Re: Kuna kila dalili kwamba, matokeo ya uchaguzi 2015, raisi wa sasa aweza kukabidhi nchi CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Kuna kila dalili kwamba, matokeo ya uchaguzi 2015, raisi wa sasa aweza kukabidhi nchi CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by skalulu, Sep 12, 2012.

 1. s

  skalulu Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wana Jf, mwenendo wa kisiasa hapa nchini inajionyesha kabisa kwamba CHADEMA ni chama ambacho kitapata ushindi kwa asilimia kubwa. Japo kuwa wana CCM mta criticise lakini huu ndiyo mtizamo wa watu wengi sana kwa sasa ambao unapelekea kuwa kweli. Tizama tu mikutano ya CCM na CHADEMA, na ukisikia watu wengi wanavyoongea mitaani na vijijini ni kwamba Chama tawala kimezidiwa nguvu. Watu wengi wana jiuliza, je Chama tawala kitaweza kweli kukubali matokeo?, maana inavyoelekea watu wengi sana watakuwa wamepata mwenendo wa matokeo ya vituo vyote kupitia ripoti za mawakala wa vituo, na yatakuwa yanawekwa kwenye mitandao kila sekunde, kila dakika na hivyo kuona wazi kabisa chama kipi kinaongoza. Nahisi kutokea kama Zambia japo kuwa nchi haina watu wengi lakini waliyajuwa matokeo mapema mno ndani ya usiku huohuo na watu wakaingia mitaani kushangilia, vivyo hivyo hata sisi hapa Tanzania chaweza kutokea. Nahisi itakuwa vigumu kwa CCM kuamini kwamba kweli kimeshindwa, je kama hawataweza kuamini kitakachotokea, wana Jf itakuwaje, hebu tujaribu kupiga picha, mgombea wa Uraisi kutoka CCM ameshindwa, haiwezi kuwa kama ilivyotokea Kenya 2007 Kivuitu kutangaza Kibaki kashinda, na kuapishwa haraka haraka, au kama kule Ivory coast mpinzani aliyeshinda akakaa hoteli kwa ulinzi wa majeshi ya kimataifa huku Bagbo akidai mshindi na kuuda serikali. Na je vipi upande wa vyombo vyetu vya dola jeshi na polisi itakuwaje au wanaweza kupokea vipi matokeo hayo na kitu gani au hatua gani zinaweza kufuatwa. I have a dream: CHADEMA will win the 2015 election. Sure! this dream will come true. hofu ni kwamba upande mwingine i.e CCM na serikali kipindi hicho kabla ya kuapishwa itakuwaje?. sijui siku ya kuapishwa itakuwaje kwa hamasa ya watu na PEOPLES POWER!.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hizi ndoto cha mchana huwa na mathara yake baadaye kwa anayeota. CHADEMA wachukue nchi kwa kigezo gani, Maandamano, Vurugu , Majungu, uchu wa madaraka. Ikitokea mimi nahamia Kenya kuliko kuwa chini ya utawala wa kimafya, kwetu ni karibu sana na kwa ODINGA.
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Ndoto njema sana!
   
 4. H

  Hiraay Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM kwa hakika watashinda na hili CCM inajua, hawana namna kwa umakini wa CDM kura zitalindwa kama ilivyofanyika Arumeru mashariki. CCM (makundi) ijitayarishe kuwa chama cha upinzani
   
 5. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  [QUOTE=skalulu

  hata mimi niliona CDM inayo nafasi kubwa ya kushinda lakini wasiwasi ni hii singo ya udini inaopandikizwa kwa kasi inaweza kugawa kura japo imani badi ipo kwani dini ya watanzania kwa sasa pingamizi dhidi ya dhuluma na maisha magumu na kutaka mabadiliko.
   
 6. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwanafunzi akiwa hana kitu kichwani halafu ikitokea akabahatisha akapata 23 kwenye mtihani basi atajiona ana akili sana kumbe maskini ya mungu 23 nayo ni F
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kweli CDM inaweza kushinda tena kwa kishindo 2015, tatizo nilionalo ni tishio la Tendwa kukifuta chama hicho kabla ya 2015. Take it from me Tendwa ni mtu hatari sana.
   
 8. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  alinacha ati kupata 23 kati ya 200 na kadhaa. Ndo uchukue nch huku wao wamekutazama tu
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,072
  Likes Received: 10,426
  Trophy Points: 280
  Hebu edit kwanza ulichoandika...
  Umeandika kama umetoka kuharisha..
   
 10. n

  nyangwe Senior Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HAKIKA CDM itashinda ila wasi wasi wangu mkuu ni kuwa vyombo vya usalama vitatumika kupoka ushindi wa cdm, na hasa polisi, lenye watu kama chagonja, IGP mwema, pia JWTZ lenye watu kama shimbo nakadhalika.
   
 11. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,072
  Likes Received: 10,426
  Trophy Points: 280
  Huo ni ukweli usiopingika CDM 2015 tutaongoza nchi, tutakuwa tupo Kanani ya ahadi, tutafurahi sana.

  Mungu tuweke hai tuione Kanani ya Tanzania.
   
 12. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hamia sasa maana ukweli ndo huo. ukichelewa utaliwa maso bure
   
 13. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bora uhamie Kenya mapema, maana CHADEMA ikishachukua madaraka tu,wewe na mafisadi wenzako mtajua kumbe jela ipo kwa watu wote na si masikini tu!
   
 14. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  kama kawaida na "mathara" yako na "kimafya"
   
 15. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,795
  Likes Received: 2,569
  Trophy Points: 280
  Muungano wa upinzani tu ndio utangusha CCM. KANU ilipete muda mrefu hadi hapo upinzani uliungana na kutosa chama tawala porini.
   
 16. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  kama ulivyowahi kuandika Said Mwema ni "undergraduate" wa UDSM
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  A day dreamer.
   
 18. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sijaona uwanja unaotosha kumwapishia Rais wa CHADEMA 2015! It will be historical, itakuwa ni kuzaliwa upya kwa Tanzania!
   
 19. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Neno 'mathara' ni lahaja ya Kiswahili au kilugha?
   
 20. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Na utahama na akili zako mgando hizo.
   
Loading...