Maisha halisi ya Burundi

nkobhe255

JF-Expert Member
Sep 26, 2017
234
292
Kwanza kabisa niwape pole kwa mihangaiko yenu ya kila siku wana JF.

Kama heading isemavyo hapo juu, mwezi uliopita/Septemba nilifanya ziara ya kitalii nchini burundi, kwa niliyoyakuta ni balaa tupu, very dangerous. Pia kama kuna Warundi humu basi mje mkanushe au myatolee ufafanuzi haya ninayoenda kuyaongea.

1. Hakuna kuoa zaidi ya mke mmoja, hili lilinishangaza sana ndipo nikaamua kulivalia njuga nikaulizia chanzo. Wenyeji waliniambia eti'' ubhanye abhagore bhenshi nta amatogo yachwiye''

2. Zaidi ya 90% ya wafanyakazi wa serikali ni wa chama tawala, wenyewe wanaita IMIGAMBWE. Kwa huku kwetu TZ, Maadili ya viongozi yanakataza wafanyakazi wa serikali kuwa na milengo ya kisiasa, ila kwa Burundi , Waalimu, madaktari, n.k utawakuta kazini wamevaa t-shirt zenye picha ya Rais na chama chake cha CMDD-FDD

3. Mishahara ya wafanyakazi ni pasua kichwa, ni nusu ya hapa kwetu, ila watu bado hawagomi na wanachapa kazi. Mfano, Mwalimu wa shule za upili/Secondary school ni chini ya laki 3 Tsh

4. Wafanya kazi wa ndani ni shida tupu, wengine wanaita UBHUBHOYI au UBHUYAYA, yaani mtu unalipwa Tsh 4000/month, duuu pathetic.

5. Vijana wenye nguvu hukimbilia Tanzania katika mikoa ya Kigoma na Kagera kutafuta vibarua vya kulima mashamba, na hii ni kama uti wa mgongo wa kilimo cha mkoa wa Kigoma, Warundi ndio hulima mahekta mengi kwa ujira mdogo huku wao wakiona ni hela nyingi. Mfano, mtu unalima Hekari ya mita 100 kwa Tsh laki 1 then unaona hela nyingi, duuu

6. Mademu wa burundi ni pasua kichwa, zaidi ya 80% wanatumia pombe kama kuonesha Ubitoz. Na ukimtaka tu wewe mnunulie pombe basi, wanawaogopa watz eti ni Malaya/Abhagilanyi duuu, ila ukipiga kiswahili kizuri ukaahidi kumuoa basi yuko tayari, lakini hataki muishi Burundi bali Tz.

Ongezeeni na mengine, karibu kwa mjadala basi matusi nooo

nkobhe255
 
Back
Top Bottom