RCs, DCs, DEDs, Madiwani na WEOs wote huishi maeneo yao ya kazi. Kwanini Wabunge hawapendi kuishi na wanajamii wanaowawakilisha?

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
695
935
Katika utafiti wangu usio rasmi nimegundua asilimia zaidi ya 90 ya wabunge wa nchi hii wanaishi nje ya maeneo Yao ya uwakilishi, na wengi urudi majimboni Kwa muda wakati wa uchaguzi.

Mimi naamini Kwa kuwa mbali wanashindwa kutimiza wajibu wao kama vile kuhamasisha shughuli za maendeleo ktk maeneo Yao, lakini pia wanashindwa kufamiliarize na changamoto za jamii zao hivyo kushindwa kuzibeba na kuziwakilisha vyema katika Bunge la Taifa ili serikali izitafutie ufumbuzi.

Nashauri vyama vya Siasa ambavyo ndivyo udhamini wagombea nafasi hizo, watoe vipaumbele kwa wagombea ambao makazi yao ya kudumu ni katika jamii husika/ au iwepo kanuni ya kumlazimisha wabunge kuishi ktk maeneo yao kama wafanyavyo ma RCs na DCs (kama wanabanwa na kanuni kuhudhuria vikao vya Bunge pia wabanwe kufanya KAZI katika maeneo yao ili uwakilishi wao upate mantiki).

Alternatively, wananchi tufanye kuchagua wawakilishi kutoka miongoni mwetu na tuwaache wale wenye shughuli zao nyingine katika miji waendelee huko ili Ile mantiki ya uwakilishi ilete tija (imagine mbunge wako anaishi Dar na wewe uko Ujiji na yeye hutokea Dar kwenda Dodoma kukuwakilisha na bila aibu Haji jimboni kwako kupata maoni mawili au matatu?). Wabunge wa aina hii lazima wakuwakilishe kinadharia na si kihalisia.
 
Mkuu umejenga hoja na kuuliza swali,sasa mbona unajibu mwenyewe?
Ungeliacha kwanza wadau watiririke,then uwe unajaziajazia mtizamo/mapendekezo yako.
Anyway mchango mzuri.
 
safari hii tunataka mbunge anae ishi jimboni.wanatelekeza majimbo kweli. Muda wa uchaguzi wanaibuka. Wamulize mbunge wa Makete mheshimiwa king Norman sigala. Kila kijjiji alichopita juzi kati swali lilikuwa ulikuwa wapi!?
 
safari hii tunataka mbunge anae ishi jimboni.wanatelekeza majimbo kweli. Muda wa uchaguzi wanaibuka. Wamulize mbunge wa Makete mheshimiwa king Norman sigala. Kila kijjiji alichopita juzi kati swali lilikuwa ulikuwa wapi!?
Unatania aisee; baada ya uchaguzi anaondoka utamfukuza?
 
Back
Top Bottom