RC wa Dar ' Comrade ' wangu Amos Makalla jiangalie sana Suala la ' Wamachinga ' linaenda ' Kukufyeka ' usipoachana nalo

Wakuu wa mikoa wenye kufuata taratibu za miji na sio matamko wala hawatasumbuliwa na tumbua tumbua sababu kwa hakika hao machinga hawakutakiwa kuwepo hapo mahali.
 
CCM haikubaliki, kwa hiyo njia pekee kubwa iliiyobaki ni kuwakumbatia machinga, mama ntilie na bodaboda wote nchi nzima. Sasa kama wewe ni mtumishi wa umma na unaona kazi imekuchosha basi wewe fanya jambo la kuyaudhi makundi haya.

Kwa sababu ya hii siasa tusipokuwa makini basi machinga anaweza kuja kupanga nguo getini kwako as long as gate linatazama barabarani na kuanza biashara zake, sasa mguse uone moto utakaoupata.

Pamoja na kushangilia kufukuzwa kwa Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wake ila tukubali tu kwamba tuna tatizo kubwa kuwahusu hawa wamachinga, mama ntilie na bodaboda.
 
Kusema kweli wamachinga wamechafua Sana hili Jiji kila mahali moto barabarani mpaka majiko ya gesi kwenye vituo vya daladala wanachukua bidhaa kwenye maduka makubwa wanauza bila risiti wanauza bia huko barabarani kumekuwa na groceries na nusu bar sasa hao wanaolipa kodi WATAUZA NINI
 
Kwani kumbe ccm huwa wanategemea sanduku la kura ili kushinda uchaguzi?
Na mimi ndio nilikuwa nafikiria hivi kweli kura ndio zinamuweka MTU pale kwenye kile KITI !! CCM inawajua WATANZANIA kuliko raia wenyewe wanavyo jifahamu.

Hao machinga wanaweza tolewa na CCM ikashinda kwa kishindo uchaguzi MKUU.
kwanza asilimia kubwa ya vijana huwa hawapigi kura kabisa .
 
Na mimi ndio nilikuwa nafikiria hivi kweli kura ndio zinamuweka MTU pale kwenye kile KITI !! CCM inawajua WATANZANIA kuliko raia wenyewe wanavyo jifahamu.

Hao machinga wanaweza tolewa na CCM ikashinda kwa kishindo uchaguzi MKUU.
kwanza asilimia kubwa ya vijana huwa hawapigi kura kabisa .
Sema ndio hutumika kuhalalisha.
 
Ninkweli mama amewekeza vijana na wanawake zaidi na wazee....ili apate alope
Wapiga Kura wa siku ni wasomi na wanaopenda vitu viwe kwa level za kimataaifa Ila mtu anayepanga bidhaa hovyo hovyo hawezi kuwa hata na kitambulisho cha Kura pia ni mtu wa kuhamahama sehemu aliyojiandikishia Ila kwenye ushabiki kama kwenye mikutano kwaajili ya kushabikia hakosekani hivyo Kama ni swala la Kura hizo Kura zipo kwa makundi ya wanaojielewa endapo wakikuelewa na sera zako zikiwalenga.
 
Back
Top Bottom