RE: Natafuta rafiki wa kike anayeishi kwa matumaini.

kikilo

Senior Member
Jan 13, 2013
114
70
Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 20, nimeathirika na ninaishi kwa matumani. Bahati mbaya nilizaliwa na hiyo hali kwani mama na baba yangu ndiyo walikuwa wameshadhirika nilipozaliwa. Kwa bahati mbaya wadogo zangu watatu wote (3), na kaka yangu wameshatangulia mbele ya haki na Baba pia ametangulia mbele ya haki mama bado yupo. Nimeamua kutafuta rafiki wa kike kuanzia miaka 18-22 ili kama itawezekana na kulingani na ushauri wa daktari tuweze kutafuta mtoto maana siku hizi mnaweza kumpata mtoto ambaye hajaadhirika ili ukoo wangu usipotee.Maana inaonyesha historia baba yangu ndiyo inaishia hapa. Kama kuna ambaye yupo radhi naomba tuwasiliaane. Kutokana na hii hali yangu sijawahi kufanya mapenzi tangu nizaliwe. ndugu zangu wamenishauri pia kuwa nitafute rafiki wa kike aliyeadhirika na wao watachukua majukumu ya kutusaidia na kutunza mtoto kama mungu atatujalia endapo nitafanikiwa.
Asanteni
Kikilo
 
Usijikatishe tamaa mdogo wangu ati ni lazima kutafuta ambae tayari ameathirika.
Unaweza chagua hata ambae hajaathirika, ili mradi tu muwe mnafanya mapenzi salama.
Na mtapata mtoto ambae ana afya nzuri na hajaathirika.

Nakuombea kwa Allah malengo yako yakamilike.
Ila ukimpata, unialike kwenye kuuchapa mpunga.
 
Asante kwa ushauri. Nitakualikeni.
 
Usijikatishe tamaa mdogo wangu ati ni lazima kutafuta ambae tayari ameathirika.
Unaweza chagua hata ambae hajaathirika, ili mradi tu muwe mnafanya mapenzi salama.
Na mtapata mtoto ambae ana afya nzuri na hajaathirika.

Nakuombea kwa Allah malengo yako yakamilike.
Ila ukimpata, unialike kwenye kuuchapa mpunga.

mimi hapa sijakuelewa vizuri mapenzi salama yakoje na wakati anahitaji kuzaa?
 
Mapenzi salama nipamoja na kufuata njia za kitabibu ili kuepuka kumuathiri kwa ugonjwa mtoto alie tumboni kwa mama, iwe mama nae ni muathirika au la.

Wewe unajua mapenzi salama ni kufanya mapenzi tu?
Kalaghabhao nitonye.
 
Last edited by a moderator:
Pole ndugu lkn usikate tamaa kwani kufa au kuish ni mipango ya Mungu.Endelea na mipango yako kama vile utaishi milele lkn usisahau kufanya ibada!
 
Mapenzi salama nipamoja na kufuata njia za kitabibu ili kuepuka kumuathiri kwa ugonjwa mtoto alie tumboni kwa mama, iwe mama nae ni muathirika au la.

Wewe unajua mapenzi salama ni kufanya mapenzi tu?
Kalaghabhao nitonye.

naomba unitoe matongotongo machoni mwangu, kufanya mapenzi na mtu ambaye hajaathirika na mnapata mtoto bila mama kupata maambukizi
 
Last edited by a moderator:
naomba unitoe matongotongo machoni mwangu, kufanya mapenzi na mtu ambaye hajaathirika na mnapata mtoto bila mama kupata maambukizi

Ndio.
Unaweza kufanya mapenzi na mwanamke ambae ameathirika na mkapata mtoto ambae yuko salama bila kipingamizi.
Ilimradi mmoja wenu asiwe na michubuko kwenye uume au ukeni.

Kama ingekuwa kufanya mapenzi na mtu aliyeathirika ni kupata ugonjwa, nadhani leo hii dunia ingekuwa nusu jangwa haswa kwa wapenda kugegeda.
 
Ushauri wangu ni kuwa usispecify sana kumtafuta aliyeathirika tu mbona hata wazima ni haki yako kuzaa nae (vigezo na masharti kuzingatiwa) tena ukipata mzima ni vizuri zaidi maana inatoa garantee ya kubaki na mtoto wenu pale chochote kile kinachoweza kutokea (japokuwa hakuna formula ya kutangulia)kuliko kutegemea ndugu kumlea mtoto wako.
 
Pole sana kikilo, usijisikie mnyonge na usikate tamaa ya maisha... Amini waweza ishi kama watu wengine wanavyoishi, kutangulia mbele za haki ni mipango ya Mungu waweza ishi miaka mingi kuliko hata huyo unayemtegemea aje akulelee mtoto wako.
Fanya ibada then ufate ushauri wa dactari.!

Kila lakheli katika katika kufanikisha malengo yako!!!
 
Dah, kuna watoto wadogo lakini mnakuwa wajasiri na mna busara
Kuweka hali yako ya kiafya wazi kabla ya kuingia kwenye mahusiano ni ushujaa
Mwenyezi Mungu akujaalie haja ya moyo wako.

Nakubaliana na wewe Kongosho, ni jasiri huyu na anastahili pongezi. Pia tunamuombea Mungu amjalie kulingana na mahitaji ya moyo wake na uaminifu wake anaouonyesha kwa binadamu wenzake.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 20, nimeathirika na ninaishi kwa matumani. Bahati mbaya nilizaliwa na hiyo hali kwani mama na baba yangu ndiyo walikuwa wameshadhirika nilipozaliwa. Kwa bahati mbaya wadogo zangu watatu wote (3), na kaka yangu wameshatangulia mbele ya haki na Baba pia ametangulia mbele ya haki mama bado yupo. Nimeamua kutafuta rafiki wa kike kuanzia miaka 18-22 ili kama itawezekana na kulingani na ushauri wa daktari tuweze kutafuta mtoto maana siku hizi mnaweza kumpata mtoto ambaye hajaadhirika ili ukoo wangu usipotee.Maana inaonyesha historia baba yangu ndiyo inaishia hapa. Kama kuna ambaye yupo radhi naomba tuwasiliaane. Kutokana na hii hali yangu sijawahi kufanya mapenzi tangu nizaliwe. ndugu zangu wamenishauri pia kuwa nitafute rafiki wa kike aliyeadhirika na wao watachukua majukumu ya kutusaidia na kutunza mtoto kama mungu atatujalia endapo nitafanikiwa.
Asanteni
Kikilo

Pole sana, na hongera kwa kuikubali hali uliyonayo. Nimefarijika sana kwa namna ulivyoichukulia hali yako in a very positive way, na kuamua kuacha nia mbaya walizonazo baadhi ya watu ambao huamua kuambikiza wengine kwa makusudi. Tungelikuwa na watu wenye fikra na busara namna hii, dunia ingekuwa mahali salama kabisa. Mungu akuzidishie baraka zake na kukufanikisha kwenye azma yako.

Best of luck,
HP
 
Mapenzi salama nipamoja na kufuata njia za kitabibu ili kuepuka kumuathiri kwa ugonjwa mtoto alie tumboni kwa mama, iwe mama nae ni muathirika au la.

Wewe unajua mapenzi salama ni kufanya mapenzi tu?
Kalaghabhao nitonye.

Asante kwa kumuelewasha hilo ...
 
Mungu atakupa hitaji la moyo wako pamoja na afya nzuri, kama wadau walivyosema waweza pata hata binti ambaye hajapata maambukizi (kuishi kwa matumaini, kila binadamu anaishi kwa matumaini) na kupata ushauri wa daktari mkapata kinga au hata chanjo ambazo ziko kwenye majaribio sasa hivi.
 
Back
Top Bottom