RC Singida amaliza mgogoro wa makao makuu ya wilaya

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
ILONGERO NDIO MAKAO MAKUU YA WILAYA

Serikali ya mkoa wa Singida imetatua mgogoro wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mapema leo katika mji mdogo wa Ilongero mkuu wa mkoa wa Singida Eng. Mathew Mtigumwe amesema kwamba makao makuu ya wilaya yatajengwa katika kijiji cha Ilongero kata ya Ilongero kama ilivyopitishwa na vikao halali vya wilaya na mkoa.

Mgogoro huu ulitokana na uamuzi wa Baraza La madiwani Halmashauri ya wilaya ya Singida wa tarehe 28 /10 /2016 kupitisha azimio la kujenga makao makuu ya wilaya katika kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya katika Mazingira ya ghiliba, rushwa, hujuma na mizengwe kukidhi matakwa ya viongozi wachache

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Singida ameeleza kwamba watu wachache wenye masilahi binafsi hawawezi kubadilisha maamuzi ya wananchi walio wengi na ametoa Agizo kwa viongozi wa Halmashauri waanze kuhamia Ilongero kuanzia Sasa na ametoa muda wa miezi 6 mchakato wa kuhamia Ilongero uwe umekamilika.

Ushindi huu unatokana na Kamati Maalum iliyoundwa kwa niaba ya wananchi wa Singida kaskazini kuandaa pingamizi lenye hoja za msingi kupinga uamuzi wa Baraza La madiwani kupeleka makao makuu ya wilaya katika kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya ambapo Kamati Maalum iliwasilisha pingamizi kwa mkuu wa mkoa Mnamo tarehe 21/11 /2016.
wanaohujumu wananchi wa Singida kaskazini kwa masilahi yao binafsi wanafahamika kwa majina na kwa mbinu zao.

MAJIPU HAYA YATUMBULIWE HARAKA
 
Hao madiwani ni wa CCM? ndio tatizo la fitna mtafitini wa nje kisha mtaanza kufitiniana wenyewe
 
hao wanaofahamika si umtaje HANJE ELIA NA NYALANDU TU??? WALE MAPACHA WATATU????
 
..waliokuwa wakipinga makao makuu yasijengwe kinyamwabo walikuwa wanadai eneo hilo halina huduma muhimu na miundombinu.

..walikuwa wanadai Ilongero pako vizuri zaidi kwamba kuna miundombinu na huduma na hivyo kuwa na sifa ya kuwa makao makuu ya wilaya.

..binafsi sijafika maeneo hayo kwa hiyo sijui nani anasema ukweli.

..lakini kama ningekuwa mdau wa Singida, na kwa kuzingatia hoja za hapo juu, ningependekeza makao makuu yajengwe Kinyamwambo.

..Uamuzi huo ungelazimisha serikali kulijenga eneo hilo liwe na hadhi ya kuwa makao makuu ya wilaya. Hivyo in the end unakuwa na Ilongera na Kinyamwambo, maeneo mawili, yenye huduma na miundombinu mizuri.

Cc Kanyunyu
 
ILONGERO NDIO MAKAO MAKUU YA WILAYA

Serikali ya mkoa wa Singida imetatua mgogoro wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mapema leo katika mji mdogo wa Ilongero mkuu wa mkoa wa Singida Eng. Mathew Mtigumwe amesema kwamba makao makuu ya wilaya yatajengwa katika kijiji cha Ilongero kata ya Ilongero kama ilivyopitishwa na vikao halali vya wilaya na mkoa.

Mgogoro huu ulitokana na uamuzi wa Baraza La madiwani Halmashauri ya wilaya ya Singida wa tarehe 28 /10 /2016 kupitisha azimio la kujenga makao makuu ya wilaya katika kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya katika Mazingira ya ghiliba, rushwa, hujuma na mizengwe kukidhi matakwa ya viongozi wachache

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Singida ameeleza kwamba watu wachache wenye masilahi binafsi hawawezi kubadilisha maamuzi ya wananchi walio wengi na ametoa Agizo kwa viongozi wa Halmashauri waanze kuhamia Ilongero kuanzia Sasa na ametoa muda wa miezi 6 mchakato wa kuhamia Ilongero uwe umekamilika.

Ushindi huu unatokana na Kamati Maalum iliyoundwa kwa niaba ya wananchi wa Singida kaskazini kuandaa pingamizi lenye hoja za msingi kupinga uamuzi wa Baraza La madiwani kupeleka makao makuu ya wilaya katika kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya ambapo Kamati Maalum iliwasilisha pingamizi kwa mkuu wa mkoa Mnamo tarehe 21/11 /2016.
wanaohujumu wananchi wa Singida kaskazini kwa masilahi yao binafsi wanafahamika kwa majina na kwa mbinu zao.

MAJIPU HAYA YATUMBULIWE HARAKA
Maskini NYARANDU pole yake
 
Pasco uko wapi? Shemeji Yako Lazaro Nyalandu ameumbuka kule Singida kaskazini, Mbunge anaposhiriki kuhujumu wananchi wake ni jambo la ajabu Sana, Amepewa ubunge kwa miaka 20 mfululizo anawapa shukrani wapiga kura wake kwa Mateke ya punda.
 
Mnyampaa Nyalandu kabwagwa chaaali & kwishney, kihisturia mchezo kama huo mwenzie Chenge aliweza kule Bariadi/Simiyu kwa kutumia uwezo wa kifedha na sheria, sio kuleta ujanjajanja wa awamu ya nne
 
Back
Top Bottom