- Thread starter
- #21
Nashukuruni sana kwa kunitia moyo. Mimi najiona mzima kabisa pamoja na kwamba nimeathirika. Nitakuwa na dhambi isiyosameheka kama sitakuwa mkweli kwa hali yangu kwa ninayetarajia kumpata nikidanganya hali yangu. Maana ukidanganya kama binadamu asili yetu ni kurudi vumbini na kama mungu akipenda atatujalia neema yake ya ahera. NAOMBENI KAMA MNAYAFAHAMU MASHIRIKA YANAYOTOA USHAURI WA UHAKIKA MNISAIDIE MAWASILIANO YAO. Shida waafrika tunajificha kuelezea hali zetu. Mama yangu ameishi na virusi kwa takriban miaka 30 sasa na hana hata dalili ya kudhoofu afya yake. Asante.