Mkuu huyo wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelote Steven akionyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho, amesema katika kijiji hicho cha Mpasa kilichoko kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika, kuwa hawezi kuvumilia kuona ugonjwa unakuwepo tangu mei 14, mwaka huu, na watu 92 wameugua ugonjwa huo na kutibiwa kwenye zahanati, huku mmoja akipoteza maisha, na ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya nkasi ikifanya siri nzito bila ya kutoa taarifa popote na kusababisha madhara makubwa.
Pamoja na maamuzi hayo mkuu huyo wa mkoa ameagiza kuundwa kwa kamati ya wataalamu, kufuatilia kwa kina kwanini taarifa hizo zilifichwa kwa muda wote huo, na kusababisha ugonjwa kuenea hadi kwenye wilaya ya jirani ya kalambo mkoani humo.
Chanzo: ITV