RC Mtaka: Hata mtu mjinga anaweza kuwa na Madaraka na akadharau Sekta binafsi

Mtaka huwa namfananisha na Mfalme Sulemani wa kwenye biblia aliambiwa omba chochote nitakupa, yeye akaomba hekima na busara na MUNGU akampa utajiri wa kutisha na hakunyanyua mabega kama akina Ndugai, Mwigulu, Olesabaya, Makonda na wapuuzi wengine
Huyu RC ni mtu muhimu sana ktk taifa hili. Anakaa sana kuwa rais huko baadae lakini si chama hiki.
 
JPM alieleza jukwaani kwamba Mtaka alikataliwa na vetting. JPM akatumia busara yake na kumpitisha kuwa mkuu wa mkoa. Huyo huyo leo hii ni mwamba bila kumbukumbu ya njia iliyomfikisha hapo alipo. Anaanza kusifia wafanyabiashara na kudhalilisha wanasiasa wenzake. Kwa ufupi yeye anajionesha ni mwelevu sana kuliko wenzake. kiumbe wa aina hii ni hovyo tu!
Unaweza kutuwekea hapa criteria za JPM kwenye vetting?

Kwa kuzingatia baadhi ya wateule wake kama Makonda, Sabaya, Gambo, Happi, Chalamila, Kasesera etc, unaweza kubashiri ni vigezo gani ambavyo JPM alivizingatia kwenye teuzi.
 
Moja kati ya wakuu wa Mikoa wenye hekima na busara ni huyu RC wa Dodoma ndugu Mtaka

Wakati wa kikao cha kuwekeana mkakati mkoani Dodoma RC Mtaka amesisitiza uongozi unapatikana kwa kuchaguliwa kwa kura au kuteuliwa, Lakini kuna wakati wananchi wanaweza kumpigia kura mtu mjinga na akawa kiongozi wao na kujiona Serikali ni kila kitu lakini sio sekta binafsi

Hata hivyo anasema Yawezekana mtu akateuliwa pia akawa mjinga na kuanza kudharau sekta binafsi, Anasema kwake sekta binafsi ni ufunguo wa Maendeleo, Hivyo amewaomba watumishi kuheshimu sekta binafsi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma RC Mtaka anasema viongozi wa Serikali waheshimu sekta binafsi kwani kufanya kazi binafsi kunahitajika akili kubwa, Viongozi wengi wa Serikali hawawezi hata kujiajiri ingawa wanalipwa mshahara Wengine mpaka Milioni mbili, mpaka wakistaafu ndio wanaheshimu sekta binafsi

Suala la elimu amesisitiza viongozi hasa walimu wawafundishe vijana na waone fahari vijana wawe kama wao au zaidi, Amesema wengi viongozi serikalini wamefika pale kutokana na walimu wao, Hivyo kila mtu Dodoma ajisikie fahari kuona vijana wadogo wanasoma na kuwa kama wao kwa ushirikiano
Jamaa ni genius sana
 
Anaye Vet siyo rais, boss! Mbona hata ukimuuliza katibu kata anajua hilo!
 
Wajita wengi niliopata bahati ya kuwaona na kukutana nao katika uongozi wako hivyo kujiona wana akili kuliko wengine, na wanakuwa na udikteta wa kisilisili, na akiwa profesa wengi si katika ujumla bali kwa wale niliokutana nao wajeuri kweli kweli. Wapo wamjuao Ndugu Mtaka kama Mtu mzinzi sana sana sasa sijui wanauzoefu gani nae, ifahamike ametokea Mzumbe kama mwanafunzi na pia akiwa DC Mvomero alizoeleka sana mzumbe na chuo na alikuwa na mazoea ya kuonekana sana mzumbe, alikuwa na duka pia pale samakisamaki morogoro kwa hio yawezkana kama binadamu wapo wanaomfahamu vizuri sana. Viongozi wachunge sana ndimi zao wasijisahau mafaili yao yako kwa watu wasio husiana nao kabisa na hawataona aibu wala huruma kuwaanika na kuwachania taswira zao. Kazi na heshima viendelee na kubebeana kupo.
 
Philosophy ya uongozi bora inamtupa mbali ukiongea nae kwa upana na kwa weredi. Kipindi kolichopita kionhoxi yryote yule sngeweza kuongoza, wilaya, mkoa, hslmashauti, nashirika na hsta vyuo bikuu.

Wakati huu unatakiwa uwezo mkubwa sana wa uongozi kwa kuwa watumishi hawana cha kuogopa ni mwendo wa kuchagua ni yapi ya kuyafanya na kivipi. Muda si mrefu viongozi wengi mtawaona wana pwaya kuliko tulivyo wafikiria huko nyuma.

Na hapa ndipo tutakuja kujifundisha kitu kuhusu uongozi.
Unasoma chekechea!!!???
 
Huyu si ndie alitutangazia ujio wa Disney Simiyu? Kwangu mimi ni kama yule aliyetaka kutuletea wataalam wa mvua.

Amandla...
Boss umenikumbusha mambo ya kufikirika aliyonayo Mtaka. Akisoma kitabu fulani naye anajitangazia ni idea yake. Simiyu ilikuwa maarufu kwa mashindano ya miss ..... baadaye maonesho ya 8-8, kwenda kula miwa. leo hii hakuna hata kitu cha kuonekana kwenye viwanja vya maonesho.
 
Moja kati ya wakuu wa Mikoa wenye hekima na busara ni huyu RC wa Dodoma ndugu Mtaka

Wakati wa kikao cha kuwekeana mkakati mkoani Dodoma RC Mtaka amesisitiza uongozi unapatikana kwa kuchaguliwa kwa kura au kuteuliwa, Lakini kuna wakati wananchi wanaweza kumpigia kura mtu mjinga na akawa kiongozi wao na kujiona Serikali ni kila kitu lakini sio sekta binafsi

Hata hivyo anasema Yawezekana mtu akateuliwa pia akawa mjinga na kuanza kudharau sekta binafsi, Anasema kwake sekta binafsi ni ufunguo wa Maendeleo, Hivyo amewaomba watumishi kuheshimu sekta binafsi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma RC Mtaka anasema viongozi wa Serikali waheshimu sekta binafsi kwani kufanya kazi binafsi kunahitajika akili kubwa, Viongozi wengi wa Serikali hawawezi hata kujiajiri ingawa wanalipwa mshahara Wengine mpaka Milioni mbili, mpaka wakistaafu ndio wanaheshimu sekta binafsi

Suala la elimu amesisitiza viongozi hasa walimu wawafundishe vijana na waone fahari vijana wawe kama wao au zaidi, Amesema wengi viongozi serikalini wamefika pale kutokana na walimu wao, Hivyo kila mtu Dodoma ajisikie fahari kuona vijana wadogo wanasoma na kuwa kama wao kwa ushirikiano
Naona huyu jamaa kailewa signature yangu vizuri sana, "Changamoto kubwa sana inayoyakabili mataifa masikini duniani na kufanya washindwe kuendelea ni nyingi ya akili ndogo kupewa mamlaka makubwa, kwa njia ya kura au kuteuliwa"
 
Najua ulileta hadithi za mitandaoni. Kama alipenda kujieleimisha mbona njia ya shule yake ni hovyo tu!

Kuna watu wanachekesha sana. Ile approach ya ukali na ubabe ndio wanaona kama ni namna ya kuongoza watu. That is very temporarily.
Tujenge system ambazo zinajitegemea na kulinda maslahi ya viongozi na wanaoongozwa.
Haya mambo yenu ya kufikiri kukaa kwenu kwenye nafasi za maamuzi ndio the best cream ni kujidanganya nafsi.
Hayupo wala hatakaa kutokea binadamu wa aina hiyo.
Ole Sabaya ni mfano wa wazi. Bado wengine wengi kwenye taasisi nyingi za umma. Just note..
Shoka liko shinani
 
Anaye Vet siyo rais, boss! Mbona hata ukimuuliza katibu kata anajua hilo!
Nimeuliza hivyo si kwamba sielewi ninacho uliza. Huyo JPM kwa maneno yake mwenyewe mara kadhaa alikiri wazi wazi kupuuza taratibu na miongozo iliyopo kikatiba na kujifanyia mambo kwa utashi wake.

Wewe mwenyewe unakiri kuwa alisema Mtaka alikataliwa kwenye vetting ila yeye akamteua kwa utashi wake, kukataliwa na 'vetting' maana yake yeye alimteua nje ya 'merits'.

Nimekupa mifano michache ya wateule wake uitumie kama reference kujibu at all kama kuna vetting inafanyika vilitumika vigezo gani kuteua hayo 'maboga'?! Je ilikuwa ni 'vetting system' au ndio walipatikana kwa utashi wa Mwendazake wa kupuuza vetting recommendations?
 
Lini vetting iliwahi kuleta viongozi wa maana? Toa mfano wa viongozi wa maana unaowafahamu, waliopatikana kwa vetting nzuri. Woote walioiba enzi za Kikwete walifanyiwa Vetting! Woote waliouza mashirika ya umma wakati wa Mkapa, akina Lubambe na timu yake walifanyiwa Vetting. Hata mawziri wezi wa enzi za Nyerere walifanyiwa vetting. Wengine hadi kuwa mawaziri wakuu na tabia zao za ukabila na upendeleo.
 
Two wrongs don't make a right, kwamba unataka kumtetea JPM kuwa alikuwa sahihi kuteua viongozi wa hovyo kwa kigezo kuwa vetting system ilileta viongozi ambao walifanya vibaya baadae?

Labda kama wewe ndio huelewi how vetting works, vetting inazingatia reputation na integrity ya muhusika kwa siku za nyuma kabla ya kumpendekeza. Anaye pendekezwa akibehave 'vibaya' huko mbeleni bado huwezi kuilaumu vetting kwa kuwa people are subject to change.

In fact hata yeye ni matokeo ya vetting mbovu plus 'ujinga wake' binafsi alio amua kuupractice akiwa in power.

Of all the Presidents nadhani JPM holds a record when it comes to 'tumbua-teua', na bado hadi anaelekea kaburini hakuwahi kufanikiwa kuteua viongozi wa maana na mwishowe alianza kurudia 'matapishi' alio aminisha umma kuwa aliwatumbua kwa utendaji mbovu. Finally, the man became a failure of his own vetting.
 
Back
Top Bottom