Re:mambo ya kutafakari kabla ya kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re:mambo ya kutafakari kabla ya kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by herbsman, Jan 5, 2012.

 1. herbsman

  herbsman Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mambo ya kutafakari kabla ya kufanya
  uamuzi wa kuoa au kuolewa
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tazama vitu vitatu....Kabla hujaamua kuoa.

  1-Tabia.

  2-Uzuri.

  3. Kama kuna pesa pesa huko...Mana kama family yao ina pesa zinasaidia saidia mshikaji.
   
 3. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,639
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  1.Uzuri
  2.uchamungu
  3.Tabia
  4.nasaba (koo yake)
   
 4. herbsman

  herbsman Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jambo la kwanza
  Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano
  wako na wazazi wako.
  Mwanzo.2:24 anasema, "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja". Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, "Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie".
  Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako.
  Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo - ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako kama umeoa, na ni mume wako kama umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako.
  Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa. Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema, "Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie".
  Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia, "your priorities must change" lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao.
  Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu. Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.
  Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana.
  Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani. Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata kama atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni, - anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; kwa nini? Kwa sababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake.
  Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi. Unaweza sasa ukaelewa kwa nini watu wengine ikifika siku ile ya "send off", yaani ya kum'send' msichana ‘off' asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwa sababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine.
  Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.
   
 5. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwa wale walioko kweny ndoa na wanaotarajia kuoa na kuolewa naomben mkatafute kitabu kiitwacho GOD'S MASTER PLAN FOR MARRIAGE by STEPHEN&GEORGINA ADEI. Ni kitabu kizur sna, wameelezea hatua ya kwanza mpaka mwisho kuhusu maisha ya ndoa! Au kwa wale waliopo Arsh, ntafuteni kwa sm yangu 0658 950 264, nitapawatia copy yake bure! Npo chuo kikuu cha Tumaini, Makumira.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...jiulize; hauwezi kuishi bila yeye?
   
Loading...