RC Mrisho Gambo wa Arusha kama Wewe ndiyo umehusika Kuiondoa Arusha United katika Ligi nakuvua Sifa ya Kiongozi bora

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,793
Baada ya hili Sakata zima la Timu ya Arusha United a.k.a Wana Utalii ya Mkoani Arusha ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na iko chini ya Mlezi wao Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisaidiwa kwa karibu na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ‘ Kujitoa ‘ katika Ligi hiyo Kinyume na Sheria na Kanuni za Ligi, TFF, CAF na hadi FIFA niliamua kwenda ndani zaidi kujua nini kinaendelea na nilichokipata kwakweli kimenishtua na kunisikitisha mno tu.

Huku sababu Kuu ya Timu hiyo ( Arusha United ) Kujitoa wakisema ni Uonevu ambao wamekuwa wakifanyiwa pindi wanapoenda Kucheza Mechi zao za Ligi Vituo vingine ukweli ambao bado naendelea Kuuthibitisha unasema kwamba wala tatizo siyo Wao Kuonewa ila ni Jambo la Kisiasa zaidi hasa likimuhusisha moja kwa moja Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo.

Kama leo hii Timu zote duniani zingekuwa zikiona zinaonewa tu Uwanjani basi zinajitoa Mashindanoni nadhani huu Mpira usingechezeka na kuwa na Maendeleo hivi bali wale wenye Kuujua Mpira na Changamoto zake za ndani na nje ya Uwanja hata kama wakionewa huwa ‘ hawadeki ‘ hovyo au ‘ Kulialia ‘ na ‘ Kujitoa ‘ isipokuwa huwa wanapeleka ‘ Malalamiko ‘ yao sehemu husika ili yafanyiwe Kazi huku Wao wakiendelea na Mashindano.

Mwaka 1986 wakati wa Mechi kati ya Argentina na Uingereza katika Kombe la Dunia Mshambuliaji Nguli na Mahiri kabisa Diego Armando Maradona alifunga Goli la Mkono na wakachukua Ubingwa lakini pamoja na Wachezaji wa Uingereza kulilalamikia lile Goli wala hawakujitoa bali walicheza hadi mwisho.

Miaka ya hivi karibuni hii ya 2000 wenye Kumbukumbu zaidi mtanisaidie kuniwekea hapa Thiery Henry a.k.a Chogo Chemba nadhani katika Michuano ya Kombe la Ulaya au la Dunia Ufaransa ikiwa inacheza alifunga Goli kwa kujipasia mpira na Mkono wake na japo Wachezaji wa hiyo Timu Pinzani walilalamika ila hawakujitoa na waliendelea na Mashindano hadi tamati yake.

Arusha United FC wao ni nani hapa Tanzania kwamba wanataka wapate ‘ Special Treatment ‘ kutoka TFF kwa Makosa / Mapungufu ambayo kwa Taarifa nilizonazo GENTAMYCINE zinasema kwamba hata Wao ( Arusha United ) wakiwa wanacheza katika Uwanja wao wa Nyumbani wa Sheikh Amri Abeid Kaluta huwa wanawafanyia ‘ Vitimbi ‘ vingi Wapinzani Wao hadi wanashinda mechi zao sasa kwanini Wao wakifanyiwa wanaanza Kulalamika, Kudeka na Kulialia hovyo?

Kama kweli haya maamuzi ya Arusha United ‘ Kujitoa ‘ yameshinikizwa na Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo basi GENTAMYCINE nasema ni Maamuzi ya ‘ Kipumbavu ‘ ambayo hayajapata kutokea duniani na si tu kwamba yamemdhalilisha Mkuu wa Mkoa huyo bali yameudhalilisha sana Mkoa wa Arusha ambao una Watu makini, wastaarabu na ambao walikuwa na ‘ Passion ‘ kubwa ya Kuupenda Mchezo wa Soka / Kandanda.

Na hapa niwaombe tu TFF kuwa wakikaa Kikao chao cha Kuijadili Arusha United FC na Maamuzi yao haya ya Kipumbavu na Kishamba kabisa wala wasipoteze muda bali waifungie Maisha hii Timu ili iwe Fundisho kwa Timu zingine zenye ‘ Upumbavu ‘ kama huu walioufanya hawa Wapuuzi. Mpira unachezwa Uwanjani na siyo Mezani au kwa Mbeleko.

Kwa taarifa za ndani kabisa zinasema kwamba moja ya sababu ya Wao Kujitoa ni baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuoana kwamba Timu hiyo haina tena nafasi ya Kupanda Ligi Kuu kwa mwaka huu na kwamba Mkuu huyo wa Mkoa hatoweza tena Kuitumia kama Ngazi yake ya Kisiasa hasa katika Uchaguzi Mkuu ujao ambapo sasa siyo Siri tena kwamba Mkuu huyu wa Mkoa anataka Kugombea hilo Jimbo.

Zingine za chini chini zinasema ya kwamba mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuona ya kwamba tayari kuna Mtu mwingine ameshaandaliwa ‘ Kugombea ‘ Ubunge hapa na anakubalika kuliko Yeye basi ameamua Kuutumia huu huu mwanya wa hii Timu ili ‘ Kuitoa ‘ Mashindanoni katika Ligi Daraja la Kwanza ili tu ikipanda isije Kumpa ‘ Kiki ‘ na ‘ Manufaa ‘ huyo ambaye Chama chake Kinapendelea ndiye awe Mgombea.

Binafsi kama GENTAMYCINE na kutokana pia na ‘ Kujichanganya ‘ Kwangu huku na kule bila kusahau kuwa hata Arusha pia nina ‘ Wadau ‘ wangu nimwambie tu Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kwamba wakati Yeye akiishutumu TFF kuwa inalea ‘ Uonevu ‘ katika Mechi zao na Timu Pinzani ila asisahau hata Yeye pia kama Mkuu wa Mkoa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wanatuhumiwa kupanga ‘ Mikakati ‘ mingi ya Kuzihujumu Timu walizokuwa wakicheza nazo na tayari kuna Watu wana Ushahidi juu ya hili hivyo sijui ‘ Bomu ‘ hili likilipuka rasmi Arusha United FC, Mrisho Gambo na Jerry Muro watajifichia wapi kwani ni aibu tupu.

Niwaombe tu Arusha United FC kutengua haya Maamuzi yao, waombe radhi kwa Wadau wote na hasa wana Mkoa wa Arusha wenye Timu yao na waendelee na Ligi kwani Kujitoa Kwao huku kunawadhalilisha mno na Wanaonyesha ni jinsi gani wasivyo wavumilivu naWatu waliokomaa. Kuomba Radhi kwa ' Kukengeuka ' juu ya Maamuzi yenu siyo dhambi ila mkae mkijua ya kwamba Sisi Wadau wa Michezo hapa huu wa Mpira wa Miguu kwa haya Maamuzi yenu tumeshawadharau mno kama si sana tu.

Nawasilisha.
 
Wapo kundi gani hawa Wana utalii?? Na mechi gani wanalalamikia??

Kama wapo kundi moja na Geita sport wanahaki ya kujitoa kwenye mashindano!

Niliwahi kuhudhuria mechi moja Tu ya Geita sport pale nyankumbu girls nilichokiona sikutamani tena kurudi hata mechi iwe bureeee, MTU anashika Mpira katikati ya uwanja inatengwa penalty???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwa taarifa yako tu ni kwamba hawa Arusha United wamefanya zaidi ya haya na kuna Watu wana mpaka Ushahidi na muda ukifika kuna Watu watamsababisha Rais ' awatumbue ' katika Nafasi zao.
 
Ligi daraja Kwanza sio lelemama .

Hahaa...
Umenikumbusha kuna Mechi mpira ulipita juu ya goli...refa kaweka Kati...anyway sio sababu ya kujitoa, fitna zipo kwenye mpira hasa wa bongo ndio usiseme!
 
Wapo kundi gani hawa Wana utalii?? Na mechi gani wanalalamikia??

Kama wapo kundi moja na Geita sport wanahaki ya kujitoa kwenye mashindano!

Niliwahi kuhudhuria mechi moja Tu ya Geita sport pale nyankumbu girls nilichokiona sikutamani tena kurudi hata mechi iwe bureeee, MTU anashika Mpira katikati ya uwanja inatengwa penalty???

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh
nimecheka kwa sauti sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwa taarifa yako tu ni kwamba hawa Arusha United wamefanya zaidi ya haya na kuna Watu wana mpaka Ushahidi na muda ukifika kuna Watu watamsababisha Rais ' awatumbue ' katika Nafasi zao.
Kwenye taarifa yako ongezea jinsi Hamis Tambwe alivyowanawa na kuwapima oil Mikia pale Taifa mpaka mkang'oa viti. Naona umeongelea ya wakina Maradona na Henry na kumsahau Tambwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usicheke kuna Mambo ya hovyo vibaya Sana aisee, hawaruhusu mpiga picha yeyote kuingia uwanjani, Kwa ufupi kuna utekaji unafanyika ndani ya ligi daraja la Kwanza, hata kurekodi video kwa simu hawaruhusu!

Timu zinahujumiwa tff wapo tuuu wanaangalia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi kuna Timu iliyocheza michezo michafu katika mechi zake hizo kama hiyo hiyo ya Ausha United iliyojitoa? Watafute Wadau wa Mpira na hasa hasa Waandishi wa Habari za Michezo wa hapo hapo Mkoani Arusha na hapa Dar es Salaam wakupe na mengineyo ambayo huyajui. Kifupi tu ni kwamba Timu zote zinafanya na kufanyiana ' Umafia ' wa hali ya juu isipokuwa hao Arusha United wako ( unaoonekana kama vile Kuwatetea ) kuna mahala wamezidiwa ' Ujanja ' na Wenzao ndiyo maana unawaona sasa wanaweweseka hivyo hadi wamechanganyikiwa na kujikuta ' wamejitoa ' Mashindanoni.
 
Kama vyura walivyomfanyia vurugu Rais mstaafu Mwinyi wakipinga goli la kwanza katika kipondo cha goli 4 dhidi ya Simba.
Hahah tisha sana mkuu. Umenikumbusha Simba alipokula goli 4 half time akatomea kusikojulikana.
 
Hahah tisha sana mkuu. Umenikumbusha Simba alipokula goli 4 half time akatomea kusikojulikana.
Wacha kuzua wewe Chura.Mechi hiyo ilichezwa lini na wapi? Lete details. Usifikiri JF ni kikao cha ghahwa ambacho utazua tu.
 
Wapo kundi gani hawa Wana utalii?? Na mechi gani wanalalamikia??

Kama wapo kundi moja na Geita sport wanahaki ya kujitoa kwenye mashindano!

Niliwahi kuhudhuria mechi moja Tu ya Geita sport pale nyankumbu girls nilichokiona sikutamani tena kurudi hata mechi iwe bureeee, MTU anashika Mpira katikati ya uwanja inatengwa penalty???

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahahahahahahaha noma sana nakumbuka msimu uliyopita nilikuwa naaangalia mshikemshike nakumbuka kuna refa alipigwa ngumi moja matata na goalkeeper sikumbuki ilikuw ni mechi gan lakin ilikuwa ligi daraja la kwanza.....

Nilisikitika sana...
 
Haikuwa sahihi Arusha United kujitoa ila TFF inaifanya ligi hii kama ligi ya mchangani zaidi ya ndondo cup.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom