Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 20, nimeathirika na ninaishi kwa matumani. Bahati mbaya nilizaliwa na hiyo hali kwani mama na baba yangu ndiyo walikuwa wameshadhirika nilipozaliwa. Kwa bahati mbaya wadogo zangu watatu wote (3), na kaka yangu wameshatangulia mbele ya haki na Baba pia ametangulia mbele ya haki mama bado yupo. Nimeamua kutafuta rafiki wa kike kuanzia miaka 18-22 ili kama itawezekana na kulingani na ushauri wa daktari tuweze kutafuta mtoto maana siku hizi mnaweza kumpata mtoto ambaye hajaadhirika ili ukoo wangu usipotee.Maana inaonyesha historia baba yangu ndiyo inaishia hapa. Kama kuna ambaye yupo radhi naomba tuwasiliaane. Kutokana na hii hali yangu sijawahi kufanya mapenzi tangu nizaliwe. ndugu zangu wamenishauri pia kuwa nitafute rafiki wa kike aliyeadhirika na wao watachukua majukumu ya kutusaidia na kutunza mtoto kama mungu atatujalia endapo nitafanikiwa.
Asanteni
Kikilo
Asanteni
Kikilo