Re: Ufafanuzi wa pesa zilizoibiwa kifisadi na kazi ambayo ingeweza kufanywa nazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Ufafanuzi wa pesa zilizoibiwa kifisadi na kazi ambayo ingeweza kufanywa nazo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 3, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi wanaishi chini ya kipato cha dola moja.
  Sababu ya kutokushtuka juu ya wizi wa mabilioni ni kwa kuwa unaposema Bilioni EPA 133 au Richmond 155 au Rada kuongezwa Bil 40 hawaelewi. 40 ni ndogo kuliko mia na wao angalao wana 800.

  Ni vizuri wanaofanya kampeni katika awamu hii ya pili , wafafanue kile ambacho kinaweza kufanywa na Bilioni moja. Kwa mfano Bilioni moja ni shs Milioni elfu moja. Milioni 100 ingeweza kujenga sekondari moja ya kawaida. Bilioni moja ingeweza kujenga sekondari kumi.
  Bilioni 133 ingeweza kujenga shule 1333. Kwa maana ya kwamba kila mkoa Tanzania ungeweza kujengewa shule 400 ( Mia nne kwa pesa za EPA peke yake.
  Halafu uje sasa za Meremeta zingeweza kufanya nini?
  Hosptali
  Uje za Richmond zingeweza kufanya nini?
  Barabara
  Uje za Rada zingeweza kufanya nini?
  Zilizokutwa kwenye account ya Chenge Bilioni 25 zingeweza kuwalipa waalimu 4,166 mshahara kwa mwaka mzima huku kila mmoja akilipwa mshahara wa shs 500,000/= ( Laki tano)

  (Na wale wenye mawasiliano na Chama Tawala kinachokuja kuanzia November tafadhali wajulisheni umuhimu wa hili.) Watanzania wengi hawajauona ufisadi kwa sura yake na hawajajua kwa nini watu wanataka kufia madarakani.( Wengine ni Wizi mtupu sio kweli wana shida ya kutaka kuja kuwafaidisha wananchi.)
  TUNAPINGA RUSHWA HATUNA CHUKI NA WATU.
  Mtu akisema anapinga rushwa basi aonekane kuichukia na kuwachukulia hatua wote wanaoua uchumi wa nchi.
  Nampenda raisi wangu Kikwete. Lakini naichukia rushwa na ufisadi anaokataa kuuchukulia hatua. Na kwa masikitiko makubwa ni vigumu kumpa rafiki yangu mpendwa kura yangu.
  Urafiki wetu utaendelea uraiani. Na sina ugomvi na yeye wala uadui.
  Sina ushabiki na vyama vya siasa. Nina ushabiki na hoja. Chadema haiungwi mkono kwa sababu za kidini, kikabila au kirafiki. Nasukumwa na hoja zao. Na sioni ni namna gani nitatumia akili za kawaida kuikubali CCM na marafiki zangu viongozi wenzangu walioko huko.
  Ni muhimu tukamwambia mpendwa wetu ukweli. Wewe Rais ni mzuri wa moyo, una urafiki na upendo na watu wengi ila umesahau ukawa na urafiki hata na mafisadi na hilo limekuweka mahali pabaya.
  TUNAPENDA WATU TUNACHUKIA MAOVU YANAYOWAGHARIMU WANANCHI MABILIONI NA KUWANYIMA MAENDELEO.
  Naipenda CCM lakini kwa suala la ufisadi limezimwa na ni kwa kuwa walikuwa wengi. Uchaguzi huu wao watakuwa chama cha upinzani.
  Watu wengi wanatishwa na watu kumi kupita bila kupingwa. Hicho ni kifo cha demokrasia kwa mtaji wa umaskini wa watanzania.
  Pesa ni nyingi zilizoibiwa na zinazotamaniwa zikaibiwe tena. Baadhi ya waliopita bila kupingwa kupita kwao kunatia mashaka makubwa juu ya namna walivyopita. PESA PESA INAMALIZA NCHI HII.
  Wale waliokuwa wamepita na sasa wakarudishiwa wagombea ulizia kinachoendelea majimboni mwao.

  MENGI NILIYOYASEMA HAPA NIMEPATA KWENYE TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KIONGOZI MMOJA WA DINI HUKO ARUSHA JUU YA TATIZO LA UFISADI. NILIDHANI UFAFANUZI ALIOUTOA UNGEIGWA NA CHAMA TAWALA CHA Novemba. WENYE MAWASILIANO WASISITIZIE WAMALIZIE NA UFAFANUZI WA UFISADI kwani hata wale wanaoipenda CCM hawapendi UFISADI
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Simple mathematics kama izo wengi zinawapiga chenga very alergic to numbers
   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kilimanjaro na Dar es Salaam Inaongoza kwa wingi wa shule huko ziko shule za sekondari 300 tu. Pesa za EPA zingeweza kujenga shule 400 kila mkoa kwa mikoa 30. Bado zingebaki Bilioni 13 ambazo zingetosha kuwalipa waalimu 4000 ( Elfu nne) ambapo kila shule ingepewa waalimu 10 na kwa mwaka wangelipwa shs 270,833/= Kwa mwezi.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina maana shule 400 kila mkoa Tanzania jumla zingejengwa shule 1200 mpya. Hivyo zingekuwa ni shs Bilioni 120 zimetumika. Zile 13 zilizobaki ndizo zingelipa mshahara wa shs karibu laki mbili na themanini kwa mwaka kwa kila mwalimu.
  Bado tuwakumbatie hawa?
  Wana mahesabu karibuni mtoe changamoto kwa haya mahesabu.
   
Loading...