Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Chakustaajabisha ni pale jengo linakaa bure mmiliki hataki kushusha kodi na anaona ni bora likae tupu hata miaka kumi ilipaswa kwa wakati huu sisi wanyonge tukalie haya maghorofa
hiyo mwanamboka plaza kinondoni ground floor, toka ahame NBC BANK mwaka juzi hakuna mpangaji mpya, hapo ni mjini kabisa.
 
Mkuu tulijaribu kufanya hivyo ila wanasema kuwa biashara iko very high na wateja wako wengi sana Ila mpaka leo Nikipita Hapo naona kuna vyumba viwili tu ndo vina watu
Labda vyumba vingine wameyapangisha majini mahaba yanafanyia massage
 
Amepata,,ila cheki hii ingemfaa kama asingepata
Mh Mbezi beach hio ni kodi ya nyumba ya kawaida sana. Nina mtu wangu kahangaika sana kupata angalau two bedroom kwa 350,000/- kakosa kaishia Mbezi upande wa juu.
Screenshot_20210308-172848.jpg
 
Watu humu waongo kishenzi yaani mtu atoe 30m hlf ndio atajiwe kodi kiasi gani yaani hii 30 anaitoajetoaje sijui ni kkoo gani tunayoiongelea humu tuna ndugu na marafiki tunajua kinachoendelea kkoo kwa sasa

Hayo masuala mbona yanawezekana mkuu, na naamini yameshafanyika. Ijapokua sasa hali ya biashara imekua ngumu mno lakini kwa kipindi cha nyuma inawezekana kabisa.
 
Ameuaje? Sema amefanya nini ambacho kikwete hakufanya?

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Vingi tuu ila kikubwa hajui kubalance uchumi wa watu na vitu,hajui kipi ni kipaombele chenye tija ya mda mfupi na Kati au mrefu.

Hawezeshi sekta ya kilimo na ame centralize sekta ya fedha

Mwisho serikali inafanya biashara badala ya kuwezesha sekta binafsi kukua na kyajiri.Ni mengi Sana aliyoharibu kuliko kuboresha.
 
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.

Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.

Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.

Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.

Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.

Je, hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?
Unazungumzia commercial real estate tu au?
 
Mbona sababu ziko wazi? Watu wanauliza as if hawajui mambo yanavyokwenda (Kodi nyingi while purchasing power ya wananchi ni ndogo). Wanauchumi waliokuwa na guts especially wa ulinzani walishauri na kushauri lakini hakuna hatua zilizokuwa zikichukuliwa. Serikali inayojiona imejikamilisha kilakitu ndio serikali idondokayo.
Jiwe kavuruga hadi soko la Mazao ya kilimo but anyway acha wachapwe mitano tena mliwachagua webyewe
 
Ngoja mirad mikubwa ya kukamuana ya kukamuana kodi za kila aina iishe, ndipo hapo mkanda unawezwa kulegezwa kidogo..labda 2030 hivi.
Haitakaa itokee gharama za uendeshaji zitakuwa kubwa hivyo yatakuwa yale yale ikiwemo kulipa madeni

Ndege zmenunuliwa umeona kuna ndege inayoleta faida? Kodi inatumika kuziendesha ndivyo itakagyokuwa
 
Hii sasa ndio kuangalia tatizo nje ya siasa.
Mafundi mchundo (technicians) ndio wamekuwa wataalamu wa land development... Ukitumia urban planning vyema na kila mwaka ukawa unamlipa independent Planner kukifanyia assessment kujua catchment yako kama bado niko intact au imeanza kuwa saturated... Unaweza kupata hata ushauri wa waboresho ya jengo lako kumeet the changing needs au kuobject mabadliko ya matumizi yanaweza kuwa ya athari kwa uwekezaji wako...

Sheria zinatoa options hizo ila hakuna anayefuatilia...wekezaji wetu ni wa majaribio mno.
 
Back
Top Bottom