Re:demokrasia ia maana pana zaidi ya dhamira ya waitumiayo kufanikisha malengo yao

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,545
934
Watanzania kuna hitajika akili kubwa ya kutafakari kila jambo na kutuliza akili yetu kuchuja kila jambo,uwanja wa demokrasia ndani ya Nyanja za siasa nchini mwetu zimegubikwa na changamoto kubwa sana ambazo zimejikita kihasara na kifaida. Kifaida ni pale demokrasia hiyo ambayo ni maamuzi ya wengi kukubalika kwa maslahi ya taifa na mchango wa mawazo kukubalika na wengi ili kukidhi matakwa yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuheshimmu mawazo na hoja za wachache kama changamoto za kufikia demokrasia pevu. Kihasara ni demokrasia kutumika vibaya kwa malengo ya mtu mmoja kuwa na malengo binafsi katika kufanikisha matakwa Fulani yaliyojificha ndani ya dhamira ya mtu huyo kwa kutaka kutumia huruma ya walio wengi kama uungwaji mkono wa mawazo yake bila jamii hiyo kugundua dhamira kusudiwa ya mlengwa. Tukiacha dhana ya demokrasia kama njia ya kufanikisha malengo Fulani ni lazima tujiulize kwanza kwa kupima hasara na faida ya dhamira zetu katika kuitumia demokrasia ya uhuru wa mawazo,ikiwa hasara ni kubwa kuliko faida ni bora kutafuta njia nyumbulika ambayo inaweza kuwa mbadala na yenye maslahi makubwa ndani yake kwa faida ya wote na taifa kwa ujumla wake. Kuhujumiana,kuaminiana na kukubaliana ni misingi ambayo binadamu tumejiwekea katika maisha yetu ya kila siku katika kufikia malengo muafaka katika jamii zetu,lakini unapotekeleza majukumu yako ya kila siku ni lazima utafakari kwa kina,ikiwezekana kwa kuwashirikisha wale walengwa ambao ndiyo wengi kwa kuwaonyesha mtazamo chanya kutokana na dhana unayotaka kuifanya.Jamii husika ikikubaliana nawe kwa hoja zako za uwazi na ukweli dhana halisi ya kuaminiana hujengeka na kuonyesha taswira yenye mwanga wa mafanikio. Ukifanya kinyume na matakwa ya wengi na ikajulikana kabla ya jamii husika kuhusishwa ndipo mashaka ya dhana yako inapoonekana ina uwalakini,ikishindikana kueleweka kwa urahisi huzua hofu na mashaka kwa jamii hiyo huenda ikawa dhana yako uliyoifanya ina zaidi ya usiri uliogundulika. Cha msingi ili kuwa na jamii yenye kukubaliana na kuheshimiana bila kutoaminiana ni wakati sasa wa kujenga mawazo yetu kwa uwazi ndani ya jamii yetu kwa uzito wa hoja kwa kuwashirikisha wadau ili waweze kusikia hoja zako na wao wapate fursa ya kuchanganua hoja zako na kutafakari kwa kina kutokana na mchango wa nguvu ya hoja uliyoiwakilisha kwa wadau hao ambao ndiyo wahusika wakuu ndani ya jamii hiyo ili kuweza kueleweka na kukubalika.Mawazo ya wengi na uzito wa hoja yako ikikubalika yaweza kuleta mtazamo wenye kujenga zaidi katika kudumisha mshikamano na umoja ndani ya jamii yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom