RC Rukwa sasa kutumia Polisi kudhibiti kipindupindu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
polisi.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesema atalazimika kutumia Jeshi la Polisi kusimamia zoezi la usafi na ujenzi wa vyoo salama katika Kijiji cha Namasinzi, baada ya wananchi hao kushindwa kujenga vyoo hivyo mbali na elimu ya umuhimu wa vyoo waliyopewa kwa muda mrefu.

Wangabo ametoa kauli hiyo wakati yupo katika Mkutano wa hadhara alioufanya kwenye kijiji cha Namasinzi, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga, kijiji ambacho wananchi watatu wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine wakiendelea kupatiwa huduma.

Aidha, Wangabo amesema kuwa ikifikia hatua hiyo Kijiji hicho kitafungiwa na hakuna atakayetoka wala kuingia na hatimaye kusitisha shughuli za kiuchumi za Kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hali itakayopelekea maisha magumu kwa wananchi hao jambo ambalo asingependa litokee.

Katika kuhakikisha hali hiyo haitokei Mh. Wangabo alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule na timu yake ya usafi ya halmashauri kuhakikisha wanapita kaya kwa kaya ili kuzibaini kaya zisizopenda usafi na zisizokuwa na vyoo na kuzichukulia hatua za kisheria kwani kwa kushindwa kufanya hivyo kipindupindu hakitamalizika katika bonde hilo.

"Sasa tutatumia nguvu ya dola, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi katika maisha ya usafi wala sio uchafu na kila mtu ahakikishe kwamba anakuwa na kiboko fulani ambacho ni kigumu amuone mtu anachemsha maji, anayaweka maji yake yanapoa akienda shambani anakwenda na maji mbayo yamekwisha poa, lakini mkilea lea hivi, waswahili wanasema ukicheka na nyani unavuna mabua, mabua ambayo tunayavuna ni vifo",amesema Wangabo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa ameendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka misaada katika bonde hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wataendelea kutoa elimu bila ya kuchoka akiamini kuwa wananchi hao wataelewa wakiendelea kusimamiwa.

Chanzo: EATV
 
Kuchemsha Maji ya kunywa ni utamaduni hata ulazimishe vipi kamwe kuna watu watashindwa.

Ila kutokuwa na choo huo ni uchafu namuunga mkono kwa hili.
 
Watanzania ni wagumu sana wa kuelewa.....yani vitu ni kwa faida yao bado wanataka kubisha....
Kipindupindu kikitokea watasema serikali haiwajali
 
Back
Top Bottom