RC Mtaka: Hata mtu mjinga anaweza kuwa na Madaraka na akadharau Sekta binafsi

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
172
1,000
Moja kati ya wakuu wa Mikoa wenye hekima na busara ni huyu RC wa Dodoma ndugu Mtaka

Wakati wa kikao cha kuwekeana mkakati mkoani Dodoma RC Mtaka amesisitiza uongozi unapatikana kwa kuchaguliwa kwa kura au kuteuliwa, Lakini kuna wakati wananchi wanaweza kumpigia kura mtu mjinga na akawa kiongozi wao na kujiona Serikali ni kila kitu lakini sio sekta binafsi

Hata hivyo anasema Yawezekana mtu akateuliwa pia akawa mjinga na kuanza kudharau sekta binafsi, Anasema kwake sekta binafsi ni ufunguo wa Maendeleo, Hivyo amewaomba watumishi kuheshimu sekta binafsi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma RC Mtaka anasema viongozi wa Serikali waheshimu sekta binafsi kwani kufanya kazi binafsi kunahitajika akili kubwa, Viongozi wengi wa Serikali hawawezi hata kujiajiri ingawa wanalipwa mshahara Wengine mpaka Milioni mbili, mpaka wakistaafu ndio wanaheshimu sekta binafsi

Suala la elimu amesisitiza viongozi hasa walimu wawafundishe vijana na waone fahari vijana wawe kama wao au zaidi, Amesema wengi viongozi serikalini wamefika pale kutokana na walimu wao, Hivyo kila mtu Dodoma ajisikie fahari kuona vijana wadogo wanasoma na kuwa kama wao kwa ushirikiano
 
evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,000
2,000
Huyu jamaa ana hekima na busara naiona Dodoma iliyoneemeka, alianza na simiyu alikuwa anaipeleka vizur ana mikakati yake binafsi ambapo huwa namkubal, mtaka haamini ktk kushindwa jambo, anaamini ktk kushinda, ni moja ya viongo wachache wanaopenda kupata maarifa yaliyofichika ktk vitabu
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061

Kweli tupu
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,438
2,000
Moja kati ya wakuu wa Mikoa wenye hekima na busara ni huyu RC wa Dodoma ndugu Mtaka

Wakati wa kikao cha kuwekeana mkakati mkoani Dodoma RC Mtaka amesisitiza uongozi unapatikana kwa kuchaguliwa kwa kura au kuteuliwa, Lakini kuna wakati wananchi wanaweza kumpigia kura mtu mjinga na akawa kiongozi wao na kujiona Serikali ni kila kitu lakini sio sekta binafsi

Hata hivyo anasema Yawezekana mtu akateuliwa pia akawa mjinga na kuanza kudharau sekta binafsi, Anasema kwake sekta binafsi ni ufunguo wa Maendeleo, Hivyo amewaomba watumishi kuheshimu sekta binafsi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma RC Mtaka anasema viongozi wa Serikali waheshimu sekta binafsi kwani kufanya kazi binafsi kunahitajika akili kubwa, Viongozi wengi wa Serikali hawawezi hata kujiajiri ingawa wanalipwa mshahara Wengine mpaka Milioni mbili, mpaka wakistaafu ndio wanaheshimu sekta binafsi

Suala la elimu amesisitiza viongozi hasa walimu wawafundishe vijana na waone fahari vijana wawe kama wao au zaidi, Amesema wengi viongozi serikalini wamefika pale kutokana na walimu wao, Hivyo kila mtu Dodoma ajisikie fahari kuona vijana wadogo wanasoma na kuwa kama wao kwa ushirikiano
We unaamini ana busara sana? Uliiona wapi busara ya mzinzi huyu?
Naangalia hayo uliyoandika kwamba ndo maneno yake. Angalia kama yanaonesha busara yoyote! Yeye anaamini sekta binafsi haina wajinga. Wajinga kwa kigezo chake ni watu wa aina gani? Yawezekana wewe unayemsifu unaelewa maana ya wajinga wa Mtaka. Tunayo mambo yake mengi ya hovyo sanaaa! Ishia hapo!
 
GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,042
2,000
Kiongozi hupimwa kwa maneno, vitendo msimamo wake kwa muda usiopungua mwaka. Kwa kipindi nilichoanza kumsikia Mtaka ni wazi kuwa ana kitu cha ziada!!... Hata kama ana mapungufu kama mdau mmoja alivyonadi hapo juu .... Bado Mtaka ni kiongozi mzuri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom