Re:m4c ihamasishe maendeleo kwa staili ya umoja ni nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re:m4c ihamasishe maendeleo kwa staili ya umoja ni nguvu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 28, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Vuguvugu la mabadiliko limeshika kasi kila kona ya nchi,Linalopangwa na Mungu hakuna wa kuweza kulizuia ndiyo maana zile juhudi za kukwamisha mikutano ya utambuzi wa kifikra inayofanywa na polisi inazidi kugonga mwamba.Hii inaashiria kilichopo kwa sasa ni suala la wakati na wakati wenye umefika kwa wananchi kujitambua na kukubali kuzipokea harakati hizi za kukipumzisha chama tawala.

  Harakati hizi kuelekea uchaguzi wa 2015 ni harakati za kujikomboa dhidi ya dola chovu iliyoshindwa kutekeleza yale yote waliyo waaminisha wananchi kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.Kauli mbiu hizi zilizoshindwa kufikia malengo zimekuwa chachu ya kuleta mabadiliko makubwa kwa kukipa likizo CCM isiyo na malipo.

  Yanayojiri leo hii ni ukataji tamaa kwa wananchi na kuongezeka pengo kubwa la masikini na matajiri.Umasikini unazidi kuongezeka siku hadi siku hali inayopelekea Mtanzania kuishi chini ya dola moja ya Kimarekani.Shughuli za kiuchumi kwa kila mmoja zimeshuka kwa wanyonge kukandamizwa na matajiri kubebwa kutokana na misamaha mikubwa ya kodi inayowanufaisha matajiri na kuwaacha wanyoge wakizidi kutaabika.

  CDM inaonekana ndio tumaini na pambazuko jipya la kumkomboa huyu mwananchi wa kawaida.Fursa hii mliyoipata kama chama mbadala cha kuwatetea wanyonge itumike vizuri na kuleta tija kwa wananchi.Mikutano inayofanyika itumike pia kama taasisi ya kuwaelimisha wananchi juu ya kujikomboa kiuchumi ili kuondokana na umasikini uliowagubika.

  Ndani ya CDM kuna wataalamu wa uchumi,watumiwe vizuri ili ule ukombozi wa kweli uonekane kwa kutoa mafundisho kwenye mikutano ya hadhara nini tunapaswa kufanya kuepuka umasikini huu.Tunajua kuandaa mikutano ni gharama lakini M4C inachangiwa zaidi na wananchi,basi pia gharama hizo zitumike pia kuhamasisha mapinduzi ya uchumi.

  Malengo ya CDM ni kuhakikisha kuchukua dola ili iweze kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi na kuweza kumwinua mnyonge kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine na kwakuwa hii ndiyo nia yao hasa, basi waitumie vizuri kivitendo ili imani yetu juu yao izidi kujikita zaidi ndani ya mioyo yetu.Kosa moja walilofanya CCM,iwe mtaji wa magoli mengi kwa CDM.Mimi nimeona hili la elimu ya kujikomboa kiuchumi wengine mnakaribishwa kutoa mawazo mbadala itayoisadia CDM kumkomboa mwananchi wa nchi hii na kujipambanua wao na CCM wana mitizamo tofauti.
  Sababu tunayo,uwezo na nia tunao,na kama suala ni wakati,wakati ndiyo huu.
   
Loading...