RC Paul Makonda: Halima Mdee anamlinda Ester Bulaya badala ya kuwahudumia Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Salaam Wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda amedai kumshangaa Mbunge wa Kawe Halima Mdee kufanya kazi ya kumlinda Mbunge Mwenzie Ester Bulaya badala ya kuwatumikia Wananchi wa Kawe.

Kwamba haelewi kuna kitu gani kati ya Wawili hao. "Watu wazima mumeelewa, Halima Mdee ametuchukulia nafasi yetu bure" kasema Makonda. Anasababisha Ester haolewi kwani muda wote anamlinda.

Makonda kaongeza kuwa Mbunge wa Kibamba John Mnyika atakuwa Katibu mkuu wa kwanza CHADEMA kuongoza Wabunge wasiofika hata saba wa CHAMA hicho.

Ameyasema hayo Mabwepande katika Ziara ya kukabidhi miradi ya Maendeleo iliyokamilishwa na Serikali awamu ya Tano. Katika Ziara hiyo ambayo ametumia muda mwingi kuwaelezea Halima Mdee John Mnyika kwamba hawajafanya chochote cha maendeleo, aliongozana na Viongozi wa CCM wa mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar.

Maeneo aliyo yatembelea na kukabidhi Miradi ya Maendeleo ni Pamoja na Mradi wa kuchakata takataka Mabwepande, Shule ya Wasichana ya Mwabe ya sayansi, Hospitali ya Wilaya Kinondoni inayojengwa Mabwepande, Kituo cha Afya Bunju, Tank la Maji Makongo na Kituo cha Afya msasani Mkoroshini.

Wakati huo huo Kamanda mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mambosasa, kakabidhi nyumba tisa za Askari huko Mabwepande ambazo zina uwezo wa Kubeba familia 18. Askari wanaoishi kwenye nyumba hizo wamelalamikia Ukosefu wa Maji.


=====

RC MAKONDA AKABIDHI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWENYE JIMBO LA KAWE.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara kwenye Jimbo la Kawe kwa lengo la kukabidhi Miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa Rais Dkt. John Magufuli kupitia ilani ya Chama hicho.

Miongoni mwa miradi aliyokabidhi RC Makonda ni Mradi Mkubwa kabisa wa Kuchakata taka wenye thamani ya Bilioni 5.59 uliopo Mwabwepande, Mradi wa Shule Mpya ya sekondari ya Mabwe Tumaini Girls iliyogharimu Shilingi Bilioni 2.6 na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande yenye thamani ya Bilioni 2.4.

Aidha RC Makonda amekabidhi pia Mradi wa Matank makubwa matano na Pampu za kusambaza Maji zilizopo Changanyikeni, Ujenzi wa Kituo cha Afya Bunju chenye thamani ya milioni 600, Mradi wa Makazi ya Askari Mabwepande pamoja na kukabidhi Zahanati ya Mkoroshini kata ya Msasani yenye thamani ya Milioni 408.

Akizungumza katika ziara hiyo RC Makonda amewahimiza wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi watakaowaletea maendeleo na sio viongozi wanaopinga kila jambo jema linalofanywa na serikali.

Hata hivyo RC Makonda amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kutafuta eneo kwaajili ya kujenga Kituo cha Afya Kawe ili kusogeza huduma za Afya kwa wananchi wa kata hiyo.

Kesho RC Makonda ataendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni.
IMG_20200628_124244_945.jpg
Kutoka kushoto: 1. Aron Kakurumjuli-Mkurugenzi manispaa ya Kinondoni. 2. Harold Maruma- Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar 3. Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar 4. Daniel Chongolo-Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
IMG_20200628_124336_317.jpg
Paul Makonda na Afande Mambosasa
IMG_20200628_124601_808.jpg

RC Makonda alipofika Nyumba za Askari Polisi Mabwepande zinazoonekana kwa nyuma

IMG_20200628_121930_379.jpg
IMG_20200628_112236_920.jpg

Sehemu unapojengwa Mradi Mkuba wa Kuchakata taka
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom