Rebels M23 urge Tanzania to scrap sending UN troops to DRC

Hao m23 wanapiga tu mkwara, wanajua hawana ubavu wa kuigusa tz, labda kama kuna mataifa yanawapa kiburi.
 
wamemuandikia barua kumtaka asipeleke majeshi yake kongo,wakisema akiyapeleka watalipiza kisasi.SOURCE:DDW. mchana huu
Hivi kama tuliweza kupigana na wareno huko Mozambique na nchi nyingine kusini, uwezo huo umekwenda wapi hadi tunatishiwa nyau na magaidi wa M23? Isije kuwa logistically hata hawa M 23 wako well equipped kuliko JWTZ maana leo ufisadi ni kila kona.
 
tanzania ndo nchi ambayo iko mstari wa mbele kupigania ukombozi wa bara la afrika, hatuwezi kuwa huru mpaka afrika yote iwe huru, mwl. Nyerere'

Lakini kwa Mujibu wa Membe ni kwamba Amani ya Tanzania inategemea sana Amani za mataifa jirani ikiwemo Kongo DRC.
 
Lakini kwa Mujibu wa Membe ni kwamba Amani ya Tanzania inategemea sana Amani za mataifa jirani ikiwemo Kongo DRC.

Ni pointi ya msingi lakini,

Mbona amani ya Tanzania serikali haiijali?

Amani za majirani zetu zinapatikana kwa njia ya mizinga tu?

Kama tunajali amani ki hivyo kwa nini wasifanye taratibu za usuluhishi sasa wanakwenda kupigana bila kujua wale watu wanagombania nini?

Kwa nini Kabila ameruhusu hadi waingie kwenye ndu ndu ndu wakati alikuwa na nafasi nzuri ya kulimaliza kwa njia za ki diplomasia?

Serikali ya TZ inapeleka majeshi ili kumpiga nani na kwa kosa gani?

I DONT BELIEVE IN MISSILES AS A SOLUTION FOR PEACE RESTORATION.
 
Nadhani had kurugenzi ya mawasiliano ikulu itakapo thibitisha barua hiyo ndo nitaamini. Binafsi sijasikiliza hiyo habari DW, but hiyo taarifa ilikuwa balanced? Waliuliza ikulu kama kwel wamepokea hiyo barua au ni upande wa m23 ndo wametoa hiyo habari?

But nadhan m23 hawana ubavu wa kututunishia misuli manake kwa jeshi letu kwenda congo ni kwa makubaliano ya umoja wa mataifa so Tanzania imetekeleza agizo la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhakikisha usalama wa congo na nchi jirani.wanapima kujua msimamo wa tz kama ni vigeu geu ama vipi..bt najua mh. Membe ni mtu wa misimamo na hatarud nyuma kwa vitisho hvyo vya m23
 
Watanzania tunayo amani mipakani lakini NDANI ya Nchi ni nafuu wangerudi waingereza watutawale kuliko wananchi kutokua na raha kwenye Nchi yao , eti kisa viongozi (waliowachagua wao) wanawanyanyasa. Kusema la ukweli kwa sasa mimi sina raha na udhalimu unaofanywa waziwazi na hatua zichukuliwazo! ; na uhuru wa mahakama kuamua adhabu stahiki bila kuingiliwa na MA-BOSS kadhaa. najiuliza sana mambo mengi kama ni kweli au la, na hatua zilizochukuliwa mf. EPA, RICHMOND, KAGODA INV., MAPESA YA USWIZI, TWIGA KWENYE NDEGE, LOLIONDO, RADAR, VIJISENT, MBOLEA ZA KILIMOKWANZA ZINAVYOTUMIKA, % ZA MIKATABA YA MIGODI YOOOOOTE, etc. Je,ni kweli yapo yote haya au kwangu mimi hapajakucha bado nipo NDOTONI.,!,! _-_---......!!!!!
 
Nadhani had kurugenzi ya mawasiliano ikulu itakapo thibitisha barua hiyo ndo nitaamini. Binafsi sijasikiliza hiyo habari DW, but hiyo taarifa ilikuwa balanced? Waliuliza ikulu kama kwel wamepokea hiyo barua au ni upande wa m23 ndo wametoa hiyo habari?

But nadhan m23 hawana ubavu wa kututunishia misuli manake kwa jeshi letu kwenda congo ni kwa makubaliano ya umoja wa mataifa so Tanzania imetekeleza agizo la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhakikisha usalama wa congo na nchi jirani.wanapima kujua msimamo wa tz kama ni vigeu geu ama vipi..bt najua mh. Membe ni mtu wa misimamo na hatarud nyuma kwa vitisho hvyo vya m23

Mkuu nimeisikiliza ile taarifa, haijaeleza upande wa pili kuthibitisha kupokea barua hiyo.
 
Je bunge letu limeafiki kupeleka kikosi chetu kupigana huko Congo? Wajue kuwa huko watakuwa wanapigana na jeshi la Kagame na sio hao mnaowaita M23; na jeshi la Rwanda sio la mchezo kwani mtabeba majezeza mpaka mkome!! Hizo fedha za U.N zitawatokea puani!!
 
Wametoa warning kwasababu ndani ya M23 kuna wanajeshi wa jwtz walihasi na kujiunga na kundi la m23.
They real know jwtz in and out.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
alafu sisi tukisikia label tunadhani ni kakundi kadogo tu ka wahuni lakini tusisahau kuwa hako kakundi ndio kameisumbua DRC mpaka jumuiya ya kimataifa kuamua kuingilia kati.
Kwa nchi zenye rasilimali na utajiri kama tz sio vizuri kusikia habari za labels.
Kumbuka mfano mdogo wa Marehemu Gadafi, alijidanganya kuwa ni wahuni lakini hakujua ni nani angeweza kuwa nyuma yao na matokeo yake ikamgharimu. Haya, viongozi endelezezi mipasho kama Mgogoro wa mpaka wa Malawi
 
Huo ndio ukweli. Tuache siasa! Ikiwa kama tumejipima na kuamini ya kwamba tunaweza kuwasaidia Wakongo (DRC), je kwa nini tusifanye hivyo?? Kukosekana kwa amani kanda ya Maziwa Makuu ni hatari kwa usalama wetu, Kenya n.k. Ndio maana, pamoja na sababu nyingine, Kenya ilipeleka jeshi Somalia. Pia ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Milenia, yaani kushirikiana na mataifa mengine katika kuleta maendeleo. Hatuwezi kuishi kama kisiwa. Mungu saidia jitihada zetu zizae matunda.

Unayosema ni sawa lakini unajua kenya walipeleka wanajeshi somalia kwa ajili ya kulinda usalama wao na maslai ya kenya? Wasomali walikuwa wanahujumu mpaka ndani ya kenya, tofauti na cc. Uganda inapakana na sisi kwa upande wa kusini mwa uganda, wale waasi wako kaskazini mwa uganda! Kwann nchi wanazopakana nazo kwa upande wa kule kaskazini zisisaidie wakati sisi wenyewe tunamatatizo kibao yanayozidi yao? Wale m23 ni waasi tu. Sisi hapa kwetu tunao magaidi na wanapata ruzuku ya serikali! Mi naona hizo pesa za kupeleka wanajeshi huko ni bora wangenunulia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha wasambaratishe maandamano ya magaidi.
 
tanzania ndo nchi ambayo iko mstari wa mbele kupigania ukombozi wa bara la afrika, hatuwezi kuwa huru mpaka afrika yote iwe huru, mwl. Nyerere'

Lakini kwa Mujibu wa Membe ni kwamba Amani ya Tanzania inategemea sana Amani za mataifa jirani ikiwemo Kongo DRC.
 
Daaa yani wameaanza kuogopa kabla ya kupigwa! Huo mkwara hausaidii lazima wachapwe!
 
Back
Top Bottom