Salaam, mwezi uliopita nilikuwa na download picha kuingia kwenye laptop yangu. Wakati ina download, nilipata meseji kwamba hard disk imejaa hivyo ni run 'disk clean up'. Nili run hiyo na nikapata saved space karibu nusu ya hard drive. Nilifurahi na kuendelea ku-download picha zangu. Baadae wakati nataka kuendelea na kazi zangu, niligundua ma file yote niliyofanyia kazi mwezi wa kumi pamoja na folders hazipo. Zimepotea. Nimejaribu recovery programmes kama 'Recover my files' na 'Ontrack Crisis Centre'. Imeonyesha kurejesha ma faili mengi tu lakini kazi zangu za mwezi wa kumi bado hazionekani. Naomba msaada.