sio siri.

  Ndugu zangu nawezaje pata kazi ambayo inetangazwa moja kwa moja na kampuni husika?
  Naomba msaada tafadhari asante....
   
 2. M

  MZEE RAZA JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2017
  Joined: Feb 19, 2015
  Messages: 2,032
  Likes Received: 926
  Trophy Points: 280
  Hawakuombagi 20,000 kwa ajili ya kulipia gharama za mchakato wa ajira?
   
 3. OPERATION ENTEBBE

  OPERATION ENTEBBE Senior Member

  #3
  Feb 16, 2017
  Joined: Feb 13, 2017
  Messages: 119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hahaaaa una fani gani?
   
 4. Llio 002

  Llio 002 JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 650
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 80
  Sijawahi kuombwa mkuu,sema siku nikiombwa ndipo watakapolijuwa shetani langu
   
 5. Llio 002

  Llio 002 JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 650
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 80
  Marketing mkuu
   
 6. OPERATION ENTEBBE

  OPERATION ENTEBBE Senior Member

  #6
  Feb 16, 2017
  Joined: Feb 13, 2017
  Messages: 119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Duuuuuuuuuuuuuu kuna Uzi wa marketing una trail humu
   
 7. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2017
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 22,561
  Likes Received: 21,547
  Trophy Points: 280
  Kuokoa yote hayo na kuepuka huo usumbufu JIAJIRI tu tafadhali. Na kujiajiri siyo lazima uwe na Mtaji wa Pesa bali hata tu IQ yako kama ni nzuri ukiitumia vizuri kwa kuja na mipango na mawazo ya Kiufanisi ukimtafuta Mtu mwenye Pesa mnaweza mkaungana na kufanya kitu. Tatizo letu Watanzania tunadhani kujiajiri ni lazima tu uwe na Pesa. Wazo lako zuri la Kibiashara linaweza kukufanya ugombewe na Watu wengi wenye Mitaji Pesa na ambao walikuwa hawajui nini za kuzifanyia. Tujitahidi kufikiri nje ya box otherwise kila siku tutabaki ' kulalama ' tu humu na siyo lazima ukisoma basi uajiriwe Serikalini au katika Sekta binafsi. Asubuhi njema Mkuu.
   
 8. U

  UKAWA2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2017
  Joined: Apr 22, 2014
  Messages: 2,057
  Likes Received: 1,484
  Trophy Points: 280
  Nyie team kujiajiri mngejua mnavyokera,hivi nyie mmejiajiri,mnafahamu mazingira ya kujiajiri yalivyo na changamoto nyingi kwa sasa?,mnajua mtu anapotoka tu chuoni anakuwa katika mazingira gani ya kumwezesha ajiajiri?
   
 9. Biobenga

  Biobenga JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2017
  Joined: Nov 18, 2014
  Messages: 325
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 80
  Mkuu labda nianze kukwambia kuwa interview sio maswali pekee. Wanaweza wakakuangalia jinsi ulivyovyaa, jinsi unavyoongea, na body language.

  Lakini pia inawezekana ulikua umeandaliwa maswali mengi na hayo mawili ukawa umeshindwa kujibu au wakaona hutafaa kwa nafasi hiyo. Kwa hiyo badala ya kuendelea kupoteza muda wakakwambia interview imeisha.

  Mwisho mtafutaji hachoki, bora wewe ambaye unaitwa kwenye interview, hiyo ni hatua nzuri katika kupata ajira. Wapo ambao wanafanya applications nyingi lakini hata nafasi ya interview wanaikosa. Nakushauri endelea kwenda kwenye hizo interview, naamini utafanikiwa.
   
 10. 1562013

  1562013 JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2017
  Joined: Jan 3, 2017
  Messages: 837
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 180
  we ulitaka maswali mangapi?
  hivi serious unataka kazi ww.....uliza wenzio wengine ata kuitwa interview hawaitwi na kuna wengine siku wanaitwa interview inaghairishwa. Kuwa serious
   
Loading...