RC Mtwara: Mwendokasi wa Upepo wa Kimbunga Kenneth wapungua, Watu waendelee na shughuli zao

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
RC Gelasius Byakanwa amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejiridhisha kwamba kwa hali inavyoendelea na taarifa za hali ya hewa zinavyosema, haioni kama kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa raia na mali zao

Amesema “Awali, tuliambiwa kuwa majira ya leo saa tisa alasiri upepo wa Kimbunga ungekuwa unavuma kwa mwendokasi wa Kilometa 140 kwa saa lakini mpaka saa tisa na nusu tulipoangalia mwendokasi wa upepo ulikuwa ni Kilometa 50 kwa saa”

Aidha, ameeleza kuwa kwa sasa hakuna mvua tena, hakuna radi, hakuna mawimbi baharini na hivyo kwa kuzingatia hayo pengine na kwa kujumuisha na dua zilizofanyika, balaa hilo linaweza kuwa limetuepuka

Amemalizia kuwa “Tumezingatia vigezo hivyo na kuwaruhusu Wananchi kuendelea na shughuli zao na kufanya kazi zao za msingi”
 
Jiwe umeshindwa kununua vifaa vya kisasa kuangalia hali ya hewa ona Sasa watu wengine wamehama kutoka mikindani mpaka masasi !!kununua wapinzani unaweza poor jiwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom