RC Mrisho Gambo: Serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga

nshafiwa na ndugu sana...sikuona wanasiasa...au wanaoleta siasa msibani...na wakifanya hivyo nitawafukuza

Labda Mkuu wa mkoa alikuja.Maana hamuwezi Kijani misiba mpaka mkuu wa mkoa aseme.
 
Kwa kweli ni aibu hadi unatamani kulia. Hebu pita vyuo vikuu uone jinsi vijana wasivyoweza kujadili mambo kwa hoja! Yaani inafika mahali wakipewa boom wanaona eti serikali imewajali kumbe ni haki yao!! Ukiwakuta wanasifia mpaka unapata gadhabu!! Vijana walitakiwa kupewa wanza nafasi ndogo ndogo ili kuwaandaa waje kushika madaraka makubwa wanapofikia miaka 40 na kuendelea. Ukilinganisha wakuu wa mikoa ambao walianzia nafasi za chini utaona jinsi wanavyofanya kazi zao kwa weledi!!
Ukiona mtu ajui kutofautisha kati ya HAKI na WAJIBU ni tatizo kubwa sana na ndio wasomi wengi na vijana wengi wa Tanganyika bado wanaamini katika nguvu ya Ufahamu badala ya nguvu ya Akili ktk maisha yao ya kila siku
 
safi sana rc gambo. wacha wajaze server za jf tu Hawa washabiki wa team matusi.
 
Unafahamu kua serikali kuna kitu kinaitwa kamati ya maafa kwa ngazi ya wilaya mkoa na hata taifa??...kwa kukusaidia mwenyekiti wa kamati ya maafa kwa ngazi ya mkoa ni mkuu wa mkoa.

Hiyo Kamati ilitoa shilingi ngapi au ndiyo ilikuwa pesa za Rambirambi??

Ni aibu kwa kijana mdogo kama Gambo kula pesa za Rambirambi.
 
Huyu RC kama yupo humu jamvini ajijue yy ni kilaza sana, tena sana sio kibaya ambacho viongozi wa dini na waandishi wa hbr walichokifanya, mtu kutoa rambi rambi lazima kuzipitishia kwake?mm nataka nitoe directly.Au kuna sheria yoyote inaratibu mambo ya misiba na utoaji wa rambi rambi
 
Ni serikali ya tanzania tu inayokula rambirambi za wananchi, ikiambiwa ukweli inajifanya kutumia nguvu ya dola
 
Ni kweli kabisa kuwapa madaraka vijana ni kujenga chuki na upuumbavu tu,wengi hawana busara zaidi visasi na ubishoo.

Kama wakuu wa wilaya wa awamu ya Tano hawana Management and administration skills,wao ni kick na kujionyesha kwa Mfalme kwamba wanaweza kuwakomoa Wapinzani bila kujua wanajikomoa wenyewe.Maana chuki na hasira ni juu ya Rais zaidi kuliko wao.
 
Eti ndo watu wanasema vijana wapewe madaraka!! Upumbavu mtupu. Ina maana watu kutoa rambi rambi imekuwa siasa? Serikali inapewa michango yenyewe inawapiga panga waathirika kwa nini tuendelee kupitishia michango yetu huko? Ujinga wa kiwango cha PhD huu!!
Mimi ni miongon mwa Watu waliokuwa wanapinga Vijana kupewa Madaraka kama Ukuu wa Wilaya na Mkoa,nilikuwa natambua ni vyeo vya heshima na vinavyohitaji hekima na busara katika kuwaongoza Watu wa eneo husika,sikuzoea kuona upuuz unaofanywa na hawa viongoz sasa nimeuona,kipindi cha hapo nyuma kulikuwa hakuna mgogoro wa Mkuu wa Wilaya/Mkoa na Wananchi au na Viongoz kila mmoja alitambua majukumu yake lakini sasa tunashudia miongon mwa viongoz hawa wanakula mpaka rambi rambi za wafiwa,hii ni laana,pesa zetu za miradi zitakuwa salama?,najaribu kujiuliza bila majibu
 
Huyu RC kama yupo humu jamvini ajijue yy ni kilaza sana, tena sana sio kibaya ambacho viongozi wa dini na waandishi wa hbr walichokifanya, mtu kutoa rambi rambi lazima kuzipitishia kwake?mm nataka nitoe directly.Au kuna sheria yoyote inaratibu mambo ya misiba na utoaji wa rambi rambi

Hasira yake.ilikuwa juu ya Mayor kwanini aalikwe.Na baada ya kutaka kulazimisha kupewa pesa akanyimwa hasira Mara mbili.

Ni aibu sana sana.
 
Hadi biashara ya machangu??? Naona wamejaa sana mjini.... Na mauaji ya KIBITI? Maana unasema kila kitu
kwa nini unaita uhalifu kuwa ni biashara?
mauaji na uchangudoa ni uhalifu..elewa hilo kwanza kabla ya kuwa Nyumbu.
 
Back
Top Bottom