RC Rukwa amtumbua mganga mkuu wa Nkasi kwa kuficha taarifa za ugonjwa wa Kipindupindu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
Nkasi3.png
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw.Zelote Steven ameagiza kusimamishwa kazi mara moja, kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Nkasi Dakta Makundi Mazige, kwa kuficha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kijiji cha Mpasa wilayani humo, tangu mei mwaka huu, ambapo mtu mmoja amepoteza maisha na watu zaidi ya tisini kuugua ugonjwa huo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelote Steven akionyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho, amesema katika kijiji hicho cha Mpasa kilichoko kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika, kuwa hawezi kuvumilia kuona ugonjwa unakuwepo tangu mei 14, mwaka huu, na watu 92 wameugua ugonjwa huo na kutibiwa kwenye zahanati, huku mmoja akipoteza maisha, na ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya nkasi ikifanya siri nzito bila ya kutoa taarifa popote na kusababisha madhara makubwa.

Pamoja na maamuzi hayo mkuu huyo wa mkoa ameagiza kuundwa kwa kamati ya wataalamu, kufuatilia kwa kina kwanini taarifa hizo zilifichwa kwa muda wote huo, na kusababisha ugonjwa kuenea hadi kwenye wilaya ya jirani ya kalambo mkoani humo.

Chanzo: ITV
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,215
2,000
Hivi kumbe ma RC nao wana uwezo wa kumsimamisha kazi mtumishi wa umma?
 

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
367
250
du, wakisema pia kuna kutumbuliwa....nakumbuka wakati wa njaa ilikatazwa kuitangaza hali hiyo...pengine na huyo mganga alikuwa anajiogopea maskini....kufanya kazi kwa woga na vitisho kuna athari nyingi kuliko faida!
 

mfungwa

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,291
1,500
Shida ya Africa ni ubabe ubabe. Ukipata mamlaka unadhani kama mbinguni. Weww mwenyewe mkuu wa mkoa unamakosa mangapi, mbona mdomo povu 2. Jiangalie kwanza ww usije ukaanguka. Mwenzako kawahudumia hadi mmoja tu kafariki ongea nae taratibu sio ubavu wa ajabu ajabu huo.
 

Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,418
2,000
Ni tabu tupu, ukitangaza ni shida na usipotangaza pia ni shida! Ni mwendo wa kutafuta kiki tu !
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Kama nikweli mganga huyo ni mzembe
Wale wanaomtetea niwale waliozoea siasa za kubadili rangi nyeupe kuita blue,nyie mnao mtetea nikwakua hajafa ndugu yenu?Bila kuripoti dawa zitatolewaje za kutosha?

Kwani akiripoti ataambiwa amewalisha yeye vinyesi?siwamekula kutokana na sababu mbalimbali?Kwann asiripoti kwa RC?
Weka ndani huyo amesababisha usumbufu mkubwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom