RC Ruvuma awageukia madiwani na watendaji walio sababisha manispaa ya Songea kupata hati isiyoridhisha

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christin geta Mndeme ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi au madiwani waliosababisha hati ya mashaka katika manispaa hiyo .

Hatua hiyo imekuja kufuatia mkaguzi wa hesabu za Serikali(CAG) kubaini baadhi ya hoja kushindwa kujibiwa ikiwemo ya upotevu wa fedha wa sh.Milioni 98 katika mwaka wa fedha 2018 na 2019.
Mndeme ametoa maagizo hayo jana kwenye kikao cha baraza la Madiwani la Manispaa hiyo ambalo lilikuwa rasmi kwaajili ya kupokea maelekezo ya mkuu huyo kufuatia upataji wa hati hiyo na namna ya kujipanga ili isijirudie tena.

Kufuatia hali hiyo mkuu huyo ameutaka uongozi wa Halmashauri kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote waliosababisha upataji wa hati hiyo bila kujali vyeo vyao au nyazifa zao ili kukomesha vitendo hivyo visijirudie kwa mwaka mwingine wa fedha.

Mkuu huyo amesema kuwa ofisi yake ya mkoa imesikitishwa na upatikanaji wa hati hiyo ya mashaka kwa kuwa Manispaa ya Songea ndiyo kioo cha mkoa mzima ndani ya Ruvuma na ina vyanzo vingi vya mapato ambayo yakisimamiwa hati hiyo isingeweza kupatikana.

“Haiwezekani Rais wetu Dkt ,John Pombe Magufuli anahangaika namna ya kuwasaidia wananchi hasa wanyonge sisi huku tunafanya madudu ya kuiumiza Serikali nasema sitakubali lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya waliosababisha hati hiyo”amesema mkuu huyo Christina Mndeme.

Kwa upande wake mkaguzi wa Nje wa hesabu za Serikali mkoani humo Deogratius Peter amesema Halmashauri hiyo imepata hati hiyo kutokana na sababu moja tuu ya fedha ya sh.Milioni 130 za mapato ziliibiwa zikarejeshwa baadhi ya fedha na kubakia kiasi cha sh.Milioni 98 na zikaingizwa kama sehemu ya mapato wakati hazipo jambo ambalo limepelekea dowa kwenye ripoti za hesabu za serikali.
 
Back
Top Bottom