RC Mrisho Gambo: Serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga

Nawaza msinipopoe mawe....! Hivi kiuhalisia rambirambi wanapewa wanafamilia ama shule walipokuwa wanasoma wanafunzi! Sasa kama ni wanafamilia kwa nini hao watoa rambirambi hawaendi nyumbani kwa wafiwa wanaamua kwenda shuleni? Ukizingati mkuu wa shule yuko matatani kutokana na tukio hilo. Hamuoni kuwa hao kwenda pale kunaweza kuathiri mwenendo wa kesi dhidi ya wahusika wa shule ? Gambo anaweza kuwa sahihi sema ameshindwa kujenga hoja.
Tatizo lako ni shule au uelewa tu kaka. Walioenda kutoa pole ni umoja wa wamiliki wa shule binafsi Tanzania. Huyo mwenye shule ni mshirika wao, sasa wangepelekaje rambirambi kwa wafiwa? Hujui kuwa huyu mwenye shule ndiye mfiwa nambari moja upande wa wanachama wenzake? . Kuna watu hawana akili tu, wanajifanya kuzidiwa na mahaba ya vyama vyao. Hao watu wana haki ya kumtembelea mwanachama wao, wana haki ya kutoa rambirambi kwake, na wana haki ya kumpa kila mfiwa rambirambi yake mkononi. Hata hao wanaitwa viongozi wa dini wako kama sehemu ya wanachama lakini Meya amekaribishwa ,sasa kosa ni nini hapo?
 
Serikali mkoani Arusha imewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima. Aidha amesema serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.
rc%2B1.jpg

Chanzo: www.mitandaoni.co.tz

HAKUNA.... mimi sitafuata huo utaratibu wako Bwana Gambo ama upende au usipende.....!!

Mimi na familia yangu, rafiki zangu na yeyote atakayekubaliana na mimi tutakwenda kutoa rambirambi zetu moja kwa moja kwa wafiwa halafu tuone utatufanya nini sasa, allah......

Tutoe rambirambi zetu kwa utaratibu mliouweka huku tukitambua kuwa mnakwenda kutia mifukoni mwenu na kwenye kanga za wake zenu na kisha kwenda kuzila ???

Aisee, it is impossible !!

Unachoweza kufanya na kilicho ndani ya uwezo wako ni kulazimisha taasisi zenu za kiserikali/umma kuwaletea hizo rambirambi lakini siyo sisi watu binafsi.....period !!!!
 
Serikali mkoani Arusha imewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima. Aidha amesema serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.
rc%2B1.jpg

Chanzo: www.mitandaoni.co.tz
Huko nyuma hutukuona mambo kama hayo ktk misiba hakiuwepo ila kwa utawala tutaona mengi sana. Basi ikitokea hivyo serikali lichukue jukumu hilo kwa misiba inavyotokea kwa mtindo huo
 
BASI WANGETUNGA SHERIA YA UTOAJI RAMBIRAMBI...
hihihiiii
dudu na wanawe.
 
Serikali mkoani Arusha imewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima. Aidha amesema serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.
rc%2B1.jpg

Chanzo: www.mitandaoni.co.tz

Gamble, acha ku gamble, weka hapa vigezo uanvyotumia kutambua nia za watu kabla hazijatekelezwa kama hao unaosema walitaka kuingiza siasa kwenye misiba!.

Gamble, weka hapa sheria inayosema siasa ni jinai.

Gamble, eleza wewe unajitofautishaje na siasa unapofanya uharamia wa sheria za nchi kwa maslahi ya chama chako.

Gamble, ninafahamu unaelewa vizuri sana historia.

Ulizaliwa, unafamilia hata kama huna watoto, unandugu zako wa karibu.

Tambua uko chini ya Utawala wa Mungu!.
 
Huko nyuma hutukuona mambo kama hayo ktk misiba hakiuwepo ila kwa utawala tutaona mengi sana. Basi ikitokea hivyo serikali lichukue jukumu hilo kwa misiba inavyotokea kwa mtindo huo

Ni kwa sbb viongozi chini ya utawala huu hawajioni kuwa wako ktk nafasi zao kihalali....

Hawaamini kuwa wana legitimacy ya umma kutawala, hawana uhakika kama kweli wapo hapo kwa kukubaliwa na umma....

I am sure, wanaamini kuwa wapo hapo kama kwa "zari la mentali tu" ........kuokota embe dodo chini ya mkuyu !!!

Na kwa kuwa wako ktk sintofahamu hiyo, basi wanatumia kila njia ziwe mbaya ama halali kulinda uhalali wao na pale inapolazimu hata kwa kuvunja sheria ama kuharibu taratibu za kawaida za kijamii na hata kumwaga damu....!!

Huu ni utawala wa kujihami tu kila siku, kila eneo.....!!
 
Hiyo Kamati ilitoa shilingi ngapi au ndiyo ilikuwa pesa za Rambirambi??

Ni aibu kwa kijana mdogo kama Gambo kula pesa za Rambirambi.

Serikali ilitoa zaidi milioni 100....unapozungumzia TANAPA,NSSF etc ujue ni serikali hiyo ni entities za serikali
 
Pia posts zangu zote katika uzi huu baada ya hii uliyonukuu utaelewa kama tatizo langu ni shule ama shule ni tatizo lako!
Tatizo lako ni shule au uelewa tu kaka. Walioenda kutoa pole ni umoja wa wamiliki wa shule binafsi Tanzania. Huyo mwenye shule ni mshirika wao, sasa wangepelekaje rambirambi kwa wafiwa? Hujui kuwa huyu mwenye shule ndiye mfiwa nambari moja upande wa wanachama wenzake? . Kuna watu hawana akili tu, wanajifanya kuzidiwa na mahaba ya vyama vyao. Hao watu wana haki ya kumtembelea mwanachama wao, wana haki ya kutoa rambirambi kwake, na wana haki ya kumpa kila mfiwa rambirambi yake mkononi. Hata hao wanaitwa viongozi wa dini wako kama sehemu ya wanachama lakini Meya amekaribishwa ,sasa kosa ni nini hapo?
 
Waingilie hata ndoa zetu . . ?
Hata rambirambi . . ? Hata vikao vya sendoff na harusi . . ?

Ama kweli wewe ni JINGA LAO . .
Hapo kwenye Rambirambi 'Serikali nadhani ijitathamini' haija kaa sawa km serikali itaingilia rambirambi basi liwekwe vizuri kisheria
 
Watu wanasaidia ndg zao kuwachangia nyie mnawakamata wanaochangia maw kuwaweka ndani ili wasichangie na kuwasidia ndg zao mnakazana kufuata utaratibu, acha nisiendelee kuongea mengine acha ni fute ila nadhani kwa sasa Tanzania tuna viongozi wa hovyo sana na hii ni moja ya miongoni mwa maajabu saba ya Dunia ya viongozi wapatikanao hapa Nchni pekee
 
Mkuu kwani haiwezekani watoa rambi rambi wakatumia shule kwa ajili ya urahisi wa kuwafikia wafiwa? Hebu fikria kwa Arusha mmoja awe Kwa Mromboo, mwingine awe Usa River, Mwingine Meserani au Makuyuni. Huoni itakuwa kazi sana kuwafikia? Gambo amejikanyaga sana katika hili!
Kwa Hiyo hao wazazi na Meya na wenye Shule wengine WANa mm-support Mwenye Shule kwa kuwa na gari lilobeba wanafunzi wengi kupita kiasi, lisilo na insurance na mengineyo ambayo hatuyajui kisa siasa ???
 
All in all Hakuna tatizokwa ninavyoona. Wapeleke kwenye mamlaka husika zitashughulikiwa tu.
Mamlaka siyo kuwekwa kama picha ukutani. Mamlaka ni kukubalika na wanaoitii hiyo mamlaka kwa muafaka wa utekelezaji mamlaka yenye dhamira njema.
 
Back
Top Bottom