Re: Kwa kauli hii ya mhe mkono, madiwani waandamane kudai kapunjo ya posho zao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Kwa kauli hii ya mhe mkono, madiwani waandamane kudai kapunjo ya posho zao!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by buyegiboseba, Jun 23, 2011.

 1. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana katika mjadala wa muswaada wa sheria iliyopata vuta nikuvute ya aina yake,mh Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini na mwanasheria wa siku nyingi alisimama na kusema kuwa madiwani wanapata posho sawa na wabunge, wakati akijibu hoja ya Lisu kuhusu kufuta kodi za posho zinazozidi laki moja.Kama ndivyo madiwani watakuwa wanapunjwa sana manake kama wanalipwa sawa na wabunge basi tungeona hata na bajaji.Katika hali halisi ya madiwani tulionao,kuwaambia kuwa wanalipwa sawa na wabunge ni kuwakejeli,madiwani ambao hawana posho ya nyumba,honorarium,special duty,overtime na nyingine zitolewazo kimya kimya kwa wabunge.Nionavyo mimi,mh Mkono alitaka kupata sympathy kwa madiwani kwamba anawatetea ili posho zao zisikatwe kodi wakati katika uhalisia posho za madiwani hazifiki laki moja kwa siku.Nilitegemea mtu mahiri katika sheria kama mh Mkono angekuwa mstari wa mbele kuunga mkono hoja ya kuwepo kodi katika posho kubwa kubwa ili kuleta uwiano usio wa mbali sana kati ya wenye vipato vikubwa na vidogo mfano.
  Yangu nin hayo. I remain open for inputs and corrections
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  usije ukadhani wabunge wa ccm ni mbumbumbu, ila wanajuwa wanachokifanya. Kwa taarifa yako wabunge wa ccm asubuhi akili zao huzifungia kabatini katika mahotel waliofikia na kwenye ukumbi wa bunge huenda wao na mafuvu empty basi, hao ndio ccm bana.
   
Loading...