RC: Tamisemi, CAG wanachochea mgogoro ya kiutendaji Bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC: Tamisemi, CAG wanachochea mgogoro ya kiutendaji Bagamoyo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKUU wa Mkoa wa Pwani, Amina Saidi, amesema mgogoro wa kiutendaji unaoendelea kufukuta katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo umechochewa zaidi na baadhi ya viongozi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa katika halmashauri za mkoa huo, mkuu huyo wa mkoa alisema mwanzoni mwa mwaka jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Rhoda Nsemwa, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

  Alisema kwa sasa wanashindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa kutokana na kuitwa ‘viherehere’ wa kufuatilia mambo ambayo tayari yameshakaguliwa na CAG, hivyo hawana nafasi ya kushughulikia tena.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa kuwa kamati hiyo imetembealea wilaya hiyo na kushuhudia aibu iliyopo nao wachukue nafasi kusaidia kushughulikia suala hilo, ili kuwezesha kila mmoja kufanya kazi kwa uhuru.

  “Ninachowaomba kwa kuwa nanyi mmeshuhudia muingilie kati kutusaidia sisi tumefikia hatua ya kuitwa viherehere wakati tunafuatilia fedha za miradi kujua zimetumikaje tunaambiwa kwa kuwa tayari CAG wameshakagua sisi hatuna nafasi ya kuhoji tena,” alisema.

  Alisema kuwa yeye anatambua kuwa Halmashauri ya Bagamoyo ina mapungufu mengi hususan katika upande wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndio maana anafanya jitihada za kuhakikisha hali hiyo inakomeshwa lakini kinachoshangaza kuona ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG )akiendelea kutoa hati safi katika halmashauri hiyo.

  Aidha Amina alisema kuwa mara kwa mara amekuwa akipingana na Tamisemi kuhusu taarifa zinazoandaliwa na ofisi yake jambo ambalo alisema kila taarifa aliyoitoa Tamisemi wameikataa hivyo haoni sababu ya kuendelea kushughulikia suala hilo ambalo linamjengea uhasama katika utendaji wake na hivyo ni vema kamati hiyo nayo ikaingilia kati.

  Hata hivyo, alisema anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watendaji ambao tayari walisimamishwa kazi kuendelea kuishi katika nyumba za watumishi huku serikali ikiendelea kulipa gharama kubwa na kumuacha mkurugenzi wa sasa, Samwel Sarianga, kuendelea kupanga na yeye pia akilipiwa fedha ya pango lake hali ambayo inaonyesha wazi matumizi mabaya ya fedha za serikali.

  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Idd Azzan, alisema kamati yake haijafurahishwa na hali iliyopo katika wilaya hiyo hususan katika matumizi ya fedha na pia imebaini mvutano uliopo kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani, ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Tamisemi na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

  Azzan ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha inafuatilia nyaraka zote za halmashauri hiyo ambazo zimedaiwa zimepotea na kama hazijapatikana wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

  Kamati hiyo ilifanya ziara ya siku tano kwa kutembelea halmashauri za wilaya ya Rufiji, Mkuranga, Kisarawe, Bagamoyo na Kibaha Vijijini.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Paka shume hyu ajui anacho kinena!!!
   
 3. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Hapo ndio inakuwa ngumu kuelewa, CAG anatoa hati safiiiii, na mkuu wa mkoa anasema kuna ubadhirifu na ufujaji! Tuelewe nini hapa na tumwamini nani?
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kizungumkuti bagamoyo maana tukijikumbusha kuanzia ishu ya pinda kuwafukuza kazi wafanyakazi akiwepo mkurugenzi then mhasibu na jerry muro maana nae alikua fisadi wa pale then uje ishu kama hizi hapo bagamoyo pana matatizo!
   
 5. T

  Twasila JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Rc kashindwa kazi. Hajui wajibu wake. Pwani imekula kwenu. Anamlilia nani? Wazaramo na wakwere mfuateni rais amfukuze kazi. Rais huyu hatufai na ni mbumbumbu. Karne ya 21 na rc kilaza hivi!!
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Katika kila match lazima kuwe na "winwin", DC+RC wake wanangangania washinde wao wakati wao hawana nyenzo za kukagua utendaji wa halmashauri, wenye nyenzo na wataalam wamesema halmashauri haina dosari wao wanaleta ubabe wao- shame upon them.
   
Loading...