RC Mtaka: Tumepewa akili za kufikiri na sio za kutishana

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi, Akiwa Katika vikao vya kuanisha vipaumbele mkoani Dodoma, RC Mtaka amesema yeye hayupo pale Dodoma kutisha na Kumtishia mtu bali yupo pale kwa ajili ya kuunganisha akili za watu waliozajaliwa ili kuleta matokeo mazuri mkoani Dodoma

RC Mtaka, Amesema watumishi wa wilaya zote Dodoma wachague vipaumbele vichache hawana haja ya kuwa na vipaumbele vingi.

Akitolea mfano kwa wilaya ya Kongwa kwa Job Ndugai, Mheshimiwa Mtaka amesema Kongwa kuna ng'ombe wengi sana, Lakini Je kipaumbele kiwe nyama au Maziwa au uzalishaji wa ng'ombe zaidi?

Amesisitiza kwa wilaya ya Kongwa hakuna haja ya kushika vipaumbele vyote kwa wakati mmoja, Ni kuchagua kimoja na kuunganisha akili na mawazo ili kupata manufaa

RC Mtaka amesisitiza vipaumbele vikiwa vingi sana vinatutoa kwenye mstari na baadae tunapata matokeo mabaya

RC Mtaka amesisitiza anapenda astaafu kazi kwa heshima na hata watu wakimuona waweze kumsalimia na kucheka pamoja, Amesisitiza watu inabidi waone fahari kuwaona viongozi wao Dodoma

Aidha maeneo ambayo wanalima alizeti RC Mtaka amesema suala sio kulima alizeti tu, Suala ni kujua Katika alizeti kipaumbele ni mafuta au alizeti yenyewe?

RC Mtaka ameeleza kuwa ni muhimu kuzalisha kwa kuangalia soko lipo wapi? Ni soko la ndani au Soko la nje, Na Je kuna uhitaji wa hilo zao sokoni

RC Mtaka amesisitiza kuwa RC Mahenge anayeondoka Dodoma alikuwa mtu mpole na mnyenyekevu sana na hakuwa na walinzi kwenye mambo yake nje ya ofisi kwani aliishi maisha ya kuheshimu watu Dodoma

RC Mtaka amesisitiza anapenda siku akifikisha umri wa RC Mahenge na yeye awe mtu humble na mcheshi sana kama RC Mahenge

Akihoji kama RC Mahenge alikuwa anatembea bila ulinzi, kwanini Mkuu wa wilaya ujaze walinzi
 
CV yake.Natamani angekuwa na ilani yake inayotekelezeka.Siyo kitabu kurasa 320 miaka 60 sasa eti maji maji maji,HALAFU UNASEMA NCHI TAJIRI
Mtaka anapaswa kuwa Mwl chuo cha uongozi tena asipewe ukuu wa chuo.
Chalamila chuo cha Comedian na Vichekesho.
Sabaya na Makonda wanatakiwa mbugani kupambana na majangili
 
Back
Top Bottom