jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
- Thread starter
- #61
Yaani nyie badala ya kwenda kuomboleza mnaenda kufanya kikao cha chama?Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limekiri kuwafurusha waombolezaji waliokuwa katika msiba eneo la Mabatini, kwa mabomu ya machozi kwa madai ya Chadema kutumia msiba huo kufanya vikao vya siri vya kisiasa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema "Ni kweli tumewafurusha, na tutaendelea kuwafurusha. Hatuwezi kuruhusu misiba kutumika kama kichaka cha kufanyia siasa. Kama watu wanataka kufanya mikutano ya kisiasa wafuate utaratibu. Waje waombe kibali kama wenzao (CCM) na sisi tutaamua either kuwaruhusu au kutowaruhusu, sio kutumia msiba kufanya siasa. Waambieni wakikusanyika tutawafurusha tena. Na sio kwenye msiba tu, hata kwenye harusi, matanga, vikao vya ukoo tukigundua wanafanya siasa tutawafurusha. Hata hivyo this time tumetumia nguvu ndogo sana. Siku nyingine tutatumia nguvu kubwa zaidi."