Nilikuwa naomba kufahamishwa Jambo moja kuhusu recategorization

RUBYA 455

Member
Oct 6, 2016
53
11
Habari za muda huu wadau. Nilikuwa naomba kufahamishwa Jambo moja kuhusu recategorization Kwa mwenye uelewa na haya mambo.

Mimi nimemaliza chuo mwaka Jana 2019 ,na mwaka huu 2020 mwezi February nilituma vyeti vyangu kwa mwajiri na kumuomba kuhusu kufanyiwa recategorization yaani kuhamishiwa kada nyingine.

Je naweza kubadilishwa kada mwaka huu wa fedha 2020/2021 au ni mpaka mwaka ujao wa fedha yaani 2021/2022?......Naomba ufafanuzi Kwa mwenye uelewa. Nawataki jioni njema.
 
Shida ni kuuliza swali lililo very obvious, maana kila taasisi Kuna mfumo wake lakini pia hiyo recategorization inakutoa wapi kwenda wapi. Mwenye kukupa jibu sahihi ni HR wa huko uliko period
 
Na kama unaona huna jibu ungekaa kimya pia. Huo ndiyo ustaarabu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Nenda kaongee vizuri na HR haifanyiki hivihivi hiyo. Lazima kuwe na nafasi kwenye Ikama ya watumishi wa taasisi yako. Taarifa hizo wanazo HR.

Muda huu ni mzuri kuwaona kwani ndio maandalizi ya hiyo Ikama kwa mwaka wa fedha ujao hayako mbali kiserikalini
 
Brother inatakiwa ujue Re categorization haifanyiki kwa sababu ww umemaliza shule la kisubmit vyeti, inafanyika baada ya kuona upungufu wa watu katika kada fulani na kama Ikama ya taasisi yako inaruhusu kuajiri ndio ww uliye ndani utapewa kipaumbele.

Huo ndio utaratibu.

Lakini pia kuna figisu unaweza fanya na maboss wako ukafanikiwa.
 
Inategemeana na gap kwenye ikama ya taasisi yenu. Swali lako lipo very subjective kulingana na taasisi husika.
 
Ok, nami ni mstaarabu kama we we; nilikuwa nakuchalenge tu. Siwezi kukaa kimya nasema kutokana na kuonekana kwako unatoa maneno yenye busara haijalishi umeambiwa vipi.

Ni hivi huwezi kufanyiwa recategorization mwaka 2021/2022 mpaka muda huo watakuwa wameshamaliza ishu hivyo labda wachelee,

Neno recategorization umeshalijibu mwenyewe kwenye maelezo yako labda kama kuna la ziada juu ya hilo.
 
Habari za muda huu wadau. Nilikuwa naomba kufahamishwa Jambo moja kuhusu recategorization Kwa mwenye uelewa na haya mambo.

Mimi nimemaliza chuo mwaka Jana 2019 ,na mwaka huu 2020 mwezi February nilituma vyeti vyangu kwa mwajiri na kumuomba kuhusu kufanyiwa recategorization yaani kuhamishiwa kada nyingine.

Je naweza kubadilishwa kada mwaka huu wa fedha 2020/2021 au ni mpaka mwaka ujao wa fedha yaani 2021/2022?......Naomba ufafanuzi Kwa mwenye uelewa. Nawataki jioni njema.
Kama kuna uhitaji watakufanyia as soon as possible ila pia usiwe na mkono wa birika sio mbaya ukamtoa HR hata ya maji ili akuone maana inawezekana mnaohitaaji mko wengi.
 
Back
Top Bottom